Tuesday, March 31, 2009

ACCIDENTS!















U.S. Airways pilot Chesley Sullenberger III, safely landed a US Airways airbus 320 jetliner in the Hudson River, All 155 people aboard the airplane survived.
In the pictures, Airline passengers on the wings of the aircraft wait to board a ferry to be rescued. The jetliner safely ditched in the frigid waters of the Hudson River in New York, Thursday Jan.15, 2009 after a flock of birds knocked out both its engines
(from phototricks blog)

Train Passengers Must be Assured of their Safety!

It is becoming increasingly unsafe to travel by train these days. The frequeency at which train accidents happen in the country's railway network, leaving many dead and injured in the process, is just too alarming.
The latest accident to happen occured on Sunday in which a passenger train from Dar es salaam to Mwanza and kigoma hit a stationary goods train that had stopped on the same track due to some mechanical problem near Mpwapwa. Several passengers were killed while many more were injured.
This country has seen worse in train accidents. Memories linger of two such major accidents in which almost 400 passengers killed and hundreds others injured some of them maimed for life.
The earlier one happened in the 1980s at Salanda hills Singida Region while the other took place at Igandu Hill near Dodoma Municipality in June 2002 due to break failure.
The government put the figure of the dead from the Igandu hill accident at 281. There have been other minor accidents, involving mostly goods trains that had derailed, the most fatl one happening near Tabora in 2007 in which 71 people were injured, 15 of them seriously.
Police in the region then arrested 9 people, including 6 locomotive drivers, after being suspected of sabotaging a section of the central railway line in which the train was derailed.
In all the cases mentioned, the government formed probe teams to look into the possible causes. Terms of reference had included possible sabotage, vandalism, safety laxities on the part of railway authorities and dilapidated network.
All the above points to the fact that there was, and still there is, glaring mismanagement and operational incapability on the part of the managers of the country's railway system. In sharp contrast with the past when railway transport was the safest, it is no longer so.
There is complete lack of maintanance of the wagons and the railway system is dilapidated. Lack of safety measures along the railway lines is right, left and centre criminal. The system is in shambles. The government must do something fast to check such deterioration and assure passengers of their safety(From The Daily News).
News Update: Train Accident in Dodoma:
The BBC reports that the train accident that occurred in two days ago in Dodoma could have been deliberately caused so that petrol could be stolen from the fuel tanks.
The BBC reports that seven people have been arrested, including the driver of the cargo train and the station master.
If this is true, then a life of a Tanzanian is completely worthless. It is unimaginable that people would derail a train killing so many people, causing so much damage for just a few gallons of fuel.
But in Bongoland anything is possible.The spate of Albino killing for witchcraft purpose is a recent reminder of how low in morals Tanzanians have become.We have become so obsessed with money and wealth that we are prepared to sacrifice morals and even kill to achieve our goals (From Dr.Faustine's Baraza).
Yes!: I do agree,this is disgusting. it seems the only vocabulary dominating the brains these days is "Money" that is why people kill for money. Think of Albino killings and now this?

Monday, March 30, 2009

KWA MTAJI HUU, TUTAZIDI KUPUKUTIKA!


Jamani ajali! Jamani Ajali! Kwa mtindo huu ajali zitakaa mbali na sisi kweli? Labda malaika washuke kutusaidia. Hawa jamaa juu ya gari wanaonekana hawana wasi kabisa!(picha toka glob ya mdau Maggid Mjengwa).

Sumatra ytakiwa Kuchukua Hatua Temeke!

Wakazi wa Temeke Mwisho jijini Dar es salaam wameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) kuzichukulia hatua kali za kisheria daladala zinazogoma kutumia kituo kipya cha Temeke Mwisho.
Wakizungumza na mwananchi, wakazi hao walisea tangu kituo hicho kikamilike ujenzi wake mwaka jana, bado hakijaanza kutumika kutokana na madereva wa daladala kugoma kukitumia kwa mdai kuwa hakina abiria.
Walisema ili kuhakikisha kituo hicho kinatumika na kuondoa ussumbufu wa kutembea mpaka Tandika ambako daladala hizo zinapaki, ni vyema Sumatra ikasaidia katika kuhakikisha kituo hicho kinatumika.
Kwa upande wao madereva wa daladala zinazotakiwa kutumia kituo hicho walisema itakuwa vigumu kwao kutumia kituo hicho kwa madai kuwa hakina abiria tofauti na kituo cha Tandika ambacho wanakitumia hivi sasa.
Kituo hicho cha Temeke Mwisho ambacho ujenzi wake uligharimu zaidi ya Sh. 70 milioni, kilitakiwa kuanza kutumika kuanzia Februari 2 mwaka huu kutokana na agizo la kikao cha baraza la madiwani mwisho mwa mwezi Januari(Mwananchi) .

Waitaka Serikali Itumie Busara kukomesha Ajali!

Wamiliki wa mabsi ya abiria katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara wameijia juu serikali kwa kile wanachodai ni kucheza mchezo mchafu wa kuwafilisi kwa kuanzisha mipango ya kukurupuka ambayo haiwezi kudhibiti ajali nchini.

Wanachama wa chama cha wasafirishaji wa mikoa hiyo (AKIBOA) wamedai kuanzishwa kwa utaratibu wa mabasi yote kufunga kidhibiti mwendo ni mfano halisi wa maamuzi ya kukurupuka na sasa serikali imekuja na jambo jipya.

serikali kupitia Mamlaka ya udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imetoa muda wa miezi sita kufunga kifaa kingine mithili ya kile cha kudhibiti mwendo maarufu kama 'speed governor' lakini hiki kipya kinajulikana kama 'Tachograf' na kazi yake ni kutunza kumbukumbu za mwendo wa basi.

Kifaa hicho kinadaiwa kitagharimu sh. 1 milioni wakati kile cha Speed Governor ambacho kimeshindwa kudhibitia ajali kilifungwa kwa Sh. 600,000 kwa kila basi, uamuzi ambao unadaiwa ulikuwa mradi wa vigogo serikalini.

"Gavana tulifunga kwa Sh. 600,000 lakini ime-prove failure(imeshindwa) na roho za watanzania zimeendelea kuteketea na sasa wanakuja na kitu kingine mfano wa gavana" ,alilalamika Amoni Mlaki.

Mlaki aliipasha serikali kuwa dawa pekee ya kudhibiti ajali iliyokuwa na mafanikio tangu enzi za ukoloni za ukoloni ni kusimamiwa kikamilifu kwa vituo vya ukaguzi na kufuatwa kwa ratiba za mabasi(Mwananchi).

AJALI YA TRENI-DODOMA!!






Ajali ya treni iliyotokea Dodoma katika eneo la Gulwe na Msagali wilayani Mpwapwa. Picha zinaonyesha mabehewa yaliyopata ajali.



Sunday, March 29, 2009

Dokezo La Leo!!

"Dereva Chunga Maisha................"
Wimbo wa Daudi Kabaka wa Kenya.

AJALI YA TRENI!!


Kuna taarifa kwamba imetokea ajali ya treni mkoani Singida ambapo treni ya abiria imegongana na treni ya mizigo. Habari za awali zinasema kwamba, ajali ilitokea majira ya saa 10 alfajiri.

Waliopoteza maisha inasemekana ni 16, na maiti nyingine kadha zimekandamizwa na mabehewa hivyo kufanya utaratibu wa kuzitoa kuwa mgumu sana.

Taarifa zaidi zitawajia pindi zitakapopatikana.

KWA MTINDO HUU WENGI TUTAKUFA!




Ni juzi tu kijana Lazaro(23) dereva wa taksi maeneo ya Suka Kimara, alipigwa risasi kwa kushukiwa kwamba ni jambazi jambo ambalo wakazi wa eneo hilo wamelipinga na kuwa na hisia tofauti.

Kama wanavyodai polisi kwamba siku hiyo eneo hilo kulikuwa na tukio la ujambazi na hivyo walishuku kwamba alihusika katika tukio hilo.

Katika hali ya kawaida, inatokea ghafla unaona watu wenye silaha wanakusimamisha wakitokea vichakani, je utasimama?maana hawana sare za polisi , wamevaa kiraia na wanaelekeza mtutu wa bunduki kwako. Nadhani kwamba aidha utakimbiza gari au utasimama kwa hofu kubwa ukijua kwamba sasa mambo yameishaharibika kutokana na hofu kwamba majambazi yameishakuteka!
Jeshi la Polisi linatumia nguvu na muda mwingi kuwaelimisha wananchi juu ya "Polisi-Jamii" lakini inaonekana wanasahau wajibu wa kutengeneza "Client Service charter" yaani mkataba kati ya 'mpokea' na 'mtoa' huduma. Polisi wanatakiwa kufahamu kwamba wao wana wajibu wa kufanya kabla ya kutegemea wananchi watekeleze wajibu wao.

Kwa mfano, askari anapomkamata raia au tuchukulie mfano askari aliyemmiminia risasi kijana Lazaro, wakati anamsimamisha alikuwa ametimiza wajibu wake? Je, alikuwa ana kitambulisho chochote cha kumfanya Lazaro asiwe na hofu kwamba anasimamishwa na majambazi?

Tunaona nchi za wenzetu hata katika senema, kitu cha kwanza askari anachofanya ni kutoa kitambulisho chake na hata kujitambulisha kwa mayowe "Police! police!" Wengine huvaa vitambulisho vyao kama mkufu unaning'inia shingoni-hii yote ni kumtoa hofu anayesimamishwa ajue anasimamishwa na watu wema, walinzi wa usalama. Hapo askari anakuwa amekamilisha majukumu yake katika "Client Service Charter".

Mashuhuda wanasema kijana Lazaro alihofu kufungua dirisha lote na akashusha dirisha kidogo, lakini askari wakafanya waliyofanya.

Ni lazima kufahamu kwamba kijana Lazaro alikuwa anaendesha gari jipya na historia inaonyesha kwamba katika maeneo hayo ya Suka na Temboni kuna madereva ambao waliishatekwa na kunyang'anywa magari.

Najiuliza, je kulikuwa na uwezekano wa askari hao kutoboa magurudumu ya gari ili asiweze kukimbia kuliko kumpiga risasi?
Nakumbuka tukio lililompata kaka yangu yapata miaka 6 au 7 hivi iliyopita. Alikodi teksi eneo la njia panda ya whitesands kwa nia ya kupelekwa nyumbani kwake Salasala. Mara wakaona gari ya polisi maarufu "ki-gofu" ikiwafuata kwa kasi, askari 'wakikoki' bunduki zao(SMGs) tayari kushambulia. Kisa? walidai ati walikuwa wanaenda kufanya ujambazi.Mungu saidia, dereva hakushtuka akasimamisha gari. Na kwakuwa walikuwa na sare za polisi kidogo ilileta imani kwamba ni walinda usalama japo majambazi mengine huvaa sare za polisi. Baada ya hapo walipelekwa Oysterbay Police na kugundulika kwamba gari waliyokuwa wanaifuatilia siyo yenyewe. Lakini kumtoa hapo kituoni nadhani wadau mnajua kasheshe yake.

Ni kwa mifano kama hii,ndiyo maana nasema "kwa mtindo huu wengi tutauawa". Askari wawe na vitambulisho popote pale, maana wakivaa kiraia kama raia mwingine yoyote na silaha mkononi nani atajua wao ni watu wema hasa ikiwa katika mazingira tatanishi?

Nafikiri dhana ya "Polisi Jamii" ni nzuri lakini mapungufu kama haya yatupiwe macho.
NAWASILISHA!

Saturday, March 28, 2009

Mandela Road yafungwa na lori baada ya ajali!
Leo jioni ilikuwa kizazaa baada ya lori lenye tela kuanguka kutokana na kile kilichoonekana kushindwa kwa dereva wake kulimudu kutokana na tatizo la kiufundi lilijitokeza katika gari hilo. Kilichotokea ni foleni kubwa sana kutoka njia panda ya Tabata hadi Ubungo na Ubungo hadi Shekilango na ubungo mataa hadi Mlimani City.
Kilichoonekana ni jiji kukosa 'winchi' kubwa ya kunyanyua magari mazito kama hilo!

Chenge agonga na kuua!











Habari iliyotawala vyombo vya habari leo ni kuhusu ajali iliyomhusisha Mh. Andrew Chenge Mbunge wa Bariadi Mashariki. Habari zilizopatikana ni kwamba ajali ilitokea majira ya saa 10 alfajiri jana katika eneo la Masaki Shule ambapo yeye akiendesha gari lenye namba za usajili T512 ACE aliigonga Bajaj yenye namba za usajili T 736 AXC na kuua watu wawili ambao ni abiria. Dereva wa Bajaj alikimbia baada ya ajali.
Kilichigusa hisia za wakazi wengi wa jiji ni kuona Mh. Chenge akiendesha gari ambalo Bima yake imeisha. Akiwa ni mwanasheria aliyefikia kuwa mwanasheria Mkuu wa Serikali, inatisha kuona alikuwa anaendesha gari ambalo Muda wa Bima umeisha. Waliopoteza maisha Mungu aziweke mahali pema peponi. Amin.

Wakati huo huo, Tume imeundwa kuchunguza kifo cha dereva wa taxiva Lazaro Mwapi(23 )aliyepigwa risasi na Polisi maeneo ya Stop Over kiwanjani. Inadaiwa kwamba polisi wa kikosi maalum cha kupambana na uhalifu walimshambulia kwa risasi licha ya kijana huyo kutii amri ya kusimama.
Akisimulia tukio hilo dereva anayejulikana kwa jina la Jacob anasema kwamba, "kulikuwa na tukio la ujambazi maeneo hayo na Lazaro alipata mteja na kumshusha alikokuwa anakwenda, wakati akiwa anarudi askari hao walijitokeza katika vichaka na kumsimamisha. Akasimama na kufunga vioo vya gari kwa hofu ya kwamba labda majambazi wanataka kumnyang'anya gari. Walipomwambia ashushe kioo alikishusha kidogo, na ndipo askari mmoja akavunja kioo na kumfyatulia risasi. Inasikitisha, ni kijana mdogo hapa kijiweni na amepewa hiyo gari hata mwezi haujafika"
Mungu ailaze roho ya marehemu Lazaro mahali pema peoni. Amin(picha kutoka blog ya Mroki Mroki)


The use "Bajaj" as passenger vehicles, is still a big NO for me
In recent weeks, I have written extensively against about the use of motorised tricycles, Bajaj, to ferry passengers.I am of the opinion that these tricycles are not made for passenger use. Secondly, they are being driven by unlicensed drivers with very little experience in ferrying passengers. Thirdly, these tricycles do not observe the rules of the road, they capitalise and use any openings that they can find on the road and lastly, they are contributing to the increasing traffic jam in our roads.I am pretty certain that if this practice continues unabated, we will have more Bajaj deaths.We do not need Bajaj in our roads, instead we need to focus in developing better transport system for our city. I hope we can learn from this experience.My heart goes out to the victims of the yesterday accident that involved the Bariadi Member of Parliament, Andrew Chenge(from Dr. Faustine Baraza).


Yes!: I do agree with Dr. Faustine, at Muhimbili Orthopaedic Institute(MOI) every day people are admitted after being involved in either bajaj or motorcycle accidents. True, if we want to save lives, something should be done. Faster!

Friday, March 27, 2009

''TRIANGLE'' IN STYLE




"Designed to prevent rear-end collisions after a car accident or break-down, Safe Balloon is a large-format combined warning triangle and airbag that other road users would find impossible to overlook".

Inasikitisha.......Lakini ni Ujasiri Uliyookoa Maisha ya Kichanga!

Ni katika ajali ya basi la Morning Star iliyoua watu wanane.
Katika taarifa ya tarehe 20 machi 2009, nilitoa taarifa ya ajali ya Morning Star iliyoua watu saba, na wengine kadhaa kujeruhiwa. Gari lililopata ajali lina namba za usajili T674 ADY lililokuwa likifanya safari kutoka Dar es salaam kwenda Mloka Rufiji.
Mmoja kati ya abiria waliopoteza maisha ni Bi. Havijawa Omari mkazi wa Tegeta ambaye alikuwa anaenda Kilimani Rufiji katika msiba. kwa mujibu wa ushuda uliopatikana ni kwamba, kabla ya ajali dereva alijaribu sana kuli-'control' gari lakini akashindwa na hatimaye aliwaambia abiria wake kwamba japo anajitahidi anaelekea kushindwa, hibvyo kila abiria amuombe mungu awasaidie watoke salam. Baada ya kusema hivyo, kila mmoja ndani ya basi alikuwa anafikiria ni jinsi gani ya kujiokoa na gari lilizidi kwenda mrama.
Ndipo mama huyu Havijawa Omari, akiwa na mtoto wake mchanga ikamjia akili ya haraka haraka kabla gari halijapinduka, akamtupa mtoto wake mchanga wa miezi 8 nje ya dirisha kwa lengo la kumuokoa. Baada ya kufanya hivyo gari likapinduka na Havijawa akapoteza maisha!
Mtoto wa Havijawa, Tariq Majaliwa, ni mtoto wa kiume wa miezi 8 ambaye sasa hivi analelewa na bibi yake, alivunjika mkono na kupata michuko sehemu ya usoni.
Ni tukio la kusikitisha, lakini Bi. Havijawa alifanya kile ambacho hakikutarajiwa na wengi.Tariq amelazwa katika Taasisi ya Tiba ya mifupa na Ajali Muhimbili (MOI). Afisa Uhusiano wa MOI, Jumaa Almasi alithibitisha kumpokea mtoto huyo na akasema kwamba anaendelea vizuri.
POLE: Bi Havijawa Mungu ailaze roho yake peponi, mtoto Tariq namwombea Ahueni ya haraka.

ICCT WAGAWA VITABU VYA MILIONI 500!







Injury Control Center in Tanzania(ICCT) kwa kushirikiana na Canadian Network for International Surgery(CNIS) wametoa msaada wa vitabu 7719 vyenye thamani ya Dola za Kimarekani 420,480(zaidi Tsh Mil. 500). kulingana na maelezo ya Prof Lawrence Museru ambaye ni Mwenyekiti wa ICCT, vitabu hivyo vinagawiwa katika Taasisi mbalimbali hapa nchini zinazotoa elimu ya udaktari ambazo ni, Muhimbili University of Health and Allied Sciences(MUHAS), Herbert Kairuki University, Buhando University, Kilimanjaro Christian MEdical Center(KCMC) na Muhimbili Orthopeadic Institute(MOI). Mgao wa vitabu na thamani yake ni kama ifuatavyo; MUHAS USD 11,000, Bugando USD 73,500, Herbert Kairuki USD 68,532 na MOI USD 62,000.



Prof. Museru alisema kwamba vitabu hivyo vitasaidia sana kufundishia wanafunzi wanaosomea fani mbalimbali za udaktari kama tiba ya meno, mifupa, uuguzi,dawa ya usingizi n.k. ni vitabu vipya ambavyo si rahisi kuvipata hapa Tanzania na hata vikipatikana vitakuwa ni ghali sana.



Prof. Cassian Magori akitoa shukrani kwa niaba ya Taasisi zilizopata msaada huo, alisema kwamba wanashukuru kupata vitabu hivyo ambavyo vimeandika na mabingwa wa fani mbalimbali za tiba na ni vya miaka ya hivi karibuni. Aliongeza kwamba, watahakikisha kwamba vitabu vinatunzwa ili kuwasaidia wanafunzi katika vyuo vyao. Mwisho aliipongeza ICCT kwa kazi nzuri wanayofanya.



Mwenyekiti wa ICCT, prof. Museru alisema kwamba wao kama ICCT wanafanya jitihada kubwa kwa kutoa mafunzo kwa wanaotoa huduma kwa majeruhi mbalimbali na kwamba wamekuwa wakitoa mafunzo katika hospitali jinsi ya kuhudumia majeruhi wa ajali mbalimbali(madaktari na wauguzi), wahudumu wa vyumba vya dharura.Alisema mafunzo yameishafanywa katika hospitali za; Temeke, Mwananyamala,Tumbi-Kibaha, Mkuranga, Iringa, Morogoro na hivi karibuni yalifanyika Musoma. Pia alisema wameweza kutoa mafunzo ya jinsi ya kutoa huduma ya kwanza(First Aid) katika shule za msingi za Dar es salaam pamoja na madereva wa taxi, zimamoto na Polisi wa Usalama barabarani ili wajue nini cha kufanya kuokoa maisha ajali inapotokea.Pichani Prof. Museru akikabidhi vitabu na baadhi ya vitabu vikipakiwa katika gari.

PONGEZI: Mimi kama mdau wa kupambana na ajali zinazopoteza maisha ya watanzania kila kukicha, naipongeza ICCT kwanza kwa kutoa msaada huo na pili, kutoa mafunzo ya jinsi ya kuokoa maisha inapotokea jali kwa kutoa mafunzo ya utoaji wa hudma ya kwanza. ICCT Big up sana.

Thursday, March 26, 2009

Amwagwa na Pick-Up na kufariki!

Alikuwa akidaka kofia yake iliyopeperushwa na upepo.
Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Muteseka mugusi 32, amefariki dunia baada ya kudondoka toka kwenye gari akiwa kwenye harakati za kudaka kofia yake iliyopeperushwa na upepo.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa mwanza, Jamal Rwamboh, amesema tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 11:00 jioni huko kwenye barabara ya Mriti Wilayani Ukerewe.
Amesema mtu huyo ambaye ni mkazi wa nakamwe Ukerewe alidondoka toka kwenye gari lenye namba za usajili T 316 ARR aina ya Nissan Pick-Up, lililokuwa likiendeshwa na dereva Maingu malima,25(Alasiri).

Ajali Dar......ni ya Daladala!


Moshi Lusonzo wa gazeti la Alasiri anaripoti kwamba ".......Daladala mbili jijini Dar es salaam zimevaana uso kwa uso na kusababisha abiria wake 18 kujeruhiwa na baadhi yao kulazwa hospitalini.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke Emmanuel Kandihabi amesema ajali hiyo ilitokea jana mishale ya saa 3.30 usiku katika barabara ya temeke, pale kwenye Hospitali ya Wilaya ya Temeke.

Akisimulia tukio hilo, kamanda kandihabi ameyataja magari yaliyopata ajali kuwa ni Nissan Civilian lenye namba za usajili T 405 ADZ lililokuwa likitokea tandika kwenda buguruni likiendeshwa na Jamal Juma 30, mkazi wa mkuranga na Toyota DCM lenye namba za usajili T150 AMC lililokuwa likitokea Temeke kwenda Mbagala.

Amesema katika ajali hiyo, watu 18 walijeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali ya Temeke, ambapo watu 15 kati yao, walitibiwa na kuruhusiwa na watatu wamelazwa hospitalini hapo.

Kamanda Kandihabi amesema dereva wa DCM alikimbia baada ya kutokea kwa tukio hilo na polisi wanaendelea kumtafuta".

Wednesday, March 25, 2009

Agongwa na gari na kufa papo hapo!

Ajali ilitokea katika eneo la Mbezi Kibanda cha mkaa mwanaume mmoja ambaye umri wake unakadiriwa kuwa miaka 30 na 35 aligongwa na gari(hit and run) na kupotesha maisha papo hapo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa kinondoni Mark Kalunguyeye alisema tukio hilo lilitokea wakati gari ambalo halikufahamika lililokuwa likiendeshwa na dereva asiyefahamika likitokea Mbezi Mwisho kuelekea kimara, lilipofika eneo hilo ndipo likamgonga mtu huyo.
Maiti ya marehemu ilihifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala.

Temeke Walilia Matuta Barabarani!

Ni baada ya ajali kuzidi.
Wakazi wa maeneo ya Temeke kwa maganga hususan wanaotumia barabara ya Dk Omar Ali Juma,wameitaka serikali kuongeza matuta katika barabra hiyo ili kupunguza ajali ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara.
Akiongea na nipashe kwa niaba ya wakazi hao, kaimu mwenyekiti wa mtaa wa maganga, Hussein Salum, amesema suluhisho la ajali ambazo zimekuwa zikichukua roho za raia wengi wa eneo hilo ni kuongeza matuta katika barabara hiyo ili magari yasiende kwa kasi kama ilivyo hivi sasa(Nipashe).

Wanne Wafa Ajali ya Gari, Pikipiki!

Watu wanne wamekufa na mmoja kujeruhiwa baada ya magari na pikipiki waliyokuwa wakisafiria kugongana katika barabara kuu ya Morogoro-Dar es salaam eneo la Nane Nane mjini hapa.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Ibrahim Mwamakula, alisema ajali ya kwanza ilitokea machi 21,mwaka huu saa 9.30 alasiri.
Kamanda Mwamakula alisema ajali hiyo ilihusisha basi la abiria lenye namba za usajili T 381 AXT aina ya FAU, mali ya Kampuni ya Tonda Express lililokuwa likitokea Njombe kuelekea jijini Dar es salaam. Alisema Basi hilo lilikuwa likiendeshwa na majid mohamed(46) liligongana na gari ndogo aina ya Toyota Corolla yenye namba T 666 AKJ ikiendeshwa na Sweetbert Kamugisha(28).
Wakati huo huo, mwendesha pikipiki na abiria wake wamepoteza maisha baada ya kugongwa na gari eneo hilo la Nane Nane.
Kamanda Mwamakula Alisema pikipiki iliyohusika katika ajali hiyo haikuwa na usajili ambapo iligongw na Toyota Corolla yenye namba T292 AET iliyokuwa ikendeshwa na Erick komba(26)(Nipashe).

Tuesday, March 24, 2009

HALI YA BARABARA MBALIMBALI USIKU WA LEO(23-03-2009)

Hali ya barabara mbalimbali za jiji haikuwa shwari usiku wa leo. Kulikuwa na ajali eneo la Mkwajuni iliyohusisha garo ndogo na basi la Tanzania Road Haulage. Sikuweza kufahamu mara moja kama kulikuwa na majeruhi au la, lakini kilichoonekana ni msongamano mkubwa wa magari uliosababisha na ajali hiyo. Magari ya kuelekea magomeni na yale ya kuelekea morroco yalikuwa yanatembea taratibu sana.
Katika tukio jingine, kulikuwa na msongamano mrefu maeneo ya Kimara kutokana na magari kupunguza mwendo katika matuta ya barabarni, hivyo daladala zilikuwa zinapita pembeni mwa barabara kwa kasi sana hatimaye daladala moja linalofanya safari zake kutoka Ubungo kwenda Msata yenye namba za usajili T860 ATQ ilikuwa inaenda kwa kasi sana kuelekea Mbezi. Ilipofika kimara stop over, ilimgonga mama aliyekuwa na mtoto wake wakitembea pembeni mwa barabara. Baada ya kumgonga ilimpakia huyo mama ndani na kuondoka nae.
Sijui walimpeleka wapi!

Pikipiki Zaendeleza Vibano!


Kulingana na Taarifa ya Afisa Uhusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ajali Muhimbili (MOI) Bwana Jumaa Almasi, haipiti siku bila kupokea majeruhi wa ajali ya pikipiki katika Taasisi hii. Aliyasema hayo alipokuwaakitoa taarifa ya waendesha pikipiki wawili walifikishwa hospitalini hapo jana, ambao ni Yuster kessy(35) ambaye aliangushwa katika pikipiki akiwa abiria. Aliteguka kiwiko cha mkono.

Mwingine ni Shomari Bakari saleh(39) ambaye alianguka akiwa anafanya michezo ya pikipiki lakini alipofika katika tuta la barabarani pikipiki ilimrusha na kumtupa chini. Aliumia mkono na goti na baada ya matibabu aliruhusiwa kwenda nyumbani.

Hoja: Nafikiri hatua za haraka zichukuliwe na mamlaka husika kudhibiti hili wimbi la ajali za pikipiki, kama alivyosema Afisa uhusiano wa MOI inaonekana ogezeko la pikipiki linachangia ongezeko la ajali.

Monday, March 23, 2009

GARI ZAWAFUATA PEMBENI NA KUWAGONGA!

Katika hali ya kusikitisha sana, Aisha Shabani mtoto wa miaka 12 leo amejikuta anafuatwa na gari pembezoni mwa barabara na kugongwa katika maeneo ya Tangi Bovu. Baba wa Aisha, Bwana Shabani Dadi, anasema kwamba akiwa na mwanae mara waliona gari linawafuata pembeni kwa kasi na mwanae alipokosa mwelekeo ndipo gari ikamgonga na kumvunja mguu. Amesema kwamba Aisha amelazwa wodi ya watoto ya Taasisi ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ajali Muhimbili (MOI).Aisha anasoma shule ya Msingi Kawe B. Gari iliyomgonga ina namba za usajili T 149 AQR saloon.
Mwingine ni Bwana Robert Masawe ambaye ameelezea tukio hilo kwamba, alikuwa anasubiri gari katika pembeni kabisa mwa barabara, daladala liliacha njia na kumfuata alipo na kumgonga. Robert aliteguka bega.
Mwisho ni Arumela Mwapalala(15) mkazi wa kimara alikuwa ana vuka barabara gari likamgonga ambapo alipata jeraha kubwa katika kidevu na kupoteza jino moja.alipata matibabu na kuruhusiwa kwenda nyumbani.
Afisa Uhusiano wa MOI Bwana Jumaa Almasi alisema kwamba, wagonjwa walifikishwa MOI na kupatiwa matibabu. Robert Masawe na Arumala waliruhusiwa , na Aisha alilazwa.

AJALI ZAIDI, MOROGORO WANNE WAPOTEZA MAISHA!

Vyombo vya habari vinaendelea 'kupamba' kurasa kwa habari za ajali zaidi na zaidi. Jana taarifa zilizotanda ni juu ya ajali ya basi la Tando iliyotokea mkoani morogoro ambapo watu wawili walipoteza maisha na mmoja kujeruhiwa vibaya.
Wakati huo huo watu wawili waliokuwa katika pikipiki bao walipoteza maisha hapo hapo Morogoro kufuatia ajali ya gari.

Sunday, March 22, 2009

kUTOKA MOI LEO

Kutoka Taasisi ya Tiba ya Magonjwa ya Mifupa na Ajali(MOI) Taarifa zinaonyesha kwamba Majeruhi kadhaa wamepokelewa katika Taasisi hiyo wakiwa ni wa ajali mbalimbali zilizotokea sehemu mbalimbali za jiji. Rashid abdulrahim Rashid(24) mkazi wa Ilala alipokelewa MOI saa 7 usiku baada ya kupata ajali ya pikipiki, amepata michubuko na amevunjika mguu sehemu ya paja(femur). Mwingine ni Christina Mlwale(26) ambaye amevunjika mfupa wa karibu na bega(clavicle) na mumewe Magnus Kisinga (32) wote ni wakazi wa Mbezi Louis, walipata ajali ya kugongwa na gari wakiwa katika katika pikipiki walipokuwa njiani kutoka Mbezi kuelekea Kimara. Christina amelazwa katika wodi ya Mwaisela na mumewe alitibiwa na kuruhusiwa. Wengine ni Slavatory Mathias Temba(18) mkazi wa Magomeni,alipata ajali na kuumia kichwa:Paulo Siyanga(51)naye alifikishwa MOI akiwa amevunjika Mguu sehemu ya paja(femur);Mzee Nasser(60) naye alipata ajali na kupata michubuko mwili mzima na kuumia kichwa na wa mwisho ni Ketra Bernard Frank(22) ambaye alipata ajali na kufikishwa MOI akiwa amevunjika mguu.



Bwana Jumaa Almasi Afisa Uhusiano wa MOI amethibitisha kuwapokea majeruhi na kwamba wanaendelea vizuri.



Friday, March 20, 2009

TAHADHARI!!!


Kumeibuka wimbi la watu kufanyiwa vitendo vya kiharamia wanapopanda daladala nyakati za usiku au alfajiri. Leo alfajiri kijana anayejulikana kwa jina la Abdu Rashidi Abdalla(27) amepatwa na mkasa kama huo.
Akisimulia wakati akiwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Magonjwa ya Ajali (MOI), anasema kwamba alitoka nyumbani kwake Manzese saa 11 asubuhi na kupanda daladala kuelekea Kituo cha Mabasi ya kwenda mikoani cha Ubungo. Amesema daladala hiyo ilikuwa na abiria watano na yeye alikuwa wa sita. Daladala lilipokaribia stendi ya mkoa, mmoja wa abiria alianza kumzonga kwamba amemuibia simu yake, wakati wanabishana mara abiria aliowakuta katika gari wakaanza kumpiga. alipofika stendi ya Mkoa na kutoa taarifa kwamba amefika, hawakumsikiliza na gari ikaenda mwendo kasi hadi Kimara ambapo walimtupa nje ya gari huku gari likitokomea kwa mwendo wa kasi.
Anasema, wamempora shilingi laki 2 ambazo alikuwa anampelekea baba yake ambaye ni mgonjwa na mizigo na zawadi alizokuwa anapeleka kwa wazee.
Afisa Uhusiano wa MOI amesema kwamba ni kweli Abdu amepokelewa hapo akiwa ameumia kichwa, sehemu ya bega na michuko sehemu mbalimbali za mwili na anaendelea na tiba.
TAHADHARI: Iwapo ni lazima kupanda daladala nyakati za usiku chukua tahadhari kwa kuandika namba ya usajili ya gari au ya usajili wa daladala inayoonekana ubavuni mwa gari. na iwapo ni gari ambayo haina namba ya ubavuni ya usajili wa daladala, ni vema kuwa na tahadhari. nyingi ya gari zinazofanya uhalifu huu ni zile zinazoitwa 'gari za usiku' yaani 'daladala bubu'.

SUMATRA Yazuia Vyombo Vidogo Vya Majini Kusafiri Usiku!




Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imepiga marufuku vyombo vidogo vya usafiri majini kusafiri usiku ili kupunguza ajali nchini.


sanjari na hilo, SUMATRA imepiga marufuku vyombo vidogo visivyo na mitambo (injini) kupakia abiria.


Mkurugenzi wa Usalama wa vyombo vya majini, King Chilagi aliyasema hayo juzi kwenye mkutano uliowakutanisha wamiliki, waendeshaji na wavuvi wa vyombo vidogovidogo uliofanyika katika bandari ya Bagamoyo Mkoani pwani.

Alisema SUMATRA imechukua hatua hiyo ili kukabiliana na wimbi la ajali za majini ambazo zinahusisha vyombo vidogo vidogo kutokana na vyombo hivyo kusafiri usiku vikiwa havina taa hali ambayo inasababisha kugongwa na vyombo vikubwa vya majini.

Alisema kuanzia sasa vyombo hivyo, licha ya kuzuiliwa kuanza safari zake usiku pia havitaruhusiwa kuondoka kabla ya kukaguliwa na kuruhusiwa na mkaguzi wa bandari husika baada ya kujiridhisha kuwa chombo kina vifaa vya kujiokolea pindi inapotokea ajali majini.

"Hivi sasa kila bandari ndogo atakuwepo mkaguzi atakayehakikisha chombo kinachoondoka bandarini kina vifaa vya kuokolea maisha ya watu (Life Jackets) pamoja na vyombo vya mawasiliano kama simu. Alisema chilagi(Mwananchi).

HOJA:Naamini hii ni hatua muhimu sana katika mapambano dhidi ya ajali ambazo zinachukua maisha ya watanzania kila kukicha. Ni vema kuzuia kuliko kusubiri mpaka yatokee maafa ya kutisha ndio hatua zichukuliwe. Lakini pia ni muhimu kuhakikisha kwamba, hili sio zoezi la siku mbili halafu watendaji wanalipuuzia, ni zoezi ambalo linalopaswa kufuatiliwa kila siku kama kweli tunathamini maisha ya watanzania. Kuna dhana iliyojengeka kwa watanzania wengi kwamba unapoanzisha udhibiti wa aina fulani, basi wale wanaohusika umewapa nafasi ya kujitajirisha.

Ajali Nyingine Pwani Yaua Saba!

Wakati majina ya watu 10 waliofariki kwenye ajali ya gari la abiria mkoani mbeya wakitajwa majina, ajali nyingine imetokea wilayani Rufiji na kuua watu 7, ikijeruhi wengine 20.
Jana Mwananchi iliripoti kuwa watu 20 wanahofiwa kufa katika ajali hiyo iliyotokea Barabara ya Tunduma kwenye maeneo ya Mbembera, njia panda ya JKT Itende, na eneo la Iyunga, lakini jana Mkuu wa Wialaya ya Mbeya, Leonidas Gama alisema ni watu 10 tu waliofariki kwenye ajali hiyo na si 20 kama mashuhuda walivyosema jana.
Katika ajali ya iliyotokea Mloka wilayani Rufiji, watu 7 walipoteza maisha na wengine 20 kujeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka.
Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 8 mchana ikihusisha garilenye namba za usajili T 674 ADY mali ya kampuni ya Morning Star ambalo lilikuwa linatokea jijini Dar es salaam kwenda Mloka (Na julieth Ngarabali Mwananchi 20-3-09).

Thursday, March 19, 2009

WATU 20 WAHOFIWA KUFA AJALINI MBEYA.
Zaidi ya watu 20 wanahofiwa kufa katika ajali ya barabarani baada ya lori la mizigo kugonga magari sita ikiwamo daladala katika eneo la Mbembela, lilopo Nzovwe, jijini Mbeya. Walioshuhudia tukio hilo walisema wamewaona watu wengi wakiwa wameumia vibaya baada ya lori hilo lililokuwa likienda kwa mwendo kasi likiyumbayumba na kisha likaligonga basi hilo aina ya Hiace.
Baada ya kuligonga gari hilo lililigonga gari jingine dogo lililokuwa umbali wa mita 10 kutoka katika basi hilo na kisha likaligonga gari jingine aina ya Landcruiser ambalo mbele yake kulikuwa na magari mengine mawili. Baada ya kugonga magari yote hayo moto ulilipuka(gazeti la Mwananchi 19-03-09).

MAONI KUTOKA KATIKA BLOGU YA Da' CHEMI

Maoni haya yalipostiwa siku ya Alhamisi Tarehe 1 Novemba, 2007 naona si vibaya nikayaweka hapa kwa kuwa yanahusu masuala ya ajali na jinsi ya kuziepuka.Maoni yenyewe yana kichwa cha habari kama kinavyoonekana hapo chini.Ni makala ndefu kidogo lakini inafaa kuisoma kwa kina na kuitafakuri.

Wimbi la Ajali za barabarani Tanzania!

Nimetumiwa haya maoni na msomaji Born Again Pagan:*******************************************************************************Born Again Pagan said...
Chemi, naomba uruhusu haya yangu kuhusu Ajali Barabarani Nchini:Hivi karibuni, katika mojawapo ya blogu nyingi mashuhuri za wa-Tanzania, niliahidi kwa kuwaomba wanakijiji kujipa muda wa kutafakuri na kuchangia suala la ajali barabarani na jinsi ambavyo tunaweza kupunguza “balaa” hili ambalo linaendelea kutusibu siku hadi siku, mchana na usiku.Ingawa ni wanakijiji kama wawili hivi walichangia, sikukata tamaa. Nazidi kuwaombeni tujaze blogu hizi kwa maoni yetu kuhusu maafa ya ajali barabarani. Blogu hizi zinasomwa na wengi, wakiwemo viongozi wa serikali, wabunge wetu, viongozi wa dini na mashirika yasiyo ya serikali.Napenda kurudia mchango wangu wa awali kuhusu ajali nchini mwetu, ikiwa ni sehemu ya maombolezo ya kutokwa na Naibu Waziri Salome Mbatia. Mhariri wa gazeti maarufu nchini la kila siku aliandika, “…taifa limeghubikwa na majonzi makubwa kufuatia kifo (cha Naibu Waziri Salome Mbatia) kilichotokana na ajali ya gari eneo la Kibena, Njombe mkoani Iringa Alhamisi”.
Lakini yatubidi kuzingatia kwamba si Salome Mbatia peke yake aliyekufa katika ajali hiyo. Dereva wake na utingo wa lori nao walikufa. Na sio ajali hiyo tu iliyotokea siku hiyo na kusababisha mauaji! Karibu watu kama kumi hivi walikufa kwa ajali barabarani siku hiyo! Lakini kifo cha Naibu Waziri Salome Mbatia kimepewa kipaumbele zaidi ya vifo vya wengine. Sababu zinaeleweka; sina haja ya kuzirudia.Mhariri huyo alitoa tahadhari kali kuitaka “Serikali na vyombo husika na sekta ya usafirishaji” kudhibiti ajali: “Yafaa tatizo hili la ajali za barabarani zinazotokana na uzebe na mwendo wa kasi litizamwe tena kwa makini. Bado linapoteza maisha ya watu wengi wasio na hatia wakati zinaweza kuepukwa.Madereva wengi bado wamekuwa ni vichwa maji katika uendeshaji wao barabarani.”
Kauli kama hiyo ya mhariri, sambamba na kauli nyingi za umma zisizotangazwa, inaitaka serikali yetu kamwe isingoje “kifo cha mzaliwa wa kwanza”, kama mtawala Firauni wa Misri, ndipo iamke na kufanya lolote dhidi ya “janga” hili ambalo hudonoa maisha ya wa-Tanzania wetu!
Tumezoea kusema, “Ajali haina kinga!” Lakini ukweli ni kwamba ajali inaweza ikakingika! Wengine husema, “Ngoja ajali ziwamalize kwa kumwonea Kabwe Zubeir Zitto!”Hili nitalizungumzia kwa kifupi:Katika magazeti na blogu nyingi kumeibuka tabaka la washirikina au niwaite “wanajimu wabaya, watabiri mabaya, wenye ndoto mbaya, wenye maono” wenye kungojea “kiyama” kiikumbe serikali na CCM yake.Wenzetu wanamwomba m-Bunge wetu “kijana” Zitto Zubeir Kabwe aombe miungu ya huko kwao Kigoma kuweka breki ili isiwamalize wote wale waliomnyoshea kidole - mizimu ya Kigoma inalipa kisasi!
Wanaoanisha msululu wa ajali ambazo zimetokea kwa baadhi ya viongozi wa CCM kufuatia mzozo wa m-Bunge wetu “kijana” Zitto Zubeir Kabwe eti zinatokana na “kumwonea Zitto”!Natarajia kuchangia hili la mzozo wa Zitto, kulingana na maoni ya wasomi wetu wawili: Prof. Gidion Shoo (Zitto Hakuwatendea Mema Wananchi,” kwa mujibu wa “Kanuni za Bunge”.Msomi mwingine ni Prof. Shivji (Zitto Kabwe’s Suspension an Episode or an Epitaph?) Kero ya Zitto yaonyesha jinsi ambavyo nchi yetu imejigawa. Kuna ukweli kwamba wote hatuimbi, “Tanzania, Tanzania,nakupenda kwa moyo wote;nilalapo nakuota,jina lako ni tamu sana”!
Ni lazima kuna sababu zake, mbali ya vitendo vya rushwa na ufisadi!Kuna baadhi yetu ambao wamegeuka washirikina na kuonyesha hali ya chini kabisa. Hawa wanaomba mabaya zaidi yawapate wana-CCM, kwa jumla, na hasa wale viongozi waliojeruhiwa katika ajali mbali mbali!Sioni kama hili ni ombi la kiungwana!Ni matakwa ya wendawazimu kwani endapo CCM inafanya mabaya, kuitakia mabaya nako ni vibaya! Makosa mawili hayajengi au hayazai haki!Kumtakia mwenzako kifo ni sawa na kumwua tu. Leo tunatakiana vifo; kesho tutauana kimacho macho!Kuna wengine wenye kuamini kuwa ajali “Ni mipango ya Mungu - Mungu kapenda; siku yako ya kufa ikifika, imefika!” Hili pia yanataka ufafanuzi: Je, maisha yetu yamewekewa“blinkers” za “determinism”? Je, hakuna lolote tunaloweza kufanya kuepusha hiyo “determinism”? Mbona tunataka kuingilia kati nguvu za asili (nature) kwa kualika nchini “wachawi wa mvua” kutoka Thailand?Maisha yanajengeka kutokana na kuoana kwa akili zetu na maingilio ya mazingira tuliyomo. Tunaweza kuyabadili kwa kupata elimu tosheleza na hekima ya kuweza kutafukari na kutafuta njia za kusuluhisha au kutanzua tatizo la ajali barabarani. Wengine, hasa wadini walokoke huamini kuwa Mungu huadhibu kwa sababu ya dhambi. Hii sio kwa wa-Tanzania tu bali pia wahubiri wengi walokoke duniani, hususani, Marekani.Mhubiri mmoja mlokoke wa Amerika aliwahi kutamka kuwa Jimbo la Florida lilipatwa na madhara ya kuwaka moto kutokana na dhambi za kisenge na kishoga. Mlokoke huyo huyo alimshutumu Waziri Mkuu wa Israel kwa kupatwa na mshituko uliomlemaza kuwa ni kwa sababu kagawa nchi ya Palestine - nchi ya Mungu - kwa Wapalestina!Kisa kingine cha hivi karibuni: Jaji wa “federal” hapa Amerika ameamuru kanisa moja la Ki-Baptist la Westboro - kanisa lenye kuhubiri na kueneza chuki - kulipa faini ya dola millioni 10.9 kwa kushangilia kifo na kukielezea kifo hicho cha askari Lance Cpl Matthew Snyder vitani Iraq Machi 2006 kuwa ni adhabu kutoka kwa Mungu.Washirika walokoke wengi wa hapa Amerika wanahubiri ‘injili ya chuki” dhidi ya ushoga na kubagua mazishi ya watu waliokufa kwa ukimwi. Walokole wengine wanaamini kuwa Amerika inapata majanga, kama hilo la 911, kwa sababu wameacha kumcha Mungu! Je, Mungu anatuadhibu na hizo ajali zitokeazo barabarani?Pengine hilo la ajali na kudra za Mwenyenzi Mungu nalo linahitaji muda wake maalum wa kutafukari kwa undani, hasa kwa wale wenye kutaka kujua kutoka kwa wanaolielewa vizuri.Kuna baadhi yetu wenye kuziona na kuzitafukari ajali barabarani na kwinginepo, kama matukio ya kawaida tu.
Tusitekwe nyara na fikra za kufungwa macho yetu na akili zetu kuamini kwamba ajali haina kinga; ajali ni adhabu ya Mungu, au ni matakwa mengine ya ushirikina.Ajali husababishwa na/au mchanganyiko wa haya matatu:dereva, gari na barabara. Kuna Ripoti ya Mwaka 1994 inayoelezea rasmi na kwa undani kuhusu usafiri nchini. Sijui ni wangapi kati ya matrafiki husika, wamiliki wa magari, maderera na abiria wa kawaida wameipitia ripoti hii?Kuna vitu vitatu muhimu katika njia za usafiri wa nchi kavu kwa kutumia magari barabarani: dereva, gari na barabara.
Kila kimoja kina masharti yake sawa na “Social Environment”: mshiriki (Actor/Participant), kusudi (Purpose), sheria (Rules and Regulations), mipaka (Boundaries), maadili (Morality), siasa (what is to be done), na lugha (Technical Language).Dereva: Kulingana na Ripoti hiyo, sababu kubwa ya ajali nchini mwetu hutokana na madreva wenyewe. Ajali za namna hii ni kiasi cha asilimia 76.
Napenda kuongezea kuwa u-mahiri na u-makini wa kuendesha unatokana na mafunzo tosheleza na utahini usiopendelea; dereva kujiandaa vya kutosha kabla ya safari; asiendeshe huku amelewa au amechoka; afuate sheria za barabarani; na uwezo wa dereva kubaini endapo gari lake lina udhaifu au kasoro.Ajali nyingi za mabasi, malori yetu na magari madogo yetu kugongana vichwa kwa vichwa, kama ajali hiyo iliyotokea na na kuchukua maisha ya wakina Waziri Mbatia, dereva na utingo wa lori. Hii ina maana kuwa sababu kubwa ni pale dereva wa gari linalofuata kutaka ku-“overtake” lililotangulia karibu na mwisho wa kilima au kwenye kona kali bila kujua kuwa kuna gari lingine linakuja mbele.Wakati mwingine gari hupata kasoro na dereva kushindwa kuliongoza. Sababu nyingine ni kwa dereva kuchoka na kusinzia sinzia na mwisho kupoteza saiti yake.
Madereva wengine huendesha kulingana na wimbo wa mapenzi wa Daudi Kabaka (Kenya), ambapo abiria anamsihi dereva wa basi aongeze spidi ili abiria afike au awahi “date” yake:Dereva,Choma gari moto;Nifike upesi Nikaone mtoto.Mtoto ananingoja Stendi ya basi;Fanya haraka!Kuna pia baadhi ya abiria wenye kutaka kufika mapema kungali na jua kule waendapo. Abiria kama hao huhimiza dereva aendeshe kwa kasi. Madereva wengine nao wanapenda sana kuendesha kwa kasi ili wapate muda wa kupumzika, na kupata angalau “moja baridi” au kuwaona wapenzi wao huko waendapo au mwisho wa safari.Madereva wengine ni walevi; hupenda kunywa vileo kabla ya safari na wakati mwingine kupumzika safarini kwenye visima vya ulevi. Ukiwa Dar es Salaam, mabasi ya kwenda katika mikoa mingine yanaitwa “mabasi ya kwenda mikoani”, kana kwamba Dar es Salaam si mkoa.Kuna mabasi mengine, kwa mfano, huondoka Dar kwenda Mwanza kupitia Nairobi (Kenya) huwa yana madereva wawili tu. Kuna pia mabasi yanayoondoka Dar es Salaam kwenda Lubumbashi huko Kongo (Kinshasa) kupitia Kitwe (Zambia). Habari za kuaminika zinaeleza kuwa wakati mwingi madereva huchoka kuendesha na kuanza kusinzia sinzia na huku wakiendesha.Kuna madereva wengine wenye ka-tabia ka kuendesha magari kana kwamba wana-“enjoy the cruising moment.”Madereva wengine vichwamaji huwazuia wenzao wasipite; ni kama umewatukana. Hivyo huendesha kwa ujeuri kana kwamba kuna ugomvi au vita.Madereva wengine, hasa kwenye barabara zetu zisizo na lami, wanapenda sana kutangulia kuepuka au kuogopa mavumbi yanayoachwa na gari liliotangulia. Huwa ni mashindano. Kuna wengine, hasa wamiliki, hupenda sana kushindana kuwa wa kwanza kuchukua abiria au shehena kabla ya wenzao. Tabia hii ni ya kawaida kwenye barabara zetu nyingi.Dereva wa basi ataliendesha basi lake kwa “ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya” ili awahi kuchuma. Na mara nyingine basi linaweza kupata ajali.Barabara nyingi hazina maafisa wa trafiki. Na kama wapo wengi wanahongwa; na wananyamaza, kana kwamba mambo yote ni sawia. Lakini ukificha maradhi, kifo kitakuumbua.Wamiliki wa magari na madereva wamewaweka wakuu wa trafiki wa wilaya na mikoa mikononi. Hata kama afisa wa trafiki mdogo akimkamata mhalifu, kesi yake itafutwa na “wakubwa”.Barabara: Ripoti hiyo hiyo inaelezea kuwa ajali asili mia 7 husababishwa na matatizo ya barabara. Napenda kuongezea kuwa barabara zetu ndo hivyo tena; zilitengenezwa wakati magari yalikuwa ni ya serikali au machache kwa ajili ya abiria.
Ieleweke wazi kuwa hakuna uwiano wa moja kwa moja kati ya barabara nzuri na kupungua kwa ajali.Huko Ulaya kufika mwaka 1648, barabara zake nyingi zilizokitengenezwa tangu enzi za Warumi zilikarabatiwa kukabili mapinduzi ya viwandani yaliyoleta magari ya kukokotwa na farasi hadi mwingilio wa magari ya sasa.Huko Ulaya, Ujerumani wakati wa Hitler ikawa ya kwanza kuwa na “autobahns” “highways” kukidhi mahitaji wa maendeleo ya uchumi wa nchi hiyo na endapo kutatokea vita. Nchi nyingi za Ulaya/Amerika na zingine zilizoendelea zina barabara nzuri na pana.Nitatoa mfano mdogo wa hapa Amerika:New Jersey Turnpike (Highway) ipitayo karibu na Newark Liberty International Airport ina barabara zenye safu (lanes) sita za kwenda upande mmoja. Kwa hiyo barabara kuu hiyo ni kama ina barabara 12. “Highways” nyingi zina safu 3. Kwa kuwa Amerika inaendeshea mkono wa kushoto, safu ya upande wa kushoto ni kwa wale wenye kutaka kwenda kasi bila ku- “exit”.Safu ya katikati ni kwa wale wenye kuendesha mwendo wa kawaida. Na safu ya upande wa kulia ni kwa wale wenye kutaka ku-“exit”.Pamoja na “administration and management” ya uedeshaji wa namna hiyo, kuna matrafiki wakali wa mikoa (State Troopers) wanaolinda sheria za barabarani.Wengine hufanya kazi zao wazi wazi.Endapo msafara wa magari unakwenda kwa kasi, gari la trafiki hao litatangulia mbele na kwenda spidi inayotakiwa. Hakuna dereva atakayethubutu kuli-“overtake”! Kuna wakati madereva iliwabidi kuwasiliana kwa njia ya "Citizen Band - CB" ili kujiepusha na "State Troopers".Wakati mwingine matrafiki hao hujificha vichakani kando ya marabara na kuwalopoa (kwa njia ya rada) wale wenye ku-“overspeed”, na wakati mwingine kufanya ukaguzi wa ghafula wa gari .Magari ya kubeba shehena (“rigs” au “long distance trucking or haulage”) haya yana sheria zake kali. Kila dereva ni lazima abebe utambulisho wa kile alichobeba, kinatoka na kwenda wapi, ameanza kuendesha saa ngapi, na amepumzika kwa kiasi gani. Gari lake pia ni lazima lionyeshe ukaguzi uliofanyika.Na katika mabarabara ya mikoa mingi kuna “weighing stations” za kupima magari hayo yamebeba shehena ya uzito gani, pamoja na kuchunguza mambo mengine muhimu ya ki-trafiki. Dereva mwenye hatia, hutozwa faini pamoja na kupoteza pointi fulani kutoka kwa leseni yake, hadi kiasi cha kutoruhusiwa kuendesha Gari. Ripoti hiyo niliyotaja hapo juu inaeleza kwa ajali asilimia 1 husababishwa na gari lenyewe.
Napenda kuongezea kuwa baadhi yetu wanaweza kusema gari haliui; anayeua ni dereva, sawa na kusema kuwa bunduki haiui; anayeua ni mwanadamu. Gari halina budi kuwa katika hali nzuri ya kuendeshwa. Matairi yawe katika hali nzuri na kiasi cha upepo uliojazwa, na viungo vingine muhimu vya gari vichunguzwe mara kwa mara kuona na kuhakikisha kuwa havina kasoro. Gari ni lazima lifanyiwe “servicing”.Kuna ka-tabia ka kupenda kutunza pesa kwa madai kwamba gari bado linakwenda. Wamiliki hawapendelei kukarabati magari yao.Ajali nyingi zinazotokea huwa ni za mabasi mapya. Hii haina maana kuwa basi jipya halipati ajali.Mengine huanguka kwa sababu ya spidi (ku-“overtake”) na kujaza abiria na shehena (overload). Mara nyingi mabasi ya namna hiyo hushindwa ku-“balance” kutokana na mshituko wa kona au kwa ghafla kujaribu kukwepa wakati wa ku-“overtake”.Nchini Amerika ni Jimbo la Connecticut peke yake lenye 55 m.k.s. (majimbo mengi yanaendesha 60, 65, 70 na 75 m.k.s.). Lakini takwimu za spidi na ajali hazikubaliani. Hakuna uwiano kati ya spidi kali na kutokea kwa ajali! Pengine hii ni kwa sababu ya huduma za haraka za ambulance na hospitali katika kunusuru waliojeruhiwa. Kukosekana kwa huduma za namna hiyo nchini Tanzania kunawafanya waliojeruhiwa kutokwa damu sana.Lakini hapa Amerika endapo itatokea ajali, basi magari huwa yanavaana nyuma kwa nyuma.
Kumekuwepo na ajali nyingi za mashangigi nchini mwetu. Lakini hatuna utafiti yakini wa kuonyesha au kuelezea ni mashangigi ya aina gani au modeli gani, au magurudumu ya aina gani hupasuka pasuka na kusababaisha ajali.Wakati mwingine, gari au matairi yake huwa vina hitilafu ambazo madereva wengi hawazifahamu! Ajali nyingine hapa Amerika zimesababishwa na hililafu, kama nilivyoelezea hapo juu. Ikibainika kuwa aina au modeli fulani ya magari au matairi ndio yenye makosa, basi aina au modeli au matairi hayo yatarejeshwa viwandani.Je, Tanzania itahakikishaje kuwa hitilafu kama hizo, na makosa mengineyo yanadhibitiwa? Yasemekana Tanzania yetu ni maskini haiwezi kutengeneza barabara kama za Ulaya/Amerika au kuwa na teknolojia ya kisasa ya kudhibiti nidhamu ya uendeshaji na upakizi. Nakubalina na hilo hapo juu.Lakini kuna mengi ya kufanya kudhibiti ajali barabarani. Mabasi kutoka na kurudi Mwanza/Dar yanayopitia nchi ya jirani ingefaa yawe na madereva wanne. Mmoja kati ya Dar na Arusha (apumzikie Arusha); Arusha na Nairobi (apumzikie Nbi); Nairobi na Tarime (apumzikie Tarime); na Tarime na Mwanza (apumzikie Mwanza). Kila dereva aweze kuendesha kwa muda wa kati ya masaa manane na masaa kumi hivi. Mabasi yanayokwenda Lubumbashi (Kongo-Kinshasa) nayo yadhibitiwe kikamilifu: Dar hadi Iringa; Iringa hadi Tunduma; Tunduma hadi Kitwe. Kitwe hadi Lubumbashi.Kuhusu madereva, sioni sababu kwa nini kusiwe na matrafiki wa tarafa au wilaya. Hawa matrafiki wetu waheshimike na wapokezane zamu toka tarafa hadi tarafa au toka wilaya hadi wilaya.Na kama madereva watathubutu kuwahonga, watahonga mpaka lini? CID, TAKUKURU. na Usalama wa Taifa viwashughulikie!Yafaa sana mabasi yawekewe ratiba na yazifuate ili kuzuia hiyo “marathon” ya uchu wa kuchuma pesa. Tuwape madereva mafunzo bora ya usanii elekevu wao kupitia semina, majopo au mikutano sawa na “refresher courses” za kuzidi kunoa umahiri wa kuendesha. Pengine haitawezekana kuwakutanisha maderera wetu huko Ngurdoto Hotel au Bagamoyo!Lakini tunaweza kupitia kwenye restauranti za “Mama Ntilie” ili nao wapate mtaji wa kuendeleza ulishaji mijini kwa walalahoi.Kwa wale madereva wanaoendesha wakubwa, mara nyingi kumekuwepo na malalmiko ya hao madereva kutopata muda wa kupumzika wawapo safarini. Badala ya kumwambia dereva aende akapumzike na aje amchukue wakati fulani, dereva huyo analazimika kungojea kwenye gari bosi wake amalize shughuli rasmi au za ubinafsi hadi zaidi ya usiku wa manane! Dereva anaambiwa kuanza safari ndefu asubuhi na mapema, tuseme kurudi Dar es Salaam.Na wakati mwingine madereva hao hata posho hawapati vizuri!
Tatizo la kupakia abiria na shehena nyinginezo zaidi ya kilichoruhusiwa, limesababaisha ajali kwa vyombo vetu vya usafiri si barabarani tu bali pia relini, angani na majini.Gari la moshi lilishindwa kupanda miinuko na ghafla ku-“reverse” na kurudi lilipotoka. Ndege zetu nyingine zimeshindwa kuruka shauri ya uzito wa shehena (magunia ya vyakula na matunda). Meli, boti, mashua na mitumbwi yetu imezama shauri ya uchu wa pesa kutokana kujaza sana abiria na shehena. Umuhimu wa “servicing” uzingatiwe na kuelezeka kwa msemo wa mambo ya uganga, “Wakia moja ya kinga ni bora kuliko tani ya tiba”. Tanzania si masikini; ni tajiri. Tunafuja mapesa yetu bure. Fikiria, hao mawaziri karibu sitini ya 60 ni wa nini, kama sio kuzidi kutonesha kidonda cha umasikini wetu? Hawa “mawaziri” na “wizara” zao wanamaliza mapesa kwa mishahara ya wafanyakazi, kuwapamba kwa magari ya fahari na majumba, marupurupu, ubadhirifu, ufisadi, na kurudufisha huduma.Tulishindana na Benki Kuu ya Dunia, washauri wetu wa uchumi, kututaka tupunguze sekta ya umma (serikali) ambayo ilikuwa imetuna, mithili ya mwenye kitambi. Tukashauriwa kuipeleka “gym” ikafanye mazoezi ya kukonda; ikakonda! Lakini sasa tumerudia yale yale ya kuota kitambi, tena kikubwa zaidi! Ikiwa kitambi kwa binadamu leo hii ni “skandali”, basi hata kitambi cha serikali nacho ni “skandali”!Najua nchi kongwe (kama Uingereza, Ujerumani, Ufaransa) zilikuwa tayari na dola (the State) kabla vyama vya siasa kuanzishwa. Nchi changa (kama Tanzania) zilikuwa ni lazima ziunde vyama vya siasa ili zijenge (the State) na State ijenga nchi.
Kwa kifupi, chama tawala cha siasa ndicho kiliunda State ijenge nchi.Matokeo ya kuota kitambi kitambi hicho yalikuwa ni mafanikio ya kujenga nchi. Leo hii eti tunaambiwa mambo yamebadilika. Kuna kuoana baina ya sekta ya ummana ya binafsi. Ndoa hiyo ndio kitovu cha maendeleo ya kujenga nchi….bado tunajenga nchi mpaka leo!Ubinafsi tuliouona kwa darubini ya ujamaa kuwa kama dhambi, leo hii ni nyenzo muhimu ya kuleta eti maendeleo! Tunalipendelea sana Jiji la Dar es Salaam. Wengine kati yetu wanalifananisha na New York au Shanghai kwa madhari yake.Tuliache Jiji hili lilivyo bila ya kulinyonga.Lakini Jiji la Dar limeshindwa kudhibiti wingi wa magari kwenye barabara zilizotengenezwa wakati wa Gavana akiwa ndiye mwenye gari, na wakati wa kutaka kutoka na gari hilo, barabara zilifungwa.Mpaka sasa, serikali imekataa kuhamia Dodoma; inazidi kujenga nyumba za mawaziri mjini hapo Dar! Nchi imetumia mapesa mengi kwa ajili ya hayo “makao Makuu ya Dodoma” toka enzi za “Sir” George Clement Kahama! Na “over cost” yake inazidi kila mwaka,licha ya kutojua ni mapesa mangapi Mamlaka ya Mji wa Dodoma ilitumia kuwakopesha wafanyakazi wake kujijengea nyumba zao binafsi! Tuache kuhamia Dodoma! TAKUKURU mnayajua hayo!
Itatubidi tuunde utaratibu wetu wenyewe wa madaraka mikoani ili kuendeleza baadhi ya miji yetu mingine na kupunguza msongamano wa magari jijini Dar,ikiwa ni pamoja na watu kusafiri kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya kununua vitu na huduma. Niruhusu nifupishe orodha ya wizara zetu ziwe wizara 15 tu.Orodha iwe fupi kama mini-sketi lakini ndefu kiasi cha kusetri huduma za lazima, kama ifuatavyo:Dar es Salaam: Fedha na Menejimenti ya Utumishi wa Umma; Mipango (Mipango, Uchumi, Uwezeshaji na Kazi); Habari, Utamaduni na Michezo; Nje (Mambo ya Nje, Mashirika ya Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Mashariki); na Ulinzi na JKT.Dodoma: Uhusiano wa Ndani (Muungano, Siasa na Uhusiano wa Bunge); Elimu (Elimu, Ufundi, Sayansi na Teknolojia; Sheria (Katiba na Utawala Bora); pamoja na kuwa Makao Makuu ya Vyama vya Siasa.Arusha: Maendeleo (Makazi, Jamii, Jinsia na Watoto); Mambo ya Ndani na Usalama wa Raia; ikiwa ni pamoja na kutoa huduma kwa Nairobi na Kenya Kusini.Mwanza: Afya na Ustawi wa Jamii, na Mazingira Nishati, Madini na Miundombinu, ikiwa ni pamoja na kuwa jiji la kuhudumia biashara ya Ziwa Victoria, Uganda, na sehemu za Kenya Magharibi.Kigoma: Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Maendeleo ya Vijana, ikiwa ni pamoja na kutoa huduma kwa biashara ya Ziwa Tanganyika, na DCR Mashariki.Mtwara: Uzalishaji (Viwanda, Biashara na Masoko).Mtwara hauna budi kupewa hadhi mpya kama mji wa huduma za mpango wa “Mtwara Corridor” (Tanzania, Malawi na Zambia na sehemu za Msumbiji Kasikazini). “Daraja la Umoja” kwenye Mto Ruvuma ili kuunganisha Tanzania na Msumbiji sasa linajengwa baada ya kulisubiri kwa miaka mingi tangu Awamu ya Kwanza – wakati Msumbiji inapata uhuru wake!Mbeya: Ardhi, Maji, Mifugo, Kilimo, Chakula na Ushirika; ikiwa ni pamoja na kutoa huduma kwa nchi za Malawi na Zambia.
Ni kitu cha kutia shime kuona kuwa uwamja wa ndege wa kimataifa unaendelea kujengwa mjini Mbeya.Uwanja huu utasaidia pia kuinua maendeleo kwa mikoa ya kusini. Tuwe na Mawaziri Wadogo 15 tu wakisaidiwa na nyongeza ya Makatibu Wakuu, endapo italazimika. Wizara hizi zitagawanya katika mafungu matano.Kila fungu litasimamiwa na afisa mwenye sifa za nidhamu na uchapaji kazi ili kuweza kufuatililia maazimio na miradi mbali mbali ya serikali kulingana na”manifesto” ya “chama tawala” (na kudhibitiwa na “chama tawala kivuli” kikisaidiana na vyama vingine vya siasa. Afisa huyo asaidiane na tawala za mikoa.Wakuu wa mikoa na maafisa wao wasaidizi (hadi wilayani) wafanye kazi karibu zaidi ili kufanikisha wajibu wao kwa wananchi. Naona kumekuwepo na kuteuliwa kwa maafisa wapya wa kumsaidia Waziri Mkuu katika kusimamia mipango ya sera za serikali.
Hii itasaidia sana kuangalia ni vipi tunavyotekelza yale ya Hotuba Rais aliyotoa alipokifungua Bunge la Awamu ya Nne. Na itawasaidia sana Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kuweza kufuatilia, kukagua na kudhibiti miradi na maazimio yaliyowekwa.Sambamba na kupunguza wingi wa wizara, juhudi ifanywe pia kupunguza idadi ya wa-Bunge wetu!Wa-Bunge wengine “hulala sana”! Sioni sababu kwa nini kila wilaya isiwe na na m-Bunge mmoja tu wa kuiwakilisha katika Bunge la Taifa, Dodoma! Shughuli za “wa-Bunge” wa Seriali za Mitaa wapewe hadhi na majukumu makubwa ya kusimamia maendeleo katika sehemu zao za majimbo ya uchaguzi, kulingana ana usemi wa serikali za mitaa wa nchi moja iliyoendelea: “Using local people, with local knowledge to serve the local area”.Huku tukitilia mkazo wa sera ya “madaraka mikoani” (kama kweli bado inatekelezwa), mikoa yetu haina budi kushiriki zaidi katika kupanga na kutekeleza hayo ya “maisha bora kwa kila m-Tanzania”, ikiwa ni pamoja na kudhibiti athari za ajali barabarani. Naamini Tanzania si masikini; ni tajiri! Fikiria leo hii tunajivuna kuwa tu nchi ya tatu katika Bara la Afrika kwa uzalishaji wa dhahabu!Michanga ya dhahabu inachimbwa na kusafirishwa nchi za nje.Makampuni ya kigeni kwa muda wa miaka mitatu ya kuvuna dhahabu yetu bila kulipa kodi. Yanaweza kuichimba usiku na mchana kabla ya miaka hiyo mitatu kuisha. Miaka mitatu iishapo, ili yaanze kulipa kodi, aidha yanaweza kulalamika kuwa yatafunga migodi kutokana na uhaba au ugumu wa kuchimba dhahabu yenyewe.Au wakati mwingine makampuni hao yanatishiwa na wakubwa wenye kutaka kuila Tanzania kwa kuyalazimisha kuwahonga ili waidhinishe mikataba hiyo na kuanza kulipa kodi. Hii inayafanya makampuni hayo kuuza “business” kwa wamiliki wengine wa kigeni au kuunda kampuni mpya yenye jina tofauti!Tatizo hili lipo pia katika mikataba ya gesi yetu.Utajiri wa madini na gesi yetu umeingiliwa na unyarubanja unaotekelezwa na wawekezaji wa kigeni Makampuni hayo yamepewa dhahabu ya bure. Mikataba tunatiliana na hao wawekezaji wageni ikiwa na kipengere cha “production sharing agreement”, psa (kugawana uzalishaji).Lakini inaonekana kuwa wanaonufaika na kipengere hiki ni wawekezaji, ambao kila mra huongeza vikampuni vingine vya kigeni vidogo vidogo na kunufaika. Je, huo si “unyarubanja”? Hakuna hata kikampuni cha wazawa kinachonufaika na kipengere hicho, kama ilivyo katika mikataba ya madini na gesi yetu.Labda, Tanzania iko pembeni mwa kipengere hicho! Tangu mkataba wa kwanza kusainiwa (na pengine mpaka sasa hivi) kuna kutafuta “production sharing agreement”, PSA (kugawana uzalishaji). Si ajabu mzozo wa Buzwangi umetokana na “production sharing agreement”, kama ilivyo mikataba mingi ya madini na gesi yetu!Ukifungua http://www.globeinvestor.com/servlet/story/RTGAM.20071030.wbarrick1030/GIStory/ utapata ripoti ya mgomo unaoendelea huko kwenye Mgodi wa Barrick. Mwisho wa stori hii kuna para moja juu ya vile walivyovuna mwaka uliopita: “The mine, which Barrick acquired in 1999, produced 330,000 ounces of gold last year at a total cash cost of $339 (U.S.) an ounce. It had proven and probable reserves of 11.2 million ounces as of the end of last year.” Sijui kama wameanza kulipa kodi au kutupatia 3% (royalities) zetu? Hata kama wakitupa kiasi hicho, Tanzania itapata dola ngapi? Fanya hesabu! Mwisho, naipongeza serikali kwa juhudi zake za kuwapa msasa kidogo madereva. Lakini hii haitoshi kabisa. Naomba juhudi hii isiwe ndani ya majengo tu bali huko nje barabarani ambako ajali hutokea.Matrafiki wafanye hiyo kwa maadili ya hali ya juu (mithili ya madaktari na wahubiri dini) ili kuokoa maisha na mali ya wa-Tanzania.
Hivi karibuni tulizawadishwa na serikali ya Amerika (kupitia mfuko wa Rais wa Millennium Challenge Corporation - MCC) ya zawadi (“grant”) ya dola 698 milioni kuboresha mabarabara nishati na maji nchini kwa kipindi cha miaka mitano.Pili, kulikuwa na habari kutoka Makao Makuu ya African Development Bank mjini Tunis kuwa Benki hiyo imetoa kiasi cha dola za ki-Marekani million 92 (72%) (serikali ya Tanzania itagharimia 28%) kwa ajili ya kutengeneza mabarabara ya mikoa ya Dodoma na Singida ili kuuunganisha mikoa na mikoa ya kaskazini hadi Kenya.Je, ki-mapatano, mapesa hayo yatatumikaje katika kudhibiti baadhi ya mienendo mibaya yetu inayosababisha ajali barabarani?

Wednesday, March 18, 2009

Wananchi Wawachoma Moto Waporaji wa Pikipiki Tanga!

Wananchi wenye hasira wakishirikiana na waendesha pikipiki za kukodi(bodaboda), Wilayani Korogwe, wamewaua kwa kuwachoma moto watu wawili wanaotuhumiwa kuiba kuiba pikipiki ya kijana mmoja aliyelazwa katika hospitali ya Magunga.
Kamnda wa polisi mkoani Tanga, Nyakoro Sirro, alithibitisha habari kuhusu tukio hilo.
Hata hivyo diwani wa Potwe, Rashid Mdachi alidai kuwa limetokana na 'uzembe' wa polisi wilayani Muheza, kushindwa kwenda kuwakamata wahalifu hao mahali walipokuwa wamejificha, katika kijiji cha Kilometa Saba, wilayani Muheza.
Akisimulia tukio hilo, Diwani wa Potwe, Rashid Mdachi, alisema Machi 14 mwaka huu, vijana hao waliouawa, walikwenda Manundu Korogwe na kukodi pikipiki ya Haji Ramadhani na kumtaka awapeleke kijiji cha Bombani kupitia njia ya Potwe, ambako kuna msitu na walipofika katika ya vijiji vya Potwe na kimbo vijana hao walimshusha na kuanza kumkata mapanga kichwani na mikononi hadi alipozirai. Baada ya kuona 'wameshammaliza' wakachukua pikipiki na kupotea. Lakini kijana huyo alijikokota hadi kijiji cha jirani na kupata msaada ndipo watuhumiwa wakaanza kutafutwa na kukamatwa.
Watuhumiwa waliochomwa baada ya kupigwa katika eneo la Manundu wilayani Korogwe ni, Hatibu Tobi(24) Mkazi wa Mnyuzi Korogwe na Juma Denis Kiango(31).

DOKEZO LA LEO!

"LESENI HAIENDESHI GARI, NI BINADAMU NDIYO ANAENDESHA GARI KWA HIYO KUKAGUA LESENI TU HAITOSHI"

MWENDESHA PIKIPIKI ANUSURIKA!

Katika kile kinachoonekana kuwa mwendelezo wa vitendo vya kiharamia dhidi wa waendesha pikipiki wanaobebaba abiria maarufu kama 'boda boda au mchubuko', juzi usiku alinusurika kuuawa na watu wasiojulikana. Wakisimulia mkasa huo, baadhi ya waendesha pikipiki wa eneo la mbezi kwa Musuguri wanasema kwamba, mwenzao alikodishwa na kijana amabaye hawamfahamu na alitaka kupelekwa eneo la 'Kwa Chale' kupitia njia ya Bwaloni. Wasema alimuelekeza huko lakini walipofika alidai amsogeze mbele zaidi. Na mwendesha pikipiki alishtuka na kujiandaa lakini walipofika mbele kidogo ya hapo kwa Chale, walijitokeza vijana wawili waliokuwa wamekaa pande zote mbili za barabara na kuinua waya ambao ulimkaba dereva wa pikipiki na kuanguka.
Lakini kwa kuwa ilikuwa majira ya saa moja usiku ambapo wapita njia walikuwa wengi, kijana huyo alipiga kelele na wasamaria wema walipojitokeza kiasi cha kuwafanya wezi hao wakimbie na kutokea gizani.

Tuesday, March 17, 2009

Wakati Umefika wa SUMATRA na Polisi Kuachana na Dhana Kuwa wao Wanajua Kila Kitu!

Technograph haiwezi kunusuru maisha ya watu.
Hivi karibuni Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) ikishirikiana na Jeshi la Polisi Kikosi Cha Usalama Barabarani wametangaza amri kuwa wamiliki wa mabasi ndani ya kipindi cha miezi sita ijayo magari yao yawe yameweka mikanada kwenye kila kiti na chombo kinachoratibu mwendokasi wa gari (Technograph).
Amri hii imeshangaza wengi na darubini kuanza kumulika na kujiuliza kama wenye dhamana ya kuamua mambo kama haya wana dhamira ya dhati ya kuingiza teknolojia mpya ili iweze kumsaidia na kulinda maisha ya watanzania au nao ni mateka wa wale wanaotaka kuigeuza nchi yetu kuwa jalala la kutupia vitu vilivyopitwa na wakati.
kama si mateka wa hilo, basi kuna wajanja wamebuni mradi wa kujipatia fedha wa kuuza vifaa hivyo kwa visingizio vya kuingiza teknolojia mpya kudhibiti ajali kwa kisingizio cha kunusuru maisha ya wananchi na maliz zao. Na mara nyingi zoezi kama hili hufanyika kama si mwanzo wa muhula wa utawala basi huwa mwishoni mwa muhula.
Amri hii ni ushahidi mwingine unaoonyesha kuwa licha ya nchi yetu kuwa na wasomi katika kila sekta lakini wasomi hao ama wamestaafu kufikiria au hawasomi na kufuatilia mambo mapya yanayoweza kuisaidia kuleta ufanisi. Matokeo yake wanadhani kutoa amri zilizopitwa na wakati zitawafanya waonekane ni wachapa kazi na wana uchungu na nchi.
Mwaka 1996 kulipozuka mvutano kati ya serikali na wamiliki wa mabasi juu ya kufunga vidhibiti mwendo, wamiliki wa mabasi walipendekeza badala ya kufunga vidhibiti mwendo, kifungwe chombo kinachoonesha mwendokasi wa safari nzima ya basi hizo(technograph) lakini serikali kwa ubabe ilikataa ushauri huo na kulazimisha ule wake.
Leo miaka 13 imepita tangu serikali ikatae pendekezo la kufunga chombo cha technograph kwa madai kuwa vidhibiti mwendo vimeshindwa kuzuia ajali. Serikali hiyo hiyo sasa inaamrisha kufungwa kwa technograph teknolojia ambayo sasa imeshapitwa na wakati na haiwezi tena kudhibiti ajali wala kukisaidia chombo chochote cha dola zaidi ya mmiliki.
Kwa faida ya wasomaji technograph ni chombo kinachofungwa kwenye gari na funguo hubaki kwa mwenye basi. Gari linapokwenda safari na kurudi mmiliki hufungua chombo hicho na kutoa kadi inayoonyesha mwendokasi wa gari kwa safari yote. Polisi wa Usalama barabarani hawezi kufungua chombo hicho njiani kwa vile funguo zipo kwa tajiri.
Chombo hicho ni kama kile cha kwenye ndege kiitwacho 'kisanduku cheusi' ambapo hadi ajali itokee ndipo hutafutwa ili kujua kipi kilichosababisha ajali, ni mwendokasi au vipi? Sasa chombo hicho imeamriwa kifungwe ndani ya miezi 6 tu muda huo ni mfupi hata kwa wasimamizi wa sheria barabarani kujiandaa kujua namna ya kusoma chombo hicho.
Kinachoshangaza, vyombo vinavyosimamia sheria na taratibu za usafiri wa nchi kavu na majini, wanapaswa kwanza kufanya utafiti wa kina kabla ya kuja na amri mpya ambazo haisaidii kutatua matatizo ya usafirishaji zaidi ya kuongeza gharama za uendeshaji na hivyo serikali kushindwa kuwalinda wawekezaji wa sekta hii ambao wengi ni wazalendo.
Wakati SUMATRA na polisi wanafikiria kufungwa kwa chombo kilichopitwa na wakati cha technograph, baadhi ya kampuni hapa nchini sasa zinatumia mfumo mpya kabisa wa kudhibiti mwenendo wa mabasi ujulikanao kama fleet management system au tracking system unaounganishwa kwenye mtandao hutoa ripoti hapo hapo.
Basi hufungwa chombo kinachofanana na flashi ya kompyuta. Kila dereva ana namba yake ya siri. Endapo kutakuwa na dereva hana namba ya siri lakini akataka kuliendesha basi hilo halitawaka abadani. Chombo hicho kina uwezo wa kuonesha basi hilo lipo wapi, linakwenda mwendokasi upi na hali ya hewa ikoje hapo lilipo kila baada ya dakika mbili.
Chombo hicho huonyesha hata makosa ya kiutaalamu yaliyofanywa na dereva na muda aliofanya kosa hilo endapo mtandao wa GSM ukienea nchi nzima. Mtandao huu unaweza kulionesha basi hilo muda sawia na hapo lilipo kwenye runinga ya kompyuta. Teknolojia hii ingekuwa sahihi kutumika na polisi na SUMATRA kwa sasa.
Kumekuwapo na vikao vya mara kwa mara na wadau kuhusu uboreshaji wa sekta ya usafiri lakini vikao hivi vinaonesha ni kiini macho cha waliokabidhiwa dhamana ya usimamizi na uboreshaji wa sekta hii ili kuhalalisha mambo wanayodhani yana maslahi kwao zaidi kuliko pande zote zinazohusika yaani Mwnachi, serikali na mwekezaji.
Amri kalikali zinapotolewa na zisipofanya kazi ndipo wahusika huanza kufikiria kuwatafuta wadau na kuketi nao kujadili tatizo, ni vizuri wadau wakahusishwa kabla ya uamuzi kufanywa na pia wadau hao wakashirikishwa pia katika maandalizi kabla amri hiyo kuanza kutekelezwa ni dhahiri technograph haitasaidia kudhibiti ajali.
Mamlaka za usafiri nchini Kenya ziliamua tangu mwaka 2003 kila basi linalobeba abiria hadi matatu (hapa kwetu daladala) kila kiti kiwe na Mkanda wa usalama wa abiria.
Wametekeleza kwa nguvu zao zote hadi mabasi ya watanzania yafanyayo safari zake huko yametekeleza amri hiyo na kila abiria abiria anatekeleza amri hiyo kwa umakini.
Hapa nchini yapo mabasi yenye mikanda lakini abiria kila wanapoambiwa kufunga mikanda hiyo hudharau.
Hakuna sheria inayowabana abiria, endapo kungekuwepo na sheria inayowabana abiria kama ilivyo huko Kenya abiria akikutwa hakufunga mkanda hutozwa faini ya shilingi 500 za nchi hiyo la sivyo mikanda hiyo itakuwa mapambo (Habib Miradji, Mwananchi Machi 8).
HOJA: Nimekutana na hii makala ambayo nilionelea ni vema wasomaji wangu wakapata ladha kama niliyoapata mimi na kuweka mjadala wazi ili tuchangie na kuona ni jinsi gani labda mamlaka husika zitazinduka na kujua kwamba Tanzania ya sasa sio ya mwaka 47. Watanzania wapo macho!!!

Monday, March 16, 2009

Leo Kutoka Taasisi Ya Tiba Ya Mifupa na Magonjwa Ya Ajali Muhimbili(MOI)

Pikipiki nazo.....haya!!!

Utafiti uliuofanywa mwisho wa wiki Katika Taasisi ya Mifupa(MOI) unaonyesha kwamba Idadi ya waendesha pikipiki wanaopata ajali bado imesimama juu! kwa mfano katika siku ya jumamosi walikutwa waendesha pikipiki wawili wamelazwa katika Taasisi hiyo wakiwa na majeraha mbalimbali kama ifuatavyo;Godfrey Ndunguru(19) Kutoka Tegeta, amekutwa wodini akiwa amevunjika mguu na kupata majeraha sehemu mbalimbali za mwili. Akielezea tukio hilo anasema kwamba, siku ya tukio yeye alikuwa anaendesha pikipiki za "boda boda" au kwa jina jingine "mchubuko" ambazo hubeba abiria. Alipokuwa njiani abiria wake aliomba asimame ili ajisaidie. Aliegesha pikipiki kando ya barabara akiwa pembeni ya gari. Anasema mara ilikuja gari aina ya toyota 'Chaser' ambayo dreva alionekana kushindwa kuimudu ndipo aligonga pikipiki na kumpitia na yeye!


Mwingine ni Kulwa Slim(37) Mkazi wa Tegeta, Ansema siku ya tukio aligongwa na gari akiwa kwenye pikipiki anatoka Tegeta kwenda Kawe ndipo gari ndogo aina ya Toyota 'Corolla' ilimgonga. Amevunjika mguu wa kulia na kupasuka goti.


Christian Malenda(40) kutoka Morogoro, amevunjika mguu mara mbili . Anasema siku ya tukio alikuwa 'round about' anasubiri gari jingine lipite mara trekta lilikosa mwelekeo na kumgonga.
POLE:Tunawapa pole majeruhi wote na kutoa wito kwamba, ni lazima suala la ajali za pikipiki liangaliwe kwa makini.

Saturday, March 14, 2009

DOKEZO LA LEO!

"WAENDESHA MAGARI NI WENGI, LAKINI MADEREVA NI WACHACHE"

Thursday, March 12, 2009

Mpaka lini Tutapangwa kama Hivi?Sasa Tuseme!



Hawa ni baadhi ya waliopoteza maisha baada ya ajali ya gari. Kwa kweli Inauma sana, kila mmoja anawajibika kukemea uzembe wa wale wote wanaochangia kutokea kwa ajali kama hii.Mimi nimekemea, wewe je?
blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker