Saturday, February 14, 2009

AGONGWA NA KUFA PAPO HAPO!

Mwendesha pikipiki ,yenye namba za usajili T 831 AVN, Rajab Said (31) amefariki baada ya kugongwa na gari katika barabara ya Mbande jijini. Abiria aliyekuwa amebebwa katika pikipki hiyo aliyejulikana kwa jina la Mohamed Said alijeruhiwa vibaya sana. Gari lililosababisha nii aina ya Toyota Corolla yenye namba za usajili T956 ADQ lililokuwa likiendeshwa na Ramadhani Kapata(32) akitokea Chamazi kwenda Mbagala. Hiyo ni kwa mujibu wa Taarifa ya Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Emannuel Kandihabi.
katika tukio jingine, Kamanda wa Mkoa wa kipolisi Ilala,Faustine Shilagile, alitoa taarifa kwamba Kulwa Lucas au Lugame mkazi wa mtoni sabasaba alikufa papo hapo baada ya kugongwa na gari akijaribu kuvuka barabara. Ajali ilitokea jana majira ya saa 1.30 usiku katika barabara ya Nyerere katika njia panda ya Jet.

AJALI! AJALI! AJALI!

Hii ni wiki ambayo imepambwa na matukio ya ajali kama ilivyokuwa wiki iliyopita. Ndani ya wiki, kuanzia tarehe 7 Februari hadi kufikia leo ambapo watu wanaadhimisha siku ya wapendao ni mengi yametokea na si vibaya kama tukiyaangalia kwa makini na kutafakari kama ajali zinaashiria kupungua au kuongezeka hapa nchini.

Kama kawaida timu ya Mr. Bobos Class imekuwa ikipitia Taasisi ya Tiba ya Mfupa(MOI) ili kungalia majeruhi waliopokelewa katika Taasisi hiyo. kwa Mujibu wa Taarifa za Ofisa Mawasiliano wa MOI Bwana Jumaa Almasi, ndani ya wiki inayoishia leo, wamepokea majeruhi zaidi ya 50 na wengi wao wameruhusiwa baada ya kupata matibabu na baadhi waliokuwa na majeraha makubwa walilazwa. aliwataja baadhi ya majeruhi kuwa ni: Athumani Ramadhani(40) aliyevujika mguu, Mathias Juma(33) aliyepata ajali na kusagika mkono kutoka kimbiji, Castory Mussa(19) aliyevunjika mfupa wa paja na Eric Nyaonga kutoka Bagamoyo aliyevunjika mfupa wa paja na kupata maumivu ya kichwa.

Wengine ni:Michael Samwel Miyoyi(39), aliyepokelewa kutoka Hospitali ya Amana akiwa amepata majeraha mwilini na maumivu ya kichwa, Peter Sylvester(54) aliyepokelewa kutoka Hopsitali ya Tumbi, Kibaha akiwa amepata aliyeumia kichwa, Ahmed kandoro (23) aliyepata maumivuu ya kichwa, Joseph Mpanda aliyevunjika mguu chini ya goti na Joseph Robert (36) aliyepelekwa na polisi kutoka Temeke akiwa amevunjika mguu wa kushoto sehemu ya paja.

Kufuatana na Taarifa ya Bw. Almasi, wodi za MOI kwa sasa hivi zimejaza wagonjwa kuliko uwezo wake kutokana na kupokea majeruhi wengi sana.

Bwana Almasi alimaliza kwa kutoa ushauri kwamba, wakati huu ambao watu wengi wanasherehekea Siku ya Wapendanao "Valentine Day", ni vema watu wote wakazingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali zisizo za lazima, kwani kwa muda mrefu imeonekana Wakati wa sikukuu kama hizi ajali huongezeka sana.

Wakati huo huo, taarifa zilizotoka katika gazeti la majira zilieleza kwamba askari mmoja amekamatwa na vitu vinavyoaminika kuwa vya wizi vilivyopatikana kwa majeruhi wa ajali, jambo ambalo linasikitisha sana kwani kumekuwa na malalamiko sehemu mbalimbali za nchi kwamba kuna watu ambao baada ya tukio la ajali wao hufanya kazi ya kuwapora majeruhi na maiti. lakini la askari amabaye anatakiwa kulinda usalama, kukutwa na vitu kama hivyo inashtua sana.
Gazeti la Alasiri jana na leo limeripoti kuhusu ajali mbalimbali. ajali ya jana ni ile iliyopelekea watu 6 kufa papo hapo na leo Alasiri limeripoti kwamba lori aina ya scania lenye namba za usajili T110 AAG na tela lenye namba T 773AEA lilokuwa likitokea Rufiji kueleka Dar es salaam liliacha njia , kupinduka na kusababisha vifo vya watu watatu kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa polisi Mkoa wa Pwani Absalom Mwakyoma. Pia alieleza kwamba, katika ajali nyingine gari aina ya Toyota Landcruiser lenye namba T354 AEC lilimgonga mwendesha baiskeli mmoja ambaye alifariki baada ya kufikishwa Hospitali ya Tumbi. Aidha alieleza zaidi kwamba katika eneo la Ubena Zomozi gari lenye namba T 932 AGK lilimgonga kijana anayeitwa Simon Kaluna (22) na kufa papo hapo.

Saturday, February 7, 2009

SUMATRA YAANZA KUNG'ATA

Mamlaka ya Usafirishaji Majini na Nchi Kavu(SUMATRA) wameanza zoezi la operesheni ya kuondoa magari madogo ya abiria au "vipanya" katikati ya jiji la Dar es salaam ambayo leseni zake zimeisha muda.
Kwa mujibu wa Afisa mwandamishi wa Mamlaka hiyo Bwana Walukani Luhamba, wame amua kufanya zoezi hilo pamoja na kukamata magari mengine yenye makosa mbalimbali kama vile kukatisha ruti, kutoza nauli za juu, kunyanyasa wanafunzi, sare chafu na lugha chafu.
Katika kamata kamata hiyo magari 100 yameshakamatwa na wamiliki wake watatozwa faini kwa mujibu wa sheria. Mr. Bobos Class tunapongeza jitihada hizo kwani tuna imani kwamba itasaidia kupunguza ajali zisizo za lazima.(habari kwa hisani ya dullonet.com)

MTOTO AGONGWA NA KUFARIKI

Mtoto mwenye umri wa miaka 7, mwanafunzi wa darasa la kwanza Osama Hamidu amegongwa na gari na kufariki. Kamanda wa polisi Mkoa wa Temeke, Emmanuel Kandihabi alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 1.30 asubuhi katika barabara ya Kilwa eneo la Mbagala rangi tatu jijini Dar es salaam. Alisema maiti ya mtoto huyo imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Amana.
Dreva wa gari lililo mgonga mtoto huyo, Mustafa Saidi(52) anashikiliwa na polisi.

AJALI ZAIDI, VIFO ZAIDI!

Taarifa zilizopatikana jioni hii zinasema kwamba taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) impeokea waogonjwa wanne ambao wamelazwa kufuatia ajali zilizotokea jana na leo alfajiri. Waliopokelewa jana ni Mwema Nicolaus (27) ambaye amepata maumivu ya kichwa na Kajim Ally(22) ambaye alivunjika mkono wa kulia. Waliopokelewa alfajiri leo hii ni Abdulrahman Shiloo(34) aliyevunjika mguu na Mudhihir Ubagala(35) ambaye amevunjika mfupa wa paja. Afisa Uhusiano wa MOI, Bw. Jumaa Almasi amethibitisha kuwapokea wagonjwa hao.
Wakati huo huo, imeripotiwa kwamba ajali 384 zilua watu 58 na kujeruhi 487 mkoani Kigoma mwaka jana. Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana nifahamishe.com zikimnukuu Mkuu wa polisi Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kigoma SSP Said Mbaga. Hii ni kutokana na ajali 211 zilizosababisha majeruhi 487 na ajali za kawaida 121.
SSP SMbaga alisema kuanzia Januari 2009 mpaka mwezi huu wa February kumekuwa na jumla ya ajali 18 ambapo mtu 1 amepoteza maisha. mbali na hayo imefahamika kwamba kesi 68 za makosa mbalimbali ya usalama barabarani zilifikishwa mahakamani, kati ya hizo 33 wahusika walitiwa hatiani na nyingine 31 bado zinasikilizwa.
Hapo jana nifahamishe.com ilitoa habari ya ajali iliyohusisha magari yapatayo saba iliyotokea katika barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam imesababisha vifo na majeruhi kadhaa waliokimbizwa hospitali wengine wakiwa katika hali mbaya sana
Ajali hiyo imetokea leo asubuhi, maeneo ya Kimara Bucha katika barabara ya Morogoro ambayo inasemekana gari aina ya RAV 4 kupinduka, pia yakiwemo mabasi mawili ya daladala aina ya Isuzu Jorney na Toyota Hiace.Mengine yaliyohusika katika ajali hiyo ni Toyota LandCruiser, Toyota Hilux, Nissan Patrol na RAV 4 ambayo yote yalikuwa yakitokea Mbezi kuelekea Mjini.Inasemekana kuwa gari moja kati ya hayo lilileta hitilafu ya breki barabarani na kusababisha kutoweza kusogea pembeni ndilo lililosababisha mengine sita yaliyo nyuma yake kulivaa na kugongana kimpigo.
Katika Mtandao huo leo hii kuna taarifa kwamba mtu mmoja amefariki dunia baada ya kugongwa na kusagwasagwa na treni wakati alipopitiwa na usingizi katikati ya reli ya Tazara eneo la Ukonga jijini Dar es Salaam.
Mr. Bobos Class tunasikitika sana kufuatia ongezeko la ajali hapa nchi na kusababisha vifo kadhaa na uharibifu wa mali unaosababisha hasara kubwa.

Thursday, February 5, 2009

WANNE WALAZWA KWA AJALI MOI

Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) leo imepokea usiku wa kuamkia leo wamepokea wagonjwa wa ajali wanne kwa mujibu wa Afisa Uhusinao wa Taasisi hiyo. Waliopokelewa ni Sefu Lenjeka(42) ambaye alipokewa MOI kutoka Hopitali ya Mwananyamala ambaye aliumia kichwa (Mild Head Injury), mwingine ni Charles Lupande(19) aliyevunjika mfupa wa paja(femur), Juma Mwadia(29) ambaye alipokelewa kutoka Hopitali ya Amana na kuumia mguu wa kulia, na wa mwisho ni Michuzi Chande ambaye amefahamika kuwa ni mgonjwa wa akili ambaye aligongwa na gari na kuumia mguu wa kulia na kupata maumivu ya kichwa (head injury) hali iliyosababisha apokewe kama mgonjwa asiyetambulika (unknown male) lakini baadaye alitambuliwa na ndugu.

Sunday, February 1, 2009

MAISHA ZAIDI YATEKETEA!

Wiki inayoishia leo zimetokea ajali ambazo zimeteketeza maisha ya wananchi kadha na kuwaacha wengi wakiwa majeruhi.
kwa kujibu wa gazeti la "Habari Leo" la tarehe 31 Januari 2009, lilikuwa na kichwa kisemacho "Ajali zaua watu 15", watu 15 walikufa katika ajali zilizohusisha magari na treni katika mikoa ya Daresalaam na Morogoro huku zikiacha majeruhi zaidi ya 20.
Katika ajali hizo mbili iliyotokea Dar es salaam watu 9 walikufa papo hapo na wengine 10 kujeruhiwa na ajali ilitokea maeneo ya Jet Club, Kipawa barabara ya Nyerere, wakati Morogoro watu 6 walikufa papo hapo na wengine 10 kujeruhiwa katika ajali ya treni ya Kampuni ya Reli Tanzania(TRL).
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, inaonekana kwamba ajali zote zilisababishwa na uzembe wa madereva. Dreva wa dalala lenye namba za usajili T700 Toyota Hiace "kipanya" lililoua watu 9, aliligonga lori lenye namba za usajili T452 ACP ambalo lilikuwa limepinduka. Inasemekana "kipanya" kilikuwa kinafanya safari za usiku tu kutokana na leseni yake kumaliza muda wake.
Kwa kweli inasikitisha kuona kwamba, wakati jitihada za makusudi zinafanywa na wadau mbalimbali ili kuokoa maisha na mali za wanaopata ajali, bado kuna wachache ambao wanafanya uzembe wa makusudi na kurudisha nyuma jitihahada zote hizo.
Mr. Bobos Class tunaamini kwamba sheria itachukua mkondo wake na wale wote watakaobainika kuwa na makosa ya uzembe watachukuliwa hatua kali za kisheria.
blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker