Sunday, January 18, 2009

BARAZA NALO LAGUSWA.

Kile kinachoonekana kuwagusa wadau mbalimbali wa nyanja ya usafiri sasa kimeligusa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Nchi Kavu na Majini(SCCC), nacho ni ongezeko la ajali zinazoteketeza maisha ya watanzania wengi kwa sasa hivi. Mwenyekiti wa Baraza hilo Bwana Gilliard Ngewe katika taarifa yake ya wiki hii alisema kwamba “…ili kuondokana na matatizo ya upandishaji wa nauli kiholela, alitoa wito kwa taasisi zote zinazohusika na sekta ya usafiri kuanza kuandaa mchakato wa kuendesha usafiri kwa njia ya makampuni. Alifaamisha kuwa kampeni hiyo itaenda sambamba na kutoa elimu kwa madereva kuhakikisha madreva wanapimwa kiasi cha pombe walichokunywa wakiwa wanaendesha gari na kwamba dereva yeyote atakayekamatwa anaendesha gari akiwa amekunywa pombe atanyang’anywa ufunguo na hataruhusiwa kuendesha kwa siku hiyo.lengo likiwa ni kupunguza ajali za barabrani zinazotokea mara kwa mara na kuua watu wengi”.
Inatia moyo sana kuona kwamba kila mdau katika nyanja ya usafiri anaguswa na tatizo hili la vifo visivyo vya lazima vinavyosababishwa kwa kiasi kikubwa na uzembe wa madereva kwa kuendesha wakiwa wamelewa au kutozingatia sheria za barabarani na matokeo yake ndio hayo tunayoyaona. Wengi wanaguswa wanaposikia kwamba ajali imeua makumi ya watu, lakini husahau baada ya muda mfupi tu. Ni jukumu la kila mdau na hata mwananchi wa kawaida kupinga vifo visivyo vya lazima vinavyotokana na uzembe wa madereva.(Kwa msaada wa gazeti la Mwanachi na vyanzo vingine)

No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker