Showing posts with label Amputations Victims. Show all posts
Showing posts with label Amputations Victims. Show all posts

Friday, April 24, 2009

Kutoka MOI!Shattered Dreams?


Kijana Salum Saleh baada ya kukatwa miguu yote
Kijana Salum Saleh(19) amelazwa taasisi ya Tiba ya Mifupa na Magonjwa ya Ajali Muhimbili (MOI) kufuatia kupata ajali mbaya iliyosababisha yeye kupoteza miguu yote miwili baada ya madaktari kuona uwepo wake unahatarisha maisha ya Salum.
Anasema kwamba,yeye ni mchuuzi wa nguo mikononi, na siku hiyo alipanda daladala ili kutoka Mwenge kwenda Tazara. Dereva wa gari hilo alikuwa anaendesha mwendo kasi na abiria wakaanza kumfokea ili apunguze. Yeye alikuwa miongoni mwa abiria waliokuwa wanakemea mwendo wa dereva huyo na alimfuata na kumwambia.Hii ilileta mtafaruku kidogo na ndipo wakati anashuka makondata walimsukuma, gari likampanda miguuni na kumsukumia katika mfereji wa maji machafu kiasi cha kumpa infection ambayo baada ya masaa machache miguu ilibadilika rangi na kuanza kutoa harufu mbaya sana.
Ili kuokoa maisha yake, ilionekana ni vema miguu yote iondolewe. Kijana Salum(pichana)amepoteza miguu yote,imebaki sehemu ndogo tu ya paja. Salum amekuwa mlemavu ghafla, ndoto za maisha yake zimeisha badilika na anakata tamaa ya kuishi.

(Salum Saleh,19,lost both legs following motor traffic accident. He was pushed by the bus conductor of a passenger bus he was in, following a misunderstanding between him and the bus operators. Having fallen down the bus tyres ran over his legs and pushed him in a drainage with contaminated water.His open wounds were infected instantly, which led to severe gangrene. Then,both limbs had to be amputated up to his thighs to save his life. Salum is desparate, lost hope and his life dreams are gone! )

Baada ya kupoteza Mkono!

Yasin amepoteza mkono wa kulia na baadhi ya vidole vya mkono wa kushoto
Yasin akielezea mkasa jitihada zake za kupata mkono bandia.

Yasin Ali(43) anasema anapata shida sana katika jitihada zake za kupata mkono wa bandia baada ya kupoteza mkono wake katika ajali iliyotokea mwaka 2003. Anasema kwamba, ajali ilimwacha akiwa hana mkono wa kulia na baadhi ya vidole vya mkono wa kushoto pia vilikatika.
Anasema amejitahidi sana kupata mkono bandia lakini jitihada zake zimegonga mwamba kwa sababu gharama ndio kikwazo kikubwa. mkono huo unauzwa Sh. 1,600,000 kufuatana na profoma invoive aliyokuwa nayo kutoka KCMC Moshi.
Yasin ameanza jitihada za kuwatafuta wasamaria wema ili waweze kumchangia aweze kutapata mkono huo. Kama umeguswa na utahitaji kumsaidia Yasin, tafadhali wasiliana nami nitakupa mwongozo wa jinsi ya kumpata.
(Yasin Ali,43, lost his right arm and some few fingers of  his right arm following motors traffic accident in 2003. To date he is stuggling to raise Tanzanian shilling 1.6million which is about 1500 US dollars for an artificial arm,but in vain)

Saturday, March 7, 2009

WAATHIRIKA WA AJALI WASIKATE TAMAA!




Waathirika wa ajali mbalimbali ambao wamepoteza viungo vyao, huhitaji vifaa kama hivi vya viungo bandia ili angalau kuwasaidia kufanya shughuli zao za kila siku kama walivyokuwa kabla ya kuathirika kwa ajali. Vifaa kama hivi hupatikana Taasisi ya Tiba ya Magonjwa ya Mifupa na Ajali(MOI) Mkoa wa Dar es salaam, hospitali ya KCMC Kilimanjaro na CCBRT mkoani Dar es salaam.
Viungo vya bandia huwasaidia waathirika wa ajali ambao wamepoteza viungo waweze kujisikia kama hawajapoteza kitu kwani huwasaidia kurudia maisha ya kawaida kwa kufanya shughuli zao mbalimbali. lakini wamekumbwa na matatizo kadhaa katika jitihada za kupata vifaa hivyo. Kwanza, waathirika wa ajali wapo nchi nzima, lakini Taasisi ambazo zinatengeneza vifaa hivyo kwa kiwango ni kama zilivyotajwa juu kwa hiyo mwathirika kutoka Lindi , Songea nk anahitajika kusafiri kutoka huko kwenda kuja Dar ili aweze kupata kifaa hicho ambapo wengi wao kupata nauli tu ni mtihani.Pili, gharama za vifaa ni kubwa kwa mwananchi wa kawaida. Kwa mfano, mguu uliokatwa chini ya goti ni shilingi 250,000 na juu ya goti si chini ya shilingi 500,000 za kitanzania.Kwa wananchi wengi hicho kiwango ni kikubwa sana. Kwa mfano nimeshuhudia msichana wa miaka 20 akitafuta mguu bandia kwa miaka2 bila mafanikio. Wengine hata magongo ya kutembelea(crutches) kabla ya kupata mguu bandia tayari ni tatizo na wameishia kutembea kwa kutumia vipande vya miti!
Idara ya ustawi wa jamii imeshindwa kuwasaidia kutokana na ukata, na mara nyingi wanapoenda huko huambiwa waache maelezo yao(particulars) halafu fedha ikipatikana watapewa taarifa! kwa hili hata mtoto mdogo atajua anadanganywa. Kwa maana nyingine ni kwamba kama anatoka Songea arudi huko halafu "Afisa" huyo atamtafuta!
KWA LEO NAOMBA WATANZANIA WENZANGU KAMA UNAJUA MAHALI AMBAPO TUNAWEZA KUWAELEKEZA HAWA WENZETU WAKAPATA MSAADA TAFADHALI WASILIANA NAMI, AU HATA KAMA WEWE UNAWEZA KUSAIDIA SI VIBAYA. CHONDE CHONDE TUWASAIDIE WATANZANIA WENZETU WANAOTAABIKA! NAWASILISHA!
blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker