
Mr. Bobos Class, ni blog inayotoa taarifa mbalimbali za ajali na athari zake.Itangalia ajali zote lakini zaidi zile za barabarani.Mbali ya kutoa taarifa pia inatoa elimu jinsi ya kuzuia ajali na ushauri nasaha kwa waathirika,na jinsi wanavyoweza kupata msaada baada ya kupata athari.Pia Blog hii itaungana na wadau mbalimbali wanaohusika na masuala ya ajali kwa njia moja au nyingine, kuelimisha na kutoa ushauri.Blog inatumia Kiswahili na Kiingereza.
Showing posts with label Daladala. Show all posts
Showing posts with label Daladala. Show all posts
Sunday, June 21, 2009
Inafurahisha!
Inafurahisha kuona kwamba konda wa daladala anajaza watu katika daladala lakini kwa kujua hilo yeye haweki kichwa chake ndani kwa kuwa anajua kwamba upumuaji ndani ya gari kama inavyoonekana pichani, ni shughuli pevu! Ni lini tutakuwa kama wenzetu wa Uganda ambao hawaruhusu kabisa abiria kujazana katika dalada?Monday, June 8, 2009
Daladala Everywhere Are The Same!
I saw this on the blog, Faustine's Baraza and it occured to me that we could share the experiences with others everywhere! I know of the daladala in Tanzania, the "Matatu" in Kenya and now the "Taxi" in South Africa all these are commuter buses with different names but its seems the drivers and the conductors have got the same characters. Can you share with us your experiences wherever you are? Be it in Egypt, Malaysia, you name it!
The message on this commuter bus reads "Don't be too close, this taxi stops anytime anywhere".
Interesting!Source: Faustine's Baraza
Saturday, April 18, 2009
Kutoka MOI Leo!


Kondakta wa daladala anayejulikana kwa jina la Juma Maduma(28) mkazi wa Kitunda, amepokelewa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Magonjwa ya Ajali Muhimbili(MOI) akiwa na maumivu makali ya kiuno baada ya daladala analofanyia kazi kugongwa na jingine kwa nyuma hali iliyopekelekea yeye kushtuka kiuno. Pichani Juma anaonekana akiwa na maumivu makali.
Afisa Uhusiano wa MOI, Jumaa Almasi amethibitisha kumpokea mgonjwa huyo.
Thursday, April 9, 2009
Daladala ni 'Headache' Jamani!
Katika pitapita mitaani, nilikutana na daladala hii ambayo dereva wake pamoja na wanaomsukuma walifanya kitu cha ajabu sana kwani walisukuma daladala hili na kukatisha barabara bila kujali watumiaji wengine wa barabara! Bajaj inayoonekana pembeni kama isingekuwa na breki nzuri basi tungeshuhudia ajali ya kutisha.
Nafikiri kuna haja ya askari wanaopiga patrol kuzungukia hata njia ambazo zipo mbali au nje ya barabara kuu! Hii ilikuwa njia ya Mabibo jirani kabisa na geti la Chuo cha Usafirishaji!
Friday, April 3, 2009
Kutoka MOI Leo!

Kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ajali Muhimbili(MOI) ni taarifa ya kusikitisha ya kijana Athumani Steven Mwakipesile(28) ambaye amelazwa katika Taasisi hiyo kufuatia ajali aliyopata baada ya kusukumwa na kondakta wa daladala inayofanya safari zake kati ya Mbezi na kariakoo. Kulingana na maelezo ya kijana huyo, ni kwamba alitoa noti ya Sh. 10,000 ili konda akate Sh. 250 ya nauli yake. Alipofika Magomeni na kuomba chenji,'konda' alikataa kumpa na kumsukuma nje ya gari ndipo akadondoka chini ya gari na tairi za gari hiyo zikamptia sehemu za kifuani na kumkanyaga mguu wa kushoto.
Hivyo athumani amevunjika mbavu na mguu (fracture of left femur) na kupata maumivu yaliyopelekea afanyiwe upasuaji wa dharura .
Anachoweza kukumbuka ni kwamba gari ilikuwa DCM yenye namba T 738....hakuweza kukumbuka namba zote, lakini anasema taarifa zipo polisi na wanaendelea kuitafuta hiyo gari.
Yes!imekuwa ni kitu cha kawaida kwa makondakta kuwanyanyasa abiria, ni lazima SUMATRA na vyombo vingine vifanye kazi ya ziada kudhibiti hali hii. Kijana Athumani angeweza kupoteza maisha kirahisi tu!
Subscribe to:
Posts (Atom)
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.