Showing posts with label hit and run. Show all posts
Showing posts with label hit and run. Show all posts

Friday, October 2, 2009

Wanafunzi Walala Barabrani Baada ya Mwenzao Kugongwa!

Habari nilizozipata hivi punde zinasema kwamba, leo jioni majira ya saa kumi jioni mwanafunzi mmoja wa shule ya sekondari aligongwa na gari maeeo ya Mbezi kwa musuguri. Mashuhuda wanasema aligongwa na gari aina ya Toyota Landcruiser ambalo lilikuwa katika mwendo wa kasi. Inasemekana baada ya ajali hiyo, dereva wa gari hilo hakusimama alitokomea.
Kufuatia tukio hilo wanafunzi wanaosoma na mwanafunzi huyo,waliamua kulala katikati ya barabara jambo ambalo lilisababisha foleni kutoka Mbezi kwa Musuguri hadi ubungo na kupelekea askari kuelekea eneo hilo na kufyatua mabomu ya kutoa machozi.

Friday, May 15, 2009

Mtaalam wa 'Nusu-Kaputi' Muhimbili Agongwa na Kufa!

Bakari Atilio mkazi wa Mabibo na mfanyakazi wa kitengo cha nusu kaputi cha hospitali ya Taifa Muhimbili, amefariki baada ya kugongwa na gari. Mkasa wenyewe ulikuwa kama hivi:

Mashuhuda wamesema kwamba Bakari alikuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T 438 ARN maeneo ya mabibo aligongwa na gari ndogo 'taxi' kwa nyuma. aliamua kushuka katika gari lake ili kuangalia uharibifu uliotokana na kugongwa. Mashuhuda wanasema, dereva wa taxi hiyo alirudi nyuma na kukanyaga mafuta hivyo alimgonga na kumburuza hadi chini ya gari.
Kufuatana na ajali hiyo, alivunjika mguu wa kulia(ankle joint), mfupa mkubwa wa paja(femur),mfupa wa shingo(cervical),mbavu na majeraha ya ndani ya mwili(visceral injury).Pamoja na jitihada kubwa za madaktari wa MOI, Bakari alipoteza maisha.Pichani Bw. Bakari akipatiwa matibabu ya dharura.
Ni kitendo cha kusikitisha sana na cha kikatili kilichafanywa na dereva huyo. Tunamwomba Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amin.

Tuesday, April 7, 2009

Kutoka MOI Leo! The 'Hit and Run' Victim Laid to Rest!




As you might remember, I posted a story of Anna Rogers Mpemba(24) seen in the photo, a victim of 'Hit and Run' accident who died after the accident and no relatives were seen.
Through efforts of various individuals,we managed to get someone whose wife hails from the same village,and through her we managed to get Anna's relatives. She was laid to rest last Saturday at Tekwa, her home village.
I thank all the individuals touched by the story and did all they could to make sure that Anna is burried decently.May almight God rest her Soul in Eternal Peace, Amen.
Meanwhile, the other victim of 'Hit and Run' accident is still in the Intensive care Unit (ICU)of the Muhimbili Orthopaedic Institute(MOI). This is according to MOI's Principal Public Relations Officer, Mr. Jumaa Almasi.
Tunashukuru kwa wale wote waliofanikisha kupatikana kwa ndugu wa marehemu Anna Rogers(24) na hatimaye kuzikwa kijijini kwao Tekwa huko Bumbuli wilayani Lushoto. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amin. (Also read; http://ajali-traumaclass.blogspot.com/2009/04/kutoka-moi-leo-hit-and-run-victim.html).

Thursday, April 2, 2009

Kutoka MOI Leo! Another 'Hit and Run' Victim!




Upon arrival at the Muhimbili Orthopaedic Institute(MOI) she was identified as "unknown Female Patient", after 3 days relatives appeared and her true identity was known. She is called Zena Ally Mng'agi born in 1970, a resident of Mtawanya-Bungu near Kibiti Secondary School. She was knocked by fast moving car at Mtoni kwa Azizi Ally area, but the car never stopped. She is in MOI's Intensive Care Unit (ICU).




Yes! Kumekuwa na ongezeko la watu kugongwa na madereva kukimbia!Dereva ambaye angeokoa maisha ya majeruhi kwa kusaidia kumpeleka hospitali ndio huyo anakimbia na kutokomea kaimuacha majeruhi anatapatapa. Nafikiri kuna haja ya madereva kuelimishwa juu ya hili japo kuna mazingira mengine dereva akisimama maisha yake yanaweza kuwa hatarini.


Je, dereva anapomuona mgonjwa akiwa chumba cha wagonjwa mahututi kama inavyoonekana pichani, anajisikiaje?Au ndiyo akishakimbia hajali hata kama aliyemgonga amepoteza maisha?Nafikiri Tubadilike!

Wednesday, April 1, 2009

Kutoka MOI Leo! The 'Hit and Run' Victim!




In the picture is the girl who was knocked by a fast moving car at Tegeta last saturday. The car never stopped. After the accident she was sent to Muhimbili Orthopaedic Institute(MOI) while unconcious and 'unknown'. She lasted in the Intensive Care Unit for some few hours and passed away.
Fortunately, someone noticed her 'voter registration card' at the scene of the accident and took it to MOI.
Through the card, herbears the name, Anna Rogers Mpemba,born in 1985, at Tekwa Village , Funta ward, (Bumbuli)Lushoto District in Tanga Region. Her registration center is Kwengeza Primary School.
According to MOI Principal Public Relations Officer, Mr. Jumaa Almasi, the body is till in the mortuary and NO RELATIVES so far.
Please inform whoever you think comes from Bumbuli areas before the body is buried by the City Council next Sunday.

Jamani tufanye hisani, kama unamfahamu yeyote anayetoka maeneo ya Bumbuli huko Lushoto mpe taarifa ili ajaribu kufanya mawasiliano na huko kabla huyu marehemu hajahifadhiwa na 'City'.
blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker