Thursday, May 14, 2009

Ubovu wa Barabara Wakwamisha Msafara wa Waziri Mkuu Mara Tatu Rukwa!

MSAFARA wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ulichelewa kwa zaidi ya saa tatu kufika kwenye kijiji cha Muze katika bonde la Rukwa kwa sababu ya kukwama njiani mara tatu kutokana na utelezi.
Tukio lilitokea juzi asubuhi wakati akitoka Sumbawanga mjini kwenda kijijini hapo kukagua Chama cha Akiba na Mikopo (SACCO) cha Muze na kuzungumza na wananchi akiwa njiani kwenda Mamba, wilayani Mpanda kwa ziara ya siku mbili jimboni kwake.
Katika hali ya kawaida, safari ya kuteremka bonde la Rukwa ingechukua saa moja au pungufu ya hapo. Baadhi ya magari yaliyonasa katika utelezi huo ni gari la RPC, gari la walinzi na la Wasaidizi wa Waziri Mkuu.
Utelezi huo ulitokana na mvua zilizonyesha usiku wa kuamkia jana huku barabara aliyopita ya Ntendo hadi Muze ikiwa imemwagiwa kifusi ambacho kilikuwa kimeanza kusambazwa lakini hakijashindiliwa. Barabara hiyo ina urefu wa kilometa 37, lakini sehemu korofi ilikuwa na umbali wa kilometa 15.
Meneja wa TANROADS wa mkoa wa Rukwa, Mhandisi Joseph Nyamhanga alisema barabara hiyo ilikuwa inafanyiwa ukarabati wa awali, ili iweze kufikia kiwango cha barabara zilizo chini ya mradi wa kuzikarabati barabara ili zipitike muda wote ambao ni wa miaka mitano (Source: Mwananchi).

Stranded Driver in the Middle of the the Road!

Hii ilitokea jana usiku katika makutano ya Sam Nujoma Road na barabara itokay Chuo Kikuu Mlimani. Eneo hili lina taa za kuongozea magari, lakini kutokana na msongamano wa magari huwa inatokea kwamba kila mtu anajiona ana haki ya kupita hata kama taa nyekundu inawaka.
Anayeonekana pichani ni dereva ambaye alichoshwa na uhuni uliokuwa unafanyika, akaamua kuacha gari yake na kuanza kuongoza magari.Je lini madereva bongo watastaarabika?

Kubeba Watoto Katika Baiskeli!


Mara nyingi nimekutana na waendesha baiskeli wakiwa wamewabeba watoto katika kiti cha nyuma cha baiskeli. Leo asubuhi saa 12.30 nimemuona huyu bwana katika picha(bofya picha) akiwa amembeba mtoto(angalia mshale) ambaye alikuwa anaonekana aidha amechoka au ana usingizi wa kuamshwa asubuhi sana kuwahi shule.Ninachoona mimi, huyu mtoto mikono yake haina nguvu kama ya mtu mzima, njia anayopita ni ina mashimo mashimo na inarusha kiasi kwamba huyu mtoto anaweza kuachia na kudondoka. Naomba tunapoona hilo tukemee ili kunusuru maisha ya watoto kama huyu.


DART Blah! Blah!
Ahmedabad : A five-member team from Tanzania will get a first-hand look at the ongoing Bus Rapid Transit System (BRTS) project in the city. The team is on a study tour in preparation for launching Dar Rapid Transit (DART), a similar system in East Africa.
The DART team has already taken a look at successfully running BRTS projects in Bogota and Curitiba. DART is the government authority of Dar es Salaam in Tanzania that will oversee the bus system for the city having around 3.5 million residents.
The delegation will be headed by regional commissioner of Dar es Salaam William Lukuvi. The team includes Permanent Secretary, Ministry of Infrastructure and Development, Omar Chambo and DART Chief Executive Cosmas Takule, Director of Systems and Operations Enoch Kitandu and Director of Transport Asteria Mlambo.
Says Municipal Commissioner IP Gautam, "We receive one or two requests from different state governments in the country and abroad to see our BRTS project."A robust urban transport system has gained in importance for proper development and management of traffic in cities across the globe, he adds. BRTS system ensures dedicated bus corridors, physically segregated lanes, pre-paid ticketing system and level boarding, among other facilities.
(Source: Times of India as seen on Faustine's Baraza blog).

Wednesday, May 13, 2009

Mapambazuko!

Hii ni mandhari ya jiji la Dar es salaam kunapopambazuka. Inavutia sio?Sisi wenye nafasi ya kuona haya mapambazuko si kwa kupenda, bali ni katika harakati za kukimbia msongamano wa magari unaowakwaza wakazi wa jiji hili.
Nafikiri modernization of Dar Roads utatukomboa. Au wadau wa kule Kimara, Mbezi, Kibamba, Tegeta, Segerea, Ukonga Mnasemaje?
(Sunrise in the city of Dar es salaam)

Ajali Mbaya Kibaha Kwa Matias!


Kuna taarifa kwamba ajali mbaya imetokea maeneo ya Kibaha kwa Mathias, inasemekana watu wawili wamefariki papo hapo na mmoja amefariki akiwa njiani kuelekea taasisi ya tiba ya Mifupa Muhimbili(MOI).Ajali hiyo imetokea baada lori(fuso) la mchanga kugonga pikipiki na hatimaye kwenda kugonga gari la abiria aina ya 'hiace' lililokuwa na abiria.
Waliofikishwa MOI ni Venosa Liseki(32) ambaye ameumia kichwa na kuvunjika mguu wa kulia na mwingine ni mwanaume ambaye jina halikuweza kupatikana kwa kuwa amepoteza fahamu.
Pichani kulia ni majeruhi Venosa Liseki na kushoto ni majeruhi ambaye hajatambulika.

Miundo Mbinu Duni!



Gari la mizigo likiwa limezama katika matope kufuatana na mvua zinazoendelea kunyesha katika sehemu mbalimbali za nchi (Source:Mwananchi)
blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker