ABIRIA 380 wa treni ya Express waliokuwa wakitokea Kigoma kuelekea Dar es salaam wamenusurika kufa baada ya kupata ajali mkoani Tabora.
Ajali hiyo ilitokea usiku wa manane wa kuamkia juzi baada ya kichwa cha treni na mabehewa mawili kuanguka kati ya stesheni za malongwe na Tura mkoani Tabora.
Hata hivyo hakuna abiria aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa na abiria wote walilazimika kurejeshwa mjini Tabora mapema baada ya ajali na kuondoka siku iliyofuatia.
Baadhi ya abiria wamelaumu kwamba tangu mwanzo wa safari ilionekana kwamba kichwa cha treni hiyo kilikuwa na matatizo lakini hakuna aliyeonyesha kujali. Pia abiria hao walilaumu kwamba wametelekezwa, wanalala na kushinda njaa pamoja na watoto wadogo.
Wengine wamesema ni wagonjwa na hawana msaada wowote wa dawa.
Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Reli (TRL) imeunda tume ya kuchunguza ajali hiyo.
No comments:
Post a Comment