Showing posts with label No number plate. Show all posts
Showing posts with label No number plate. Show all posts

Monday, April 27, 2009

Jingine Tena..........No numbers!

Hapa linaonekana likiweka mafuta bila wasiwasi

Hapa linaanza kukata mitaa kwa nafasi!

Huu ni muendelezo wa ufuatiliaji wa haya magari ya takataka ambayo yanaonekana kukatiza mitaa ya jiji bila hata namba za usajili. Sijui wahusika wanayaona au vipi. Nimekuwa nikifuatilia na nitaendelea kufuatilia mpaka hapo wahusika watakapoona umuhimu wa kuyafuatilia.






Friday, April 17, 2009

Hii Tena.........! No number Plate! Pt. 3

Kama zilivyo post zangu zilizopita kuhusu magari ya takataka, leo tena nimekutana hili likiwa limepaki eneo la majeneza pale njia ya kuelekea muhimbili. Mbali na makosa mengine kama vile kuegesha eneo ambalo haliruhusiwi, hili la kukosa namba ni kosa kubwa sana! Bado najiuliza kama wanapopita barabara kubwa askari wa usalama barabarani hawaoni?


Thursday, April 16, 2009

Hii Tena imezidi! No number Plate! Pt. 2

Gari la kubeba takataka (juu katikati) linaonekana likipita bila namba ya usajili .




Bado tunaendelea kuyatupia macho magari ya kubebea takataka. Mara ya mwisho tuliona kwamba mengi yana mapungufu na mengine hayana namba usajili kabisa, lakini yanatembea barabarani na mengi yamekuwa kero kwa watumiaji wengine wa barabara. Cha kusikitisha ni kwamba, yanapita katika barabara zetu na vyombo vya usalama vinayaona na kuyafumbia macho. Yakishaleta madhara ndio tutaona kila mmoja anazinduka usingizini na kuanza kuyafuatilia. kwanini yasifuatiliwe sasa?

Magari ya takataka ambayo hayana namba za usaji kama hilo hapo juu pichani,yanaendelea kudunda katika mitaa ya jiji la Dar. Je, nani wa kumuuliza kuhusu hilo?
blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker