Sunday, October 11, 2009

Marufuku Askari Kuwapoka Madereva Leseni

Polisi mkoani Arusha imepiga marufuku tabia ya baadhi ya askari wa kikosi cha Usalama Barabarani, kuwapokonya funguo na kadi za magari, madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani.
Msimamo huo ulitolewa hivi karibuni na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Matei Basilio, alipokuwa akizungumza katika sherehe za kufunga Wiki ya Nenda Kwa Usalama.
Alisema kumekuwepo na malalamiko juu ya baadhi ya askari wa kikosi hicho kuwapokonya madereva funguo na vitu vingine kutoka kwenye magari, jambo ambalo ni kosa.
"...Kama dereva amefanya makosa afikishwe polisi au alipe faini na kama itakuwa lazima basi afikishwe katika ngazi za juu badala ya kumpokonya leseni au kitu kingine", alisema Basilio.
Source: Mwananchi
Mtazamo wangu: Nashukuru Kamanda Basilio ameliongelea hili kwa sababu inakera sana kuona askari wa usalama barabarani anamnyang'anya dereva wa daladala ufunguo huku akiwa amebeba abiria. Kwanini asimwambie dereva akashushe abiria halafu aipeleke gari kituo husika? Hii inaonyesha ni jinsi gani watanzania tusivyojaliana. Tamko la Kamanda Basilio linastahili pongezi.

No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker