Friday, October 2, 2009

Wanafunzi Walala Barabrani Baada ya Mwenzao Kugongwa!

Habari nilizozipata hivi punde zinasema kwamba, leo jioni majira ya saa kumi jioni mwanafunzi mmoja wa shule ya sekondari aligongwa na gari maeeo ya Mbezi kwa musuguri. Mashuhuda wanasema aligongwa na gari aina ya Toyota Landcruiser ambalo lilikuwa katika mwendo wa kasi. Inasemekana baada ya ajali hiyo, dereva wa gari hilo hakusimama alitokomea.
Kufuatia tukio hilo wanafunzi wanaosoma na mwanafunzi huyo,waliamua kulala katikati ya barabara jambo ambalo lilisababisha foleni kutoka Mbezi kwa Musuguri hadi ubungo na kupelekea askari kuelekea eneo hilo na kufyatua mabomu ya kutoa machozi.

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker