
(Jamani, niliona kitu cha kushangaza kidogo nikaona nishee nanyi. Nikiwa Morogoro road karibu na shule ya jangwani, abiria wa pick alitupa chupa ya maji barabarani baada ya kumaliza kunywa maji. ghafla dereva wa gari mark II iliyopo mbele yangu alitoka katika gari,akaokota hiyo chupa na kumrudishia jamaa aliyeitupa kwamba anachafua mazingira. Ni kitu kigeni kwa Tanzania. Lakini ni mfano wa kuigwa kuona tuna watu wanajali mazingira kiasi hicho. Pichani inaonekana hiyo Mark II yenye namba T297ACS na pickup inaonekana kulia kwake mbele kidogo.
No comments:
Post a Comment