Sunday, October 11, 2009

Hili La Matuta Kimara Limewakera Wengi!

Nimekutana na hii barua ya msomaji katika gazeti la Mwananchi inayogusia uwekaji wa matuta katika barabara mbalimbali za jiji la Dar es salaam.
"Mimi kama mmoja wa waathirika wa mkasa wa kukwama katika Barabara ya Morogoro,kutokana na ujenzi wa matuta Kimara, Dar es salaam.
Niikerwa na mfumo wa maofisa wanaohusika, wakiwemo polisi na wakala wa Barabara Tanzania(Tanroads), kuruhusu ujenzi huo kufanyika wakati ambao wazungu wanauita 'pick-hour' yaani ule ambao unakuwa na msongamano mkubwa wa magari na kuacha siku kama za jumapili na kuiga nchi zilizoendelea kama Uingereza,ambazo hufanya ujenzi kama huo usiku wa manane wakati hakuna magari mengi.
Hii inaonyesha jinsi tusivyojali wengine, mkandarasi husika alijali fedha na kuwaweka vibarua kufanya kazi hiyo mchana bila kufikiria usumbufu aliousababisha. Hii ni mara ya pili kufanyika hivyo na usumbufu huwa wa kiasi hicho lakini wahusika wanafumbia macho".
Barua imeandikwa katika gazeti la Mwananchi na mbogojj@yahoo.co.uk
Mtazamo wangu: Nikiwa mmoja wa waathirika wa usumbufu uliotokea siku hiyo, namuunga mkono mwandishi wa barua hii, kwakweli Tanroads walistahili kutuomba radhi kwa usumbufu wa siku ile. Tulikaa masaa manne barabarani mpaka askari wa usalama barabarani walipoingilia kati na kusimamisha ujenzi huo.

1 comment:

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker