Saturday, January 17, 2009

AFRIKA INAONGOZA KWA AJALI?

Ni hali ya kusikitisha kuona kwamba idadi ya watu wanaopoteza maisha kutokana na ajali Afrika, inazidi kuongezeka siku hadi siku. Hali ambayo imelishtua hata Shirika la Afya Duniani (WHO). Maneno yafuatayo hapa chini ni ushahidi tosha wa haya ninayosema kulingana na utafiti uliofanywa na BBC mwaka jana na kufuatiliwa na wadau mbalimbali ndani na nje ya Afrika.
Inasema kwamba:
‘’Trauma rates in Africa are among the highest in the world. According to the World Health Organization, each year there are more than 200 000 road traffic deaths in Africa and perhaps 20 to 30 times as many people seriously injured. And trauma in Africa is definitely getting hotter, with injury rates predicted to increase by around 80% by 2020’’.

Hizi si takwimu za kufurahia, ni takwimu ambazo zinaonyesha kama hatua za kudhibiti hali hii hazitachukuliwa, hali itaendelea kuwa mbaya na watu wengi watapoteza maisha kutokana na ajali. Watu 200,000 kupoteza maisha sio kitu kidogo au cha kuangalia tu na kuacha kiendelee kuchukua maisha ya watanzania.
Swali lakujiuliza ni kwamba, “Je, katika hiyo idadi ya vifo 200,000 vya ajali ni vingapi vimetokea Tanzania?” kwa jinsi idadi ya ajali inavyoongezeka, ni dhahiri kwamba mchango watanzania katika idadi hiyo ni mkubwa sana kuliko mtarajio ya wengi. Katika wiki hii, ajali ya Basi la Tashrif iliyotokea Mji wa Hale Mkoani Tanga, imechukua maisha ya watanzania wasiopungua 28 na wengine 24 walijeruhiwa vibaya. Na tangu mwaka huu wa 2009 uanze idadi ya watanzania waliopoteza maisha katika ajali mbalimbali ni zaidi ya 70? Je, tunaridhika na hali hii na kukaa kimya?
Profesa Ian Robertson (Professor of Epidemiology and Population Health) anasema kwamba:
‘’One pointed out that doctors needed to do 30 trauma laparotomies to make the grade in trauma surgery. This can take three years in the north but only three months in Johannesburg’’.
Kwamba kwa daktari kutoka uingereza anatakiwa kufanya operesheni za tumbo (Laparatomy) kwa majeruhi wa ajali 30 kwa wagonjwa wa ajali, na akiwa Uingereza au nchi yoyote ya Ulaya itachukua miaka mitatu kupata idadi hiyo ya wagonjwa. Lakini kwa mshangao, ukiwa Afrika katika jiji la Johannesburg unapata idadi hiyo ndani ya miezi mitatu. Na Ninathubutu kusema Tanzania idadi kama hiyo itapatikana ndani ya miezi miwili kulingana na takwimu za ajali zinavyokwenda kwa sasa hivi.
Wadau wote katika fani ya masuala ya ajali, tunatakiwa kufunga mikanda ili kudhibiti hali hii inayoonekana kutishia maisha ya watanzania wengi.
Binafsi ninapongeza hatua zilizochukuliwa na SUMATRA (Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini) kwa kuyafungia kutoa huduma mabsi ya makapuni ya Sumry, Air Buffalo,na Zuberi kutokana na kutokidhi viwango vya biashara ya usafirishaji Abiria na kuhatarisha usalama wa maisha na mali zao.
Kwa kufanya hivyo nina imani kwamba, si tu maisha ya watanzania yataokolewa bali pia uharibifu wa mali zao na miundo mbinu utadhibitiwa kwa kiwango kikubwa. Aluta Continua!

No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker