Wednesday, January 14, 2009

HUDUMA YA KWANZA INAOKOA MAISHA

Huduma ya kwanza ni huduma inayotolewa kwa jili ya ugonjwa au majeraha. Kwa kawaida hutolewa na na mtu yeyote ambaye hajasomea tiba mpaka msaada wa kitalaam unapofika.Baadhi ya magonjwa yanaweza yasihitaji msaada zaidi wa matibabu baada ya kupata msaada wa huduma ya kwanza. Kwa kawaida huduma ya kwanza huwa ni hatua rahisi ambazo mtu anaweza kufunzwa na kutumia vifaa rahisi.
Huduma ya kwanza inaweza kutolewa kwa wanyama waliojeruhiwa pia, lakini inahusisha zaidi binadamu.
Swali tunalopaswa kuulizana ni kwamba, je ni maisha ya watanzania wangapi ambayo yamepotea kwa kuwa watanzania wengi hawajui kutoa huduma ya wkwanz? Ni mara ngapi tumeonea watu wakiwasaidia majeruhi wa ajali mbalimbali lakini katika kufanya hivyo wakiwazishia maumivu zaidi au hata kusababisha vifo vyao? Inasikitisha.
Taarifa hii inafuatilia uchunguzi uliofanywa na wadau wa ‘‘Mr. Bobos Class’’ na kugundua kwamba, watanzania wengi hawajui kutoa huduma ya kwanza hasa hasa kizazi kipya ambacho kimekumbana na mapungufu ya taaluma hiyo mashuleni.
Kwa waliosoma miaka ya nyuma wamebainisha kwamba wao walijifunza hudma ya kwanza kwa njia mbili; kwanza, walifundishwa mashuleni kama sehemu ya masomo yao, pili, wale waliokuwa maskauti walijifunza katika mafunzo ya uskauti.
Ni dhahiri kwamba watanzania wengi wamepoteza maisha yao katika ajali mbalimbali kwa kuwa wale waliokuwa karibu yao walishindwa kuwapa huduma ya kwanza.
Hivyo mjadala unafunguliwa wadau wote wanaombwa kuchangia nini kifanyike ili kuhakikisha kwamba watanzania kwa ujumla wao wanajua kutoa huduma ya kwanza.

No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker