Saturday, January 17, 2009

KAMPUNI YA BIA(TBL) YACHANGIA ELIMU

Ikiwa ni jitihada za watu binafsi na makampuni kuiunga mkono serikali katika vita vyake dhidi ya ajali nchini, Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) ilichangia kiasi cha shilingi Milioni 2.2 kusaidia kuchapisha vipeperushi vya kuelimisha jamii na madereva kuhusu sheria na kanuni za usalama barabarani.
Mr. Bobos Class Team tunaipongeza kampuni hiyo, kwani mchango wake ukitumika vema utaokoa maisha ya watu na mali zao kwa kuwakinga na ajali mbalimbali.
Msaada huo uliwakilishwa kwa Mrakibu Msaidizi wa Polisi(ASP) Joseph Mwakabonga na Bwana Maneno Mbegu ambaye ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL).

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker