Monday, January 12, 2009

MOI YALAZA 5, NA MMOJA AFARIKI

Taarifa tulizozipata leo wakati tukisherehekea sikukuu ya Mapinduzi ya zanzibar ni kwamba, Taasisi yaTiba ya Mifupa MOI imepokea wagonjwa wa ajali mbalimbali wapatao watano. Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa uhusiano Mwandamizi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) Bw. Jumaa almasi.
Majina ya waliopata ajali ni kama ifuatavyo;Sudi Magenge ambaye ana umri wa miaka 40, alipokelewa MOI akitokea Mkuranga baada ya kupata ajali na kuumia kichwa na kuvunjika mkono wa kushoto. Mwingine ni Abdallah Mohamed Abdallah mwenye umri 23,ambaye alipata majeraha ya kichwa. Pia Albert John aliyepokelewa kutoka hospitali ya Mwananyamala akiwa aamevunjika mfupa wa paja. Mwisho ni Abasi abdallah Juma mwenye miaka 26, alipokelewa MOI kutoka hospitali ya Amana akiwa amepata majeraha sehemu mbalimbali za mwili na kuvunjia mfupa wa mkono karibu na kiganja(Ulna),mfupa wa mguu chini ya goti(Tibia na Fibula), mfupa wa mguu sehemu ya paja(femur) na kuumia kichwa (Mild head injury).
Kwa mujibu wa Bw. Almasi, wagonjwa wote hao wanaendelea vema baada ya kupatiwa Tiba, lakini kwa bahati Mbaya Abdallah Mohamed Abdallah alifariki dunia pamoja na jitihada kubwa zilizofanywa na madaktari kuokoa maisha yake.
NI MASIKITIKO MAKUBWA KWA KIJANA MWENYE UMRI MDOGO KAMA HUYU ABDALLAH MOHAMED ABDALLAH(23) KUPOTEZA MAISHA WAKATI NDIO KWANZA ALIKUWA KATIKA UMRI WA KUANZA KUTEGEMEWA. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI NA MAJEERUHI WALIOBAKIA WAPATE AHUENI YA HARAKA. AMIN.
HAYA YOTE NI MADHARA YA AJALI.

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker