Wanaopata ajali hapa nchini ni wengi, na wengi wao hupata hata ulemavu na kusababisha maisha kuwa magumu sana kwao na wale wanaowategemea. ni wachache sana ambao wanajua ni hatua gani za kuchukua baada ya kupata ajali kama hizo-hasa ajali za gari. Kwa kiasi kikubwa wengi wa wale waliopata ajali walikuwa abiria katika vyombo mbalimbali vya usafiri hususan magari. na imebainika kwamba, mara nyingi ajali hizo hutokea kutokana na uzembe wa dereva, aidha anakwenda mwendokasi, anaendesha amelewa au hata kuendesha kwa kutozingatia madhara kwa abiria wake.
Japo ataadhibiwa kwa mujibu wa sheria za nchi, lakini je anajua ni watu wangapi amewaharibia maisha kutokana na uzembe wake?
Kwa hiyo blog hii pia ina lengo la kuwaonyesha hao madereva madhara waliyowaachia abiria na familia zao. Kwa mfano mtu aliyevunjika kiuno na kupooza kuanzia kiunoni hadi miguuni ni wazi kwamba hatoweza tena kufanya kazi za kujikimu yeye na familia yake. kwa maana hiyo familia nzima inakuwa imeathirika kwa ujumla.
hivyo blog hii itawaletea mifano halisi ya watu ambao wameathirika kutokana na ajali mbalimbali.
Mr. Bobos Class, ni blog inayotoa taarifa mbalimbali za ajali na athari zake.Itangalia ajali zote lakini zaidi zile za barabarani.Mbali ya kutoa taarifa pia inatoa elimu jinsi ya kuzuia ajali na ushauri nasaha kwa waathirika,na jinsi wanavyoweza kupata msaada baada ya kupata athari.Pia Blog hii itaungana na wadau mbalimbali wanaohusika na masuala ya ajali kwa njia moja au nyingine, kuelimisha na kutoa ushauri.Blog inatumia Kiswahili na Kiingereza.
Monday, January 12, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
No comments:
Post a Comment