Monday, July 27, 2009

Ajali Ya Mohamed Trans Yaua 30!

ZAIDI ya watu 30 wamefariki dunia baada ya basi walilokuwa wakisafiria la Mohammed Trans, kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam kupitia Nairobi nchini Kenya, kupata ajali wilayani Korogwe mkoani Tanga.
Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia gazeti la Mwananchi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Erasto Sima, zinasema chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa gurudumu moja la basi hilo na kugongana uso kwa uso na gari la mizigo aina ya Scania, lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Arusha.
Mpaka gazeti linakwenda mtamboni ni majeruhi 13, ndio waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Korogwe, Magunga, mkoani Tanga na katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo, iliwekwa taa ya kandili kutokana na kukosekana kwa umeme ili shughuli za kuweka miili ya marehemu hao ziendelee .
Habari zaidi zilisema ajali hiyo ilitokea katika eneo la Kwa Kombo wilayani Korogwe, majira ya saa moja jioni jana.
Sima alisema jitihada za kutoa maiti nyingine ambazo zinadaiwa kuwa zimekandamizwa na basi hilo, zilionekana kuwa ngumu kiasi cha kuagiza winchi kutoka mjini Tanga, lisaidie kuliinua basi hilo ili maiti zilizokandamizwa ziweze kupatikana.
Hata hivyo, mkuu huyo wa wilaya alisema hadi muda huo kulikuwa na maiti 27 zilizokwisha patikana, wanaume 21 na wanawake sita.
Wakati huohuo, mtu mmoja amefariki dunia katika ajali iliyotokea maeneo ya Wami mkoani Tanga baada ya gari la Kampuni ya Airbus lililokuwa likisafiri kwenda Dar es Salaam jana kugongana na lori.

Taken from: www.mwananchi.co.tz

No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker