Thursday, July 23, 2009

SUMATRA Yasihi Mradi wa DARTS Uharakishwe!

Msongamano wa magari barabara ya Morogoro, Dar es salaam


Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi kavu(Sumatra),imeutaka mradi wa mabasi yendayo kwa kasi(DART), uharakishwe ili kuondoa adha ya usafiri inayolikumba jiji la Dar es salaam.
Akizungumza na gazeti la Mwananchi kwa njia ya simu Afisa Uhusiano wa Sumatra, David Mziray alisema mradi huo unatakiwa ufanyike haraka kwani utasaidia kuondoa adha ya usafiri jijini Dar es salaam kwa kiasi kikubwa.
Mziray alisema hayo alipoulizwa juu ya maoni yake kufuatia taarifa zilizotolewa kwamba mradi huo una hatihati ya kutelekezwa mwaka huu na hata mwaka kesho kutokana na kukosekana kwa mkandarasi wa kujenga miundombinu ya barabara za zege.
Taarifa za Ofisa Mtendaji Mkuu wa DARTS, Cosmas Takule zilisema mradi huo ulipata mkopo wa dola za kimarekani milioni 190, kutoka Benki ya dunia kwa ajili ya kuanzisha mradi huo, lakini utekelezaji wake bado unasuasua jambo ambalo linatia hofu kuzuka kwa ubadhilifu baadaye.

No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker