Thursday, July 16, 2009

Apigwa Faini Kwa Kuendesha Gari Huku Akioga!

Dereva mmoja wa lori nchini China amepigwa faini baada ya kukamatwa akiwa kwenye usukani akiendesha gari huku akioga.
Polisi waliokuwa katika gari la patrol walishangazwa kuona maji yakitiririka barabarani kutoka kwenye lori lililokuwa mbele yao kwenye barabara kuu kwaajili ya magari yanayoenda kasi ya Jinyi."Tulihofia kuwa dereva atakuwa hajui kuwa gari lake lina matatizo na maji yanavuja kutoka kwenye gari lake, tulimuamuru aegeshe pembeni lori lake kwenye kituo cha mafuta cha karibu", alisema msemaji wa polisi.Polisi walipigwa na butwaa baada ya kumuona dereva wa lori hilo akiwa ametota maji mwili mzima akifurahia kupiga bafu akiwa kwenye usukani kwa kutumia maji yaliyokuwa yakitiririka kutoka kwenye bomba lililokuwa limewekwa juu ya kichwa chake.Mkewe aliyekuwa amekaa siti ya abiria pembeni yake alikuwa ameshikilia mfuko wa plastiki kuziba baadhi ya vifaa vya kwenye lori hilo visilowe.Walipokamatwa mkewe alimtetea mumewe kwa kusema kuwa walikuwa wanaharakisha kuipeleka mizigo iliyokuwemo kwenye lori hilo mji mwingine na mumewe aliamua kuoga kwenye lori hilo baada ya kiyoyozi cha kwenye lori hilo kuharibika.Polisi walimpiga faini dereva wa lori hilo hapo hapo na kumpa onyo kuwa akirudia tena kuoga huku anaenda gari basi atakuwa kwenye matatizo makubwa.

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker