Thursday, July 16, 2009

Maiti Zagawanyika Vipande Vipande Kwenye Ajali ya Ndege Iran!

Ndege ya shirika la ndege la Caspian Airlines la Iran imeanguka nchini humo na kuua jumla ya watu 168 waliokuwemo kwenye ndege hiyo na kusababisha vipande vidogo vidogo vya maiti kuzagaa katika shimo kubwa lililotokea eneo ambalo ndege hiyo iliangukia.
Ndege iliyotengenezwa nchini Urusi aina ya Tupolev ya shirika la ndege la Iran, Caspian Airlines iliyokuwa ikisafiri kutokea Iran kuelekea Armenia imeanguka baada ya kushika moto angani na kusababisha shimo kubwa sana kwenye shamba ilipodondokea na kuua jumla ya watu 168 waliokuwemo kwenye ndege hiyo.Ajali hiyo iliyotokea dakika 16 baada ya ndege hiyo kupaa kuanza safari yake, iliacha vipande vya mabaki ya ndege vikiwa vimezagaa kila kona huku miili ya watu wote waliokuwemo kwenye ndege hiyo ikiwa imekatika vipande vipande na kuteketea kwa moto.Ndege hiyo iliyodondoka majira ya saa nne asubuhi kwa saa za Tanzania, ilikuwa imebeba abiria 153 na wahudumu wa kwenye ndege 15."Niliona kidole cha abiria ardhini, kulikuwa hakuna dalili kama kulikuwa na ndege ni vipande vidogo vidogo vya vyuma vilivyokuwa vimezagaa kila kona" alisema shuhuda mmoja wa tukio hilo na kuongeza "Sikuona hata mguu au mkono uliokamilika, ni vipande vidogo vidogo vya miili ya watu vilivyokuwa vikionekana".Wachezaji wanane wa timu ya taifa ya judo ya Iran na makocha wawili walikuwa miongoni mwa waliofariki."Ndege ya shirika la ndege la Caspian Airlines imeanguka na imeteketea kabisa na kwa bahati mbaya maiti zote zimeungua na kuteketea kabisa" alisema Massoud Jafarinasab, kamanda wa polisi wa mji wa Qazvin ambako ndege hiyo imeanguka.Maafisa wa Iran walidai kuwa ndege hiyo ilikumbwa na matatizo ya kiufundi angani na ilikuwa ikijaribu kutua kwa dharura lakini kwa bahati mbaya ilishika moto angani na kulipuka."Ilikuwa ni ajali mbaya sana, mabaki ya ndege yakitapakaa kwenye eneo la mita 200" alisema afisa mmoja wa zimamoto."Kulikuwa na mlipuko mkubwa uliosababisha shimo kubwa lilokuwa na kina cha mita 10 ardhini. Kulikuwa hakuna kitu ambacho tungeweza kufanya kuokoa maisha, tulijaribu kuuzima moto uliokuwa ukiwaka kwa uwezo wetu wote" alisema afisa huyo.Sababu za kudondoka kwa ndege hiyo bado hazijajulikana.Iran imekuwa na rekodi mbaya ya ndege zake kuanguka ndani ya miongo michache iliyopita na ajali nyingi za ndege nchini humo huhusisha ndege zilizotengenezwa nchini Urusi.Vikwazo vya kiuchumi walivyowekewa Iran na Marekani vimesababisha Iran ishindwe kununua spea za ndege zao za zamani aina ya Boeing na Airbus na kusababisha wategemee zaidi ndege zinazotengenezwa nchini Urusi.
Source: http://www.nifahamishe.com/

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker