Sunday, June 7, 2009

Abiria 60 Watekwa Wavuliwa Nguo!

Abiria 60 waliokuwa wakisafiri kutoka kijiji cha Iyumbu Singida vijijini kwenda mjini Singida wamevamiwa na majambazi kwa kutekwa kisha kuvuliwa nguo zote kabla ya kuporwa fedha taslimu pamoja na simu za mkononi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Bi. Celina Kaluba alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 11.30 alfajiri katika eneo la kijiji cha Jerumani, Tarafa ya Sepuka Singida vijijini.
Bi Kaluba alisema tukio hilo lilihusisha basi la abiria lenye namba za usajili T 350 ARE mali ya Kampuni ya Sunset la Singida likiendeshwa na dereva Ahmed Hilal,35.
Source: www.majira.co.tz

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker