Monday, June 8, 2009

Wafanyakazi wa Reli Wagoma!

Wafanyakazi wa Kampuni ya Reli(TRL), walianza mgomo Ijumaa juni 5, baada ya uongozi wa shirika hilo kugoma kusaini mkataba wao wa hiari wenye kipengele cha kulipwa mkono kwaheri. Uamuzi huo umekuja baada ya Katibu mkuu wa Chama Cha Wafanyakazi wa Reli (TRAWU), Sylvester Rwegasira, kuwaeleza wafanyakazi hatua iliyofikiwa kuhusiana na suala hilo. Rwegasira aliwaeleza wafanyakazi hao kuwa TRAWU imepitia hatua mbalimbali zikiwamo kukutana na Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Juma Kapuya, hatua ambazo hadi sasa hazijazaa matunda.
Source: Tovuti:
www.newhabari.com/mtanzania

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker