Tuesday, June 2, 2009

Ajali Zaua Watu wawili Dar!

Watu wawili wamekufa na mmoja kujeruhiwa,katika ajali tofauti zilizotokea juzi usiku jijini Dar es salaam.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Faustine Ishengoma, alisema ajali ya kwanza ilitokea saa 5 usiku katika eneo la Vingunguti, Barabara Nyerere.
Alisema katika ajali hiyo, mwanamke anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30, alikufa kwa kugongwa na gari, ambayo hata hivyo namba zake za usajili hazuikuweza kufahamika.
Kamanda huyo alisema marehemu pia hajatambuliwa.
Alisema ajali nyingine ilitokea muda huohuo katika eneo la Kipawa na kusababisha kifo cha mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri na umri wa miaka 35.
Ishengoma alisema marehemu huyo naye bado hajatambulika na gari lililomgonga halikusimama. marehemu wote wawili wamehifadhiwa katika chumba cha maiti cha hospitali ya Amana.
Source:Mwananchi

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker