Tuesday, June 2, 2009

Basi Lateketea Kwa Moto!

Basi la abiri alililokuwa likitokea jijini Mwanza kuelekea Dar es salaam, limeungua moto na kuteketea.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Elias Kalinga aliwaambia waandishi wa habari kuwa, basi hilo lilipata ajali hiyo jana saa 1:00 asubuhi kwenye eneo la Hunghumalwa lililo kwenye barabara ya Mwanza-Shinyanga wilayani Kwimba.
Alisema siku ya tukio basi la abiria aina ya Scania likiwa na abiria 15 liliwaka moto na kuteketea.
Alisema gari hilo lilipata ajali wakati likiwa limesima kwa ajili ya kupakia abiria huko eneo la Hunghumalwa na ndipo moto ulipozuka kutoka kwenye injini na kuunguza gari.
Kalinga alisema kuwa abiria waliokuwa kwenye gari walifanikiwa kutoka wakiwa salama huku mizigo waliyokuwa nayo ikiteketea kwa moto.Kamanda wa Polisi alisema chanzo cha moto huo bado hakijajulikana (Habari zaidi soma Mwananchi. www.mwananchi.co.tz).

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker