Friday, June 12, 2009

Maiti 3 Zatambuliwa...Ni Ajali ya Hajees!

Miili ya watu watatu kati ya watu sita waliofariki katika ajali ya gari iliyotokea katika kijiji cha Mtumba kilometa 20 kutoka dodoma imetambulika.
Ajali hiyo ilitokea juzi eneo la mtumba manispaa ya dodoma ambapo watu 6 walipoteza maisha huku wengine 37 wakijeruhiwa wakiwamo 18 waliolazwa katika hospitali ya mkoa wa dodoma wakiendelea na amatibabu.
Mkuuwa upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa dododma Salum Msangi alisema maiti zilizohifadhiwa katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma zimetambuliwa kwa kuangalia vitambulisho vilivyokutwa katika mifuko ya marehemu hao.
Msangi aliwataja waliotambuliwa kuwa ni Dk. Shabani Kibwana wa Hospitali ya Mtakatifu Gasper iliyopo itigi wilayani Manyoni, askari wa jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ) kutoka makao Makuu dar es salaam mwenye namaba MT 69547 PTE Mohamed Salum na Jackson Alex.
Alisema jeshi la polisi linaendelea kumsaka dereva wa basi hilo aliyetoroka muda mfupi baada ya ajali na kwamba uchunguzi wa awaliunaonyesha kwamba dereva alikuwa kwenye mwendo kasi kutokana na basi hilo kuserere pembeni umbali war obo kilometa baada ya ajali hiyo kutokea.
Basi lililopata ajali ni la kampuni ya Hajees.
Source: www.mwananchi.co.tz

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker