Friday, June 26, 2009

Polisi Waruhusu Biashara Ya PikiPiki D'salaam!

Polisi katika kanda maalum ya Dar es salaam, imeruhusu kuendelea kwa biashara ya pikipiki kwa masharti ya pikipiki moja kutobeba zaidi ya abiria mmoja.
Hatua hiyo imekuja wakati watu wane wakiwa wamekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa ndani ya miezi miwili tangu biashara hiyo ilipoanza.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari na kusainiwa na kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Suleiman Kova, watu wane wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika na matukio matatu ya uhalifu yanayohusisha biashara hiyo.
“Jeshi la polisi haalijapiga marufuku biashara hiyo, ispokuwa wafanyabiashara wanatakiwa kupakia abiria mmoja mmoja katika pikipiki zao, kusajili pikipiki hizo na kufuata sheria zote za barabarani” ilisema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo pia ilisema , kama dereva wa pikipiki atabainika kuwa amekiuka sheria za barabarani, atakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Ilisema madereva wanapaswa kuwa na leseni daraja A na kuendelea.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo masharti mengine yanayotakiwa kufuatwa ni pikipiki hizo kuwa na namba ya usajili na kukaguliwa na askari wa usalama barabarani.

No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker