Sunday, June 28, 2009

Wizi Alama Za Barabarani Waikera TanRoads!

Wizi wa alama za barabarani mkoani Morogoro, umetajwa kuwa chanzo cha kuongezeka kwa ajali za magari, mkoani humu.
Hayo yalisemwa na Meneja wa Wakala wa Barabara(TanRoads) wa mkoa wa Morogoro, Charles Madinda, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu kukithiri kwa wizi wa alama hizo muhimu.
Alama hizo zimekuwa zikionyesha hali halisi ya maeneo mbalimbali ya barabara ili kuwawezesha watumiaji wa barabara, kuepuka ajali.
madinda alisema ingawa TanRoads imekuwa ikijitahidi kuweka alama hizo katika barabara mbalimbali za mkoa huu,lakini watu wasiojulikana wamekuwa wakiziiba.
alisema ahata hivyo wanaoiba alama hizo, hawazingatii kuwa hiyo ni hujuma inayoweza kusababisha ajali zinazochangia watu kupoteza maisha.
"Watu wanaiba alama hizo kwa tamaa kupata fedha na wala hawajali kuwa vitendo hivyo vinaathiri usalama wa barabara zetu na maisha ya watu kwa jumla" alisema Madinda.
Kwa mujibu wa meneja huyo, biashara ya vyuma chakavu mkoani humo, inachangia kwa kiwango kikubwa kukithiri kwa wizi wa alama hizo.
"wengi wanaiba alama hizi na kuziuza kama chuma chakavu" alisisitiza na kuwasihi wananchi kuacha kujihusisha na hujuma hizo.
Pia aliwataka wananchi kushirikiana katika kuwafichua watu wanaojihusisha na wizi wa alama hizo wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya dola.
Source: Mwananchi

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker