Tuesday, June 2, 2009

Kazi ya Kuokoa Meli Yawa Ngumu!

Kazi ya kuokoa boti ya Mv Fatih, iliyozama katika bandari ya Zanzibar Ijumaa iliyopita, bado ngumu, baada ya jitihada za kutwa nzima ya jana kutofanikisha kuivuta hadi nchi kavu.
Awali, kazi ya uokoaji ilikuwa ikifanywa na wazamiaji 30 kutoka kikosi Maalum Cha Kuzuia Magendo(KMKM) na Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ), lakini jana hiyo vikosi zaidi vya uokoaji viliongezeka.
Vikosi hivyo vilifanikiwa kuivuta meli hiyo, lakini mnyororo ulikatika na hivyo kufanya meli hiyo izame tena baharini .
Sambamba na kufanyika kwa kazi hiyo, nao askari wa Kikosi Cha Kuzuia Ghasia(FFU) walikuwa hima kudhibiti vurugu na wizi katika eneo hilo lililokuwa limefurika watu.
Miongoni mwa vitu ambavyo vilikuwa vikiibwa ni magunia ya bidhaa mbalimbali ikiwamo vitunguu,viazi,nyanya juisi na magodoro.
Hadi jana jioni majira ya saa 12.00 jitihada za vikosi hivyo zilikuwa hazijazaa matunda.
Taarifa za awali, zilisema uzembe wa Shirika la Bandari Zanzibar ndio ulisababisha ajali hiyo kwa kuwa nahodha, Ussi ali alipiga simu na kuwaeleza udhaifu wa meli hiyo wakati ikiwa njiani na kutaka kusimama eneo la Chumbe, lakini uongozi wa bandari ulikataa na kumtaka nahodha huyo kwenda hadi bandari ya Malindi.
Wakati huohuo Taarifa zinasema kwamba waliokufa katika ajali hiyo wamefikia kumi.
(Habari zaidi tembelea www.mwananchi.co.tz ).
Source: Mwananchi

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker