Wednesday, June 3, 2009

Ujenzi wa Barabara ya Ndundu-Rufiji-Somanga-Kilwa!

Na Ben Komba
Ujenzi wa barabara ya Ndundu- Rufiji mpaka Somanga- Kilwa mpaka sasa umegharimu jumla ya shilingi zaidi ya bilioni 19, ambayo ina urefu wa kilometa 56, unategemewa kukamilika rasmi mwaka 2009.Taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari waliombatana wajumbe wa bodi ya barabara ya mkoa wa Pwani, Imebainisha kwamba Barabara hiyo iliyotakiwa kukamilika baada ya miezi 30, lakini kwa sababu mbali mbali barabara hiyo inatarajiwa kukamilika rasmi hapo februari mwakani.Mradi huo unaotekelezwa na mkandarasi M.M.KHARAFI imekamilika kwa kiwango cha asilimia 13 tu, ambapo mkandarasi huyo ametoa ajira kwa wafanyakazi wapatao 410, ambao wanahudumu katika maeneo mbalimbali.Taarifa ya wakala wa barabara Mkoani Pwani imeongeza kwamba kuna vikwazo kadhaa vinavyokabili kukamilika haraka ujenzi wa barabara hiyo ikiwamo kuchelewa kutolewa kwa msamaha wa ushuru wa mafuta kwa mkandarasi wa barabara hiyo.Kikwazo kingine kikubwa ni shirika la umeme TANESCO kugoma kusimika upya nguzo zilizong’olewa wakati wa matengenezo ya barabara hiyo kwa madai ya kutaka kulipwa kama mradi mpya wa umeme hali ambayo imezoretesha kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa mradi huo.

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker