WANAFUNZI watatu, mwalimu mmoja pamoja na dereva wa Shule ya Kimataifa ya Kadama iliyoko wilayani Chato mkoani Kagera, wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupinduka.Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Bw. Henry Selewi aliliambia Majira kwa njia ya simu kuwa ajali hiyo ilitokea jana saa 6 mchana katika kitongoji cha Butengo Lumasa kilichopo Buselesele wilayani Chato.Aliwataja waliofariki kuwa ni pamoja na dereva wa basi hilo lenye namba za usajili UAJ 391 B Toyota Hiace, Bw.Tanganyika Charles (40) na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bi.Silvia Nagazibwa (35) raia wa Uganda.Wanafunzi waliofariki ni Paulo Choga(11), Baraka Furaha(12) na mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja la Owen (11).Alisema ajali hiyo pia ilijeruhi wanafunzi kadhaa pamoja na walimu waliokuwa ndani ya basi hilo huku mmoja hali yake ikielezwa kuwa mbaya na amelazwa Hospitali ya Wilaya ya Geita.Alisema kuwa wanafunzi hao walikuwa wakisafiri toka shuleni kwao kupelekwa katika kituo cha mabasi cha Buselesele ili kurejeshwa nyumbani baada ya shule kufungwa kwa mapumziko mafupi.Alisema, taarifa za awali zinadai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kukatika kwa usukani na kusababisha basi hilo kukosa mwelekeo kisha kuanguka katika mtaro kwenye barabara kuu ya Geita-Chato-
Source:Majira
WATU watatu wamekufa na wengine 16 wamejeruhiwa baada ya gari la mizigo walilopanda kushindwa kupanda mlima na kutumbukia mtoni.
Ajali hiyo ilitokea jana asubuhi katika kijiji cha Kibingo, Kigoma Vijijini na kulihusisha gari lenye namba za usajili T 922 AKR aina ya Mercedes Benz mali ya mkazi wa Kijiji cha Kalinzi, aliyetajwa kwa jina moja la Fines.Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma, George Mayunga, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja waliofariki dunia ni Daniel Masunzu (85) Mchungaji wa Kanisa la Full gospel mjini Kigoma, Mpagaze Kafikile (32) na mwingine ambaye jina lake halikufahamika.Alisema chanzo cha ajali hiyo ni gari hilo kushindwa kupanda mwinuko wa mto Mngonya na hivyo kurudi nyuma kisha kutumbukia mtoni na kusababisha maafa.
Source: Uhuru
The post taken from: Faustine's Baraza. Mdau nashukuru sana kwa jitihada zako katika kukemea uzembe unaosababisha ajali za magari hapa nchini.Na fikiri itafika siku kilio chetu kitasikika!
No comments:
Post a Comment