Wednesday, August 5, 2009

Ajali! Maoni Kutoka Faustine's Baraza!

BASI la Kampuni ya Akamba ya nchini Kenya, lililokuwa likitoka Nairobi kuja jijini Mwanza, limepinduka na kujeruhi watu 16 wakiwemo wanafunzi 13 wa sekondari za Lugeye na Nyanguge wilayani Magu.Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Jamal Rwambow alisema ajali hiyo ilitokea juzi saa 6:30 mchana katika barabara ya Mwanza -Musoma katika Kijiji cha Kandawe.Rwambow alisema basi hilo lenye namba za usajili KAU. 186 V aina ya Scania lililokuwa likiendeshwa na Daniel Njuku (50) raia wa Kenya, lilipata ajali hiyo baada ya kupasuka tairi la nyuma, upande wa kushoto na kuacha njia kabla ya kupinduka.
Mtazamo: Kuna maoni yafuatayo toka kwa Mzee wa Changamoto kuhusu bandiko langu la awali kuhusu ajali."Hivi watu wangapi wanatakiwa wafe kabla ya kuchukua hatua?"Pengine tumeshauliza swali hili saaana. Lakini labda tuanze na swali la WATU NI KINA NANI?Tunaripoti kuhusu kufa kwa watu lakini sina hakika kama wana thamani sawa mbele za viongozi wetu. LABDA HAWAONI MTU AKIFA, NI WANANCHI TUU HAWA. Kwa hiyo tusubiri mpaka afe mtu ndio watazinduka.Sijui TUANZISHE MAOMBI ILI MTU AFE TUOKOE WANANCHI NA JAMII? Tangu kuanza kwa mwezi huu wameshateketea wangapi? Ni ni wangapi wamekuwa wakiwategemea watu hao? Ni wangapi wamewekeza katika maisha ya wapendwa hao wakitegemea kupata pumziko miaka ijayo? Ni wangapi ambao wanalala wakihaha kusaka hili na lile kufanikisha maisha ya waliopoteza maisha yao ajalini? Mbona wanalopata ni salamu za Rambirambi tuuuuu?Labda hakuna mtu aliyekufa kwa sababu tunaona WATU wakiugua hupelekewa Helikopta na kusafirishwa nje ya nchi kwa matibabu. Na sijui kama kuna anayepata hata pesa ya ASPRIN japo magari yanaonesha kuwa na bima (well! kwa kuangalia kwenye vioo vya magari, sina hakika kama ni data za kweli)Lakini nadhani gharama za maisha ya sisi wananchi na HAO WATU WANAOPELEKWA NJE WAKIPATA AJALI zinaweza kuepukwa kama kutakuwa na mipango thabiti ya KUKINGA AJALI HIZI kuliko kutuacha tukiteketea".
Taken from: Faustine's Baraza

No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker