Wednesday, August 26, 2009

Ajali Zaua Watatu Moro!

Watu watatu wamefariki dunia mkoani katika ajali mbili za barabarani zilizotokea mwishoni mwa wiki.
Kamanda wa polisi mkoani Morogoro, Thobias Andengenye, alisema kuwa ajali ya kwanza ilitokea Agosti 20 katika eneo la Kiegea wilayani kilosa barabara ya Morogoro-dodoma mkoani hapa.
Andengenye alisema katika ajali hiyo gari aina ya sprinter lililokuwa likitoka jijini Dar es salaam kuelekea Singida liliwagonga watembea kwa miguu na kusababisha vifo vyao. Aliwataja waliofariki kuwa Mwanaidi Husein(200 na Anath Daglas(2) wote wakazi wa kiegea wilayani kilosa, chanzo cha ajali bado hakijafahamika.
Katika ajali nyingine gari lisilofahamika lilimgonga mtembea kwa miguu Jumanne husein(40) mkazi wa Chamwino manispaa ya morogoro (Mwananchi).

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker