Saturday, August 22, 2009

Mtoto wa Miaka 13 Amgonga na Kumuua Baba Yake Aliyekuwa Akimfundisha kuendesha Gari!

Baba mmoja wa nchini Marekani ambaye alikuwa akimfundisha mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 13 kuendesha gari, amefariki baada ya mtoto wake kumgonga na alilokuwa akimfundishia
Mashahidi wa tukio lililotokea kwenye kitongoji cha Bronx jijini New York, Marekani walisema kwamba baba wa mtoto huyo aliyejulikana kama John Cedeno, 45, alikuwa akimfundisha mtoto wake mwenye umri wa miaka 13 jinsi ya kuendesha gari.Siku ya tukio baba huyo alimpa ruhusa mtoto wake alipaki gari lake na ndipo mtoto huyo alipomgonga na kumuua hapo hapo.Familia ya mzee huyo ilikuwa imetoka kwenye mgahawa mmoja wa vyakula vya kilatino wakati mtoto huyo alipomuomba baba yake alisogeze gari lake aina ya Porsche.Mtoto huyo alikaa kwenye usukani wakati baba yake akisimama pembeni ya mlango wa gari hilo ambao ulikuwa wazi.Mtoto huyo aliirudisha gari hiyo nyuma ghafla na mlango huo wa gari ulimgonga baba yake na kumminya kwenye mti."Baba yake alitokwa na damu nyingi sana mdomoni" alisema shuhuda mmoja.Mtoto wake huku akiwa amepagawa alianza kulia huku akipiga kelele "Nimemuumiza, nimemuumiza" alisema shuhuda mwingine.Baba huyo alitangazwa amefariki hapo hapo kwenye eneo la tukio."Huu ni mkasa wa kusikitisha, bila shaka mtoto huyu ataishi maisha yake yote akikumbuka kuwa amemuua baba yake" alisema mwanamke mmoja aliyekuwepo eneo la tukio.Vyanzo vya habari vilisema kwamba hakuna uwezekano wa mtoto huyo kushtakiwa.

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker