Sunday, August 9, 2009

Treni Yapinduka Morogoro,Zaidi Ya 40 Wajeruhiwa!

Treni ya abiria iliyotoka Dar es Salaam kwenda Mwanza na Kigoma imepinduka usiku wa kuamkia leo mkoani Morogoro. Treni hiyo iliyoondoka Dar es Salaam saa 11 jana jioni imepinduka katikati ya Mazimbo na Mkata, zaidi ya watu 40 wamejeruhiwa. Ofisa Habari wa kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Midladjy Maez amesema,treni hiyo imepinduka saa nane usiku wa kuamkia leo. Kwa mujibu wa Maez, chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika. Amesema, kati ya majeruhi hao, saba wamejeruhiwa vibaya, na wamepelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Morogoro. Maez amesema, TRL imekodi mabasi 17 kuwasafirisha wasafiri ambao hawakujeruhiwa katika ajali hiyo. “Ajali hiyo imesababisha treni nyingine iliyokuwa ikitokea Bara kwenda Dar es Salaam kukwama katika eneo hilo lililoko Wilaya ya Kilosa..." amesema. Maez amesema, TRL imepeleka mabasi saba kuwasafirisha abiria waliokuwa wakitoka Kigoma kwenda Dar ili wafikishwe stesheni waendelee na safari. Amesema,kampuni hiyo pia imekodi mabasi 10 kuwasafirisha abiria waliopata ajali wanaokwenda Kigoma(Source:Habari Leo)
HISIA ZANGU:
''Ni habari ya kusikitisha ikizingatiwa kwamba kumekuwa na mvutano kati ya wafanyakazi na menejimenti ya TRL. Hii inaamsha hisia kwamba inawezekana hii ni hujuma, lakini kwanini kuhatarisha maisha ya wale wasio na hatia?Tuziachie mamlaka husika kufanya uchunguzi na kutoa taarifa rasmi na sahihi za chanzo cha ajali hiyo. Nawapa pole majeruhi wote na waliopoteza maisha Mungu aziweke roho zao mahala pema peponi. Amin".

No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker