Saturday, August 29, 2009

SUMATRA YAZINDUKA!

MAMLAKA ya Usimamizi wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) mkoani Tanga, ulizuia kuondoka kwa meli ya Mv Spice Islander, kutokana na nahodha wake kutokuwa na sifa za kuendesha meli ya abiria.Hali hiyo ilisababisha abiria zaidi ya 200 waliokuwa wakisafiri kati ya Tanga na Zanzibar, kukwama kwa saa nane katika bandari ya Tanga na kusababisha usumbufu mkubwa kwa abiria.Hata hivyo, meli hiyo iliruhusiwa kuondoka baada ya kupatikana nahodha mwingine, ambaye alionekana kuwa na vigezo vinavyohitajika baada ya kukaguliwa vyeti vyake.Wakizungumza na Uhuru, nje ya lango la kuingilia bandarini hapo, baadhi ya abiria walielezea kukerwa kwao na hatua hiyo ambayo wameiita ni usumbufu kwa abiria ambao hawana hatia.Rashid Abdalla, mkazi wa Kinowe kisiwani Pemba, alisema alifika bandarini hapo saa 12.30 asubuhi kwa ajili ya safari hiyo, lakini alizuiwa kuingia ndani ya meli baada ya kuelezwa kuwa hakuna nahodha mwenye uwezo wa kuendesha chombo hicho.
"Huu ni usumbufu ambao hatustahili kuupata kama abiria. Kama nahodha hakuwa na vigezo inakuwaje siku zote anaendesha meli hii bila kuchukuliwa hatua. Huu ni uonevu kwa abiria,”
alisema.
Kwa upande wake, Ofisa Mfawidhi wa SUMATRA mkoani hapa, Johns Makwale, alisema kuwa meli hiyo ilizuiwa kutokana na nahodha wake kutokuwa na vigezo vinavyostahili.Alisema kuwa SUMATRA iliamua kukagua vyeti vya nahodha huyo Mabruk Msellem, ambapo ilibaini kuwa hana sifa zinazomuwezesha kuendesha chombo chenye abiria.Hata hivyo, Makwale alisema kuwa mamlaka hiyo imekuwa ikifanya ukaguzi kwenye vyombo vya usafiri mara kwa mara ikiwa ni hatua ya kudhibiti matukio ya ajali za majini.

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker