Saturday, February 28, 2009

Mazingira Hatarishi kwa Watoto!



Kwa kawaida maeneo ambayo yanatumiwa na watu wengi kama maeneo ya shule, misikiti na makanisa, ni vema yakiwa na "Alama za Kivuko cha Watembea kwa kwa Miguu" au "Zebra Crossing" ili kuepusha hatari ya wavukaji katika maeneo kama hayo kugongwa na magari yaendayo kasi. Pichani ni watoto wa shule waliokutwa Mkoani Morogoro wakivuka barabara bila mpangilio maalumu na hivyo kujiweka katika hatari ya kugongwa. Ni vema mamlaka husika zikazingatia hilo kwani watoto wengi wamepata athari, wamepoteza viungo au hata kupoteza maisha kutokana na kugongwa na magari yaendayo kasi. Watoto wanaoonekana pichani walipohojiwa, walisema kwamba wenzao wengi wameishagongwa na magari katika eneo hilo.

Friday, February 27, 2009

DOKEZO LA LEO!

"Wajibu wa kwanza wa mmiliki wa chombo ni kuhakikisha usalama wa gari na abiria, wajibu wa Serikali kupitia vyombo vyake ni kuhakikisha msafirishaji anatimiza wajibu wake kwa mujibu wa masharti ya leseni na sheria za usalama barabarani, madereva au makondakta ni wakala tu"

Matumizi sahihi ya Barabara huepusha ajali!




Madereva wa Malori Wanapotawala njia!

Ni kitu cha kawaida kuona madereva wa malori wakitamba njiani na kutishia magari madogo kama inavyoonekana pichani. Wadau mnasemaje kuhusu hili?

Thursday, February 26, 2009

Hatari kwa Wanafunzi Shule ya Jangwani!


















Ni muda mrefu sasa nimekuwa nikifuatilia kuona kama kitawekwa kivuko cha watembea kwa miguu katika lango kuu la shule ya sekondari Jangwani, hilo halijatokea na kusababisha hali ya hofu hasa wanafunzi wanapotoka au kuingia shule. Ili kuepusha maafa nafiri ni muda muafaka kwa mamlaka husika kufanya hivyo.

Wednesday, February 25, 2009

ROAD ACCIDENTS ARE AVOIDABLE.

Yesterday, the meeting of Bus owners and their Agents (DARBOA) was officiated by SUMATRA Director General Mr. Israel Sekilasa. The theme of the meeting was "Road accidents are Avoidable".
Stakeholders from various institutions participated in this important meeting. One of the participants in the meeting was the National Traffic Commander, James Kombe. I am delighted to note that that the old adage that "Ajali haina kinga" is now disappering! I believe this way, we can now move forward.

Maumivu.



Pichani ni mwananchi ambaye amelazwa katika wodi ya majeruhi ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili(MOI) akiwa na maumivu makali baada ya kuvunjilka ambao unaonekana umewekewa vyuma au "antenna" kama wengi walivyozoea kuuita, lakini kwa jila kitaalam inaitwa "External Fixator" ambavyo husaidia walioumia katika kuunganisha mifupa.
Ni dhahiri kwamba uzalishajii kwa mwananchi huyu umesimama wakati akiwa na wodini na hata baada ya kutoka wodini kwani ataendelea kuuguza mkono kwa muda kidogo.
Tujiulize, anapokuwa wodini au hata baada ya kutoka wodini lakini akiwa katika hali kama hiyo,anazalisha nini, familia yake inapataje mahitaji muhimu? Ni dhahiri kwamba, yeye na familia yeke wanateseka. Swali linakuja, je dereva aliyesababisha haya kwa uzembe anafanywa nini? analipa faini ndogo na baada ya wiki moja anarudi barabarani anafanya uzembe mwingine na kuharibu maisha ya watu wengine?Nafikiri imefika wakati wa kutoa adhabu kali ambazo zitamfanya dereva awe mwangalifu na kufikiria adha atakayopata au kifungo iwapo atashindwa kulipa faini.Nina imani faini kubwa itapunguza kwa kiasi kikubwa uzembe wa madereva. (Picha na Hamisi Bilali)

Madereva Watatumaliza!!



Madhara ya ajali ni makubwa sana, watu hupoteza viungo na hatimaye kuwa na ulemavu wa kudumu. Kwa miaka mingi nimeshuhudia watu wakiumia kama inavyoonekana pichani na kupoteza viungo kama mikono yote au miguu yote. Hali hii humfanya aliyeumia kuanza maisha mapya ya mahangaiko na taabu kwa sababu anakuwa hawezi kujihudumia kama ilivyokuwa hapo mwanzo alipokuwa na viungo vyote.
Hali hii haimuathiri muumiaji tu, bali husababisha maisha magumu kwa familia na wale wote wanaomtegemea.
Takwimu za SUMATRA zinaonyesha kwamba, asilimia 55 ya ajali husababishwa na uzembe wa madereva. Na mfano mzuri ni wa ajali ya hivi karibuni ambapo dereva wa lori kutokana na uzembe, aligongana uso kwa uso na basi liitwalo Hekima.
Je, wadau tunakubali kuishia katika ulemavu wa kutisha na mateso kwetu na familia zetu? Je, tumekubali kuishia kuwa na ulemavu wa kudumu kwa ajili tu dereva ameamua kufanya mzaha akiwa barabarani? Nafikiri kila mmoja atasema "Hapana". Kama sote tunapingana na uzembe huo, nafikiri ni muda muafaka wa kusema, "NO!" Jamani, tuamke na tuanze kupambana na madereva wazembe hasa hawa wa nabasi ya abiria (picha kwa hisani ya mtandao).

Kwa Mtindo Huu....!!!



Kwa mtindo huu nadhani jitihada za kudhibiti ajali hapa nchini itakuwa ni sawa na "Kupigia Mbuzi Gitaa" kwa maana ya kwamba ajali zitaendelea na watu watapoteza maisha kama tunavyoshuhudia. Picha hii ilipigwa kutoka katika treni ya Reli ya Kati maeneo ya Mkoa wa Singida. Cha kwanza, basi limejaa mpaka watu wamekaa juu sehemu ya mizigo; Cha pili, basi likuwa linaenda kwa mwendo wa kasi ili kushindana na treni bila kujali kwamba barabara linapopita basi si nzuri ina mashimo na mengine ni makubwa sana. Bahati kutokana na umbali namba z usajili za basi hilo hazikupatikana, lakini wenyeji wa huko wakiona rangi ya basi watajua ni basi la kampuni gani.
Wadau, nafikiri kazi ya kupambana na ajali ni kubwa na nzito kuliko inavyoonekana, lakini kwa jitihada za pamoja nina imani tutashinda na hatimaye kuokoa maisha na mali(Picha na Hamisi Bilali-DSM)

Tuesday, February 24, 2009

CADILLAC ONE.


SOMEBODY SENT THIS PHOTO TO ME(SORRY IT IS NOT CLEAR).
IT IS THE CADILLAC ONE, OBAMA'S CAR. I AM MOVED WITH THE SAFETY MEASURES. IT CAN STAND THE BOMBS;BULLET PROOF WINDOWS; THE TYRES ARE PUCTURE PROOF etc;MAY BE OUR BUSES AND DALADALAS SHOULD HAVE THE SAME SAFETY MEASURES TO AVOID ACCIDENTS. CLICK ON THE PHOTO TO GET A CLEAR VIEW OF THE CAR.WADAU ,COMMENTS?


WADAU HII MNAIONAJE?
(Photo by Hamisi Bilali)


MAITI ZAIDI ZATAMBULIWA

Maiti wengine zaidi wametambuliwa kutokana na ajali ya Basi la Hekima, maiti waliotambuliwa ni dereva wa basi Jackson Kahogi, Yules Sanga, Anthony Sanga na utingo wa lori la mafuta aliyetambuliwa kama Ahadi Lwambano.
Habari zinaendelea kutufikia kwamba majeruhi wanaendelea vema.

Monday, February 23, 2009

KUTUMIKIA MABWANA WAWILI KWA WAKATI MMOJA?



Jamani japo tunalalamika kwamba kuna mapungufu kwa askari wa kikosi cha usalama barabrani kina mapungufu, lakini sisi pia tunatakiwa kujua nini cha kufanya.

Pichani anaonekana dereva ambaye anaendesha gari na kusikiliza simu yake mkononi. kwa lugha rahisi au hata kwa kuangalia tu,inaonekana umakini wake umepungua kwa sababu umakini wote amehamishia katika simu.

UNAPOENDESHA USISIKILIZE SIMU AU KUTUMA MESEJI, OKOA MALI NA MAISHA!

AJALI YAUA SITA IRINGA

Mapema leo katika "Breaking News" nilitoa taarifa ya ajali ya basi la Hekima lililoua watu 6. Ifuatayo ni Taarifa kamili ya ajali hiyo kama ilivyoripotiwa na Francis Godwin katika gazeti la Tanzania Daima la leo.
Jinamizi la Ajali za barabarani, linaendelea kuliandama taifa, baada ya jana ajali nyingine iliyohusisha basi la abiria la Hekima, kugongana uso kwa uso na lori la mafuta na kusababisha vifo vya watu sita papo hapo na kuwajeruhi wengine 20.
Miongoni mwa waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni pamoja na dereva wa basi hilo na utingo wa lori ambao hata hivyo majina yao hayakuweza kupatikana mara moja.
Mashuhuda wa ajali hiyo waliiambia Tanzania daima kuwa basi hilo lenye namba za usajili T 402 AM, mali ya Kampuni ya Hekima lilikuwa likitokea Tunduma, Mkoani Mbeya kwenda jijini Dar es salaam.
Baadhi ya abiria walionusurika katika ajali hiyo na ambao wamelazwa katika hospitali ya mkoa mjini hapa, walisema kwa nyakati tofauti kuwa chanzo cha ajali hiyo ni lori la mafuta kutaka kuyapita malori mengine mawili bila kujali basi hilo ambali lilikuwa likija mbele yake.
Majeruhi hao, Gibon Kajingili(25) na Raban Ngogo(23) wote wakazi wa mbeya, walisema dereva wa basi hilo alijitahidi kulikwepa lori hilo lakini ilishindikana na hivyo kugongana nalo uso kwa uso."Kama si uhodari wa dereva wa basi la Hekima kujitahidi kulikwepa lori hilo, huenda idadi ya vifo ingekuwa kubwa zaidi", alisema Ngogo.
Mkazi mmoja wa eneo wa eneo la ajali, Baton Ntuli, ambaye alifika na kumwokoa mmoja kati ya abiria aliyekuwemo katika basi hilo, Yules Nauli Sanga, alisema bada ya kufika eneo hilo wananchi walikuwa wakiendelea kuokoa majeruhi katika basi hilo na huenda kukawa na idadi kubwa ya watu waliopoteza masiha.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa, Dk. Oscar Gabone, alisema hadi majira ya saa 12 jana jioni, alikuwa amepokea majeruhi mmoja aliyefikishwa hospitalini hapo ambaye hata hivyo alifariki dunia wakati akiendelea na matibabu.
Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Alisema abiria watano ndio waliopoteza maisha katika ajali hiyo, akiwemo dereva wa basi na utingo wa lori ambao hata hivyo hakuweza kupata majina yao mara moja.
Kamanda Nyombi alisema katika ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 9.45 alasiri, abiria 15 ndio waliojeruhiwa na wako katika hali mbaya na wanaendelea na matibabu katika hospitali ya Mkoa wa Iringa.
Pia alisema majina ya waliopoteza maisha katika ajali hiyo bado hayajatambuliwa na kuwa miili yote imehifadhiwa katika hospitali hiyo ya Mkoa na kazi ya utambuzi ilianza mara moja jana.
Hata hivyo alisema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa lori la mafuta ambaye alitaka kuyapita magari mengine yaliyokuwa mbele pasipokuzingatia sheria za usalama barabrani.
Mkuu wa wilaya ya Kilolo, Dk. Athumani Mfutakamba, alisema kuwa jali hiyo ni mbaya kutokea katika wilaya hiyo ya Kilolo mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Saidi, alikuwa miongoni mwa viongozi wa serikali kusaidia kuwaokoa majeruhi hao.
HOJA: Jamani watanzania, hadi lini tutazidi kusikia habari za vifo kutokana na ajali zilizosababishwa na uzembe kama hii? wadau mjadala upo wazi.

DOKEZO LA LEO!

STAY OFF YOUR CELL PHONE WHEN YOU ARE DRIVING. PAY ATTENTION.

Watanzania huwa Tunashangaa badala ya Kutoa Msaada!


Nadhani wadau mtakubaliana nami kwamba, mara nyingi inapotokea ajali huwa tunajazana na kushangaa badala ya kutoa msaada kwa majeruhi. Na wengine hudiriki hata kuwaibia majeruhi na maiti badala kutoa msaada. Nimeshuhudia katika matukio ya ajali watu wanajazana na kumzunguka majeruhi kiasi cha kushindwa kupumua! Katika ajali inayoonekana pichani, ilitokea maeneo ya Vigwaza Mkoa wa Pwani. Wananchi walijazana kiasi cha kuwafanya majeruhi kupumua.

Hoja yangu: Taifa lina jukumu la kuwafundisha watanzania kutoa huduma ya kwanza(First Aid) ili kuokoa maisha.

BREAKING NEWS!

Taarifa zilizopatikana punde zinasema kwamba, basi la abiria linalofanya safari zake kati ya Dar es salaam na Iringa linaloitwa Hekima limepata ajali baada ya kugongana na lori na kusababisha vifo vya watu 6 na majeruhi kadhaa. Taarifa zaidi zaidi zitarushwa baada ya kufanya mawasilaino na vyombo husika mkoani Iringa. Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, Amin.

Sunday, February 22, 2009

JOKE!

Selfish Dar Lawyer!!!
A very successful lawyer in Dar es salaam parked his brand new RAV4 in front of his office, ready to show it off to his colleagues.
As he got out, a daladala bus passed too close and completely tore off the door on the driver's side. The lawyer immediately grabbed his cell phone, dialled the police and within minutes a policeman pulled up.
Before the officer had a chance to ask any questions, the lawyer started screaming hysterically. His RAV4, which he had just picked up the day before, was now completely ruined and would never be the same, no matter what a mechanic did to it.
When the lawyer finally wound down from his ranting and raving, the officer shook his head in disgust and disbelief......"I can't believ how materialistic you lawyers are", he said. "You are so focused on your possessions that you don't notice anything else". "How you can say such a thing?" Asked the lawyer.
The cop replied, "Don't you know that your left arm is missing from the elbow down?" it must have been torn off when the daladala hit you".
"Oh My God!" screamed the lawyer. "Where's my RAV4?"

Maoni ya Wadau Kuhusu Ongezeko la Ajali Nchini.

Ifuatayo ni taarifa niliyoikuta katika blogu ya Damija(http:www.damijablogspot.com) iliyopostiwa tarehe 17 January 2009 na nikaona ni muhimu wadau wengine pia wapate ladha. Karibuni.
AJALI ZA BARABARANI ZINATUMALIZIA WAPENDWA WETU BONGO....Ujumbe toka kwa da'Janeth Jesse.
Napenda kuleta dukuduku langu kwa wadau wote wa blog yetu ya jamii ili tulijadili ktk kujenga kuhusu AJALI ZA BARABARANI BONGO,jamani kwakweli tumechoka watu wanateketea imefikia steji sasa na tuseme ENOUGH IS ENOUGH sasa na sisi,haijatimia hata week1 tangia basi la kampuni ya TASHRIFF liwafyeke abiria zaidi ya nusu waliokuwa wakisafiri (30)na wengine 29 kulazwa ktk hospital za Muheza teule na Bombo Tanga,huu ni msiba mkubwa sana UHAI NI KITU CHA THAMANI NAFUU MTU AKUIBIE HELA AU MADINI KULIKO AKUTOE ROHO YAKO.Basi la kampuni hiihii wadau mkumbuke lilishawahi kupoteza maisha ya abiria (78) lilipofunikwa na maji meneo ya kibanda Muheza, Tanga.KITU GANI kifanyike wadau kuepuka vifo vya kizembe vya namna hii?dereva kaua kakimbia ni mhuni anakabidhiwa chombo kilichobeba roho za watu,kwa uzoefu wangu wa kuishi bongo miaka mingi naamini karibia nusu ya waendesha magari daresalaam mjini hawana leseni na nusu ya waendesha vyombo wanaendesha wamelewa,ni kawaida kuwakuta watu wamepaki magari yao bar wanakunywa pombe kisha wanaendesha,jamani jamani tunauana jama.HILI JESHI LA POLISI KITENGO CHA TRAFFIC utawakuta wote wana vitambi kwa rushwa na kutafutia watu leseni kwa njia za mazabe.JK MAISHA BORA NI PAMOJA NA SHERIA KALI ZA BARABARANI KWANI ZINAHUSU UHAI AMBAO NI KITU CHA THAMANI KULIKO CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)....MunguIibariki Tanzania Mungu Ibariki Afrika. Mdau wa Kwasemgaya safarini DENMARK mara1
Posted by Mija Shija Sayi at
10:15 PM
1 comments:
Koero Mkundi said...
Hii misemo ya kiswahili wakati mwingine huwa inanitatiza,eti ajali haina kinga, hivi kweli huu msemo bado una exist?Na je bado unafundishwa huko mashuleni? kama bado unatumika na unafundishwa huko mashuleni, basi juhudi za serikali kutoa elimu ya usalama barabarani ni kazi bure.Utafundishaje elimu ya usalama barabarani wakati tunambiwa ajali haina kinga?Nadhani umefika wakati wa hizi methali, misemo na nahau zetu kuchunguzwa kama zinaenda na wakati maana nyingine zinatufundisha uzembe. Naomba kutoa hoja.

Ajali Ya Basi la Wachezaji Nigeria!

Basi la timu hiyo liligongana uso kwa uso na basi jingine la abiria. Ado Umar kiongozi wa timu hiyo alifariki hapo hapo na mchezaji Abdullahi Sabiu alifariki jumamosi hospitali.Ajali hiyo pia ilipoteza maisha ya watu wengine watano wa basi la abiria.Wachezaji kadhaa wa timu hiyo walijeruhiwa kutokana na ajali hiyo na bado wanaendelea na matibabu katika hospitali moja katika mji wa Gombe.Afisa wa chama cha soka cha Nigeria (NPL)Tunji Babalola alisema kwamba timu hiyo ilikuwa ikisafiri kuelekea mji wa Gombe kucheza na timu ya Wikki Tourist katika mechi ya ligi ya Nigeria.Ajali hiyo mbaya imekuja mwezi mmoja baada ya timu nyingine ya daraja la chini Jimeta United kupoteza wachezaji wake 17 na viongozi wa timu baada ya basi lao kupata ajali wakati wakielekea Abuja kwenye mechi ya ligi. (Na Mohamed Kindindi -Nifahamishe.com)

TAFADHALI FUNGA MKANDA KUOKOA MAISHA




Katika picha zinazoonekana katika habari hii, ni gari (pick-up)iliyogongana na trekta uso kwa uso. Dereva alikuwa ni mwanamke mwenye umri wa miaka 30 ambaye alikufa papo hapo. Pembeni yake Katika alikuwa abiria mwenyeumri wa miaka 28, aliyejeruhiwa vibaya sana na hata jinsi ya kumtoa ilikuwa ni kazi nzito.


Kiti cha nyuma kulikuwa na watoto watatu ambao wote hawakuwa wamefunga mikanda ya kiti. Mtoto wa kwanza mwenye umri wa miaka 3, alitupwa chini ya kiti akabanwa na kufa papo hapo. Mtoto mwingine mwenye umri wa miaka 12 alikufa papo hapo baaday kutupwa tupwa ndani ya gari kwa ajili ya kutofunga mkanda, na mtoto wa mwisho mwenye umri wa miaka 15 aliokolewa na kupelekwa hopitali akiwa mahututi.


Dereva wa trekta hakuumia hata kidogo. Inasemekana dereva wa pick-up alikuwa akiendesha gari kwa mwendo wa kasi bila kujali hali ya unyevunyevu iliyokuwepo barabarani.


Tuna imani kwamba, iwapo waliokuwepo ndani ya gari wangefunga mikanda kiwango cha madhara kisingefikia hapo(Picha kwa hisani ya www.cars-accident.com).


Somo: Ni muhimu kufunga mikanda tuwapo katika vyombo vya usafiri kuokoa maisha na mali.

Saturday, February 21, 2009

DOKEZO LA LEO!

"Utafiti uliosimamiwa na SUMATRA na kufanywa na watafiti kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es salaam umeonyesha kuwa dereva ndio chanzo cha ajali kwa asilimia 55".

WATANZANIA TUCHOKE KUSIKIA HABARI ZA AJALI!


Nafikiri watanzania inabidi tufike mahali na kuamua kwamba sasa tumechoka kusikia habari za ajali kila kukicha. Kama inavyoonekana pichani,gari hili no bovu hata kwa kuangalia kwa macho tu. Lakini abiria wamekubali kurundikwa kama mihogo. Je, ikitokea ajali katika mazingira kama haya, ni watu wangapi watapoteza maisha?(picha kwa hisani ya gazeti la mwananchi)

Hoja: Watanzania tufike mahali na kuamua kwamba tumechoshwa na hizi habari za ajali na tuchukue hatua madhubuti za kuzia ajali.

MADHARA YA UDEREVA USIO MAKINI!


Kila kukicha, vyombo vya habari vinaripoti juu ya ajali mbalimbali ambazo hupoteza maisha na mali. Pichani ni mwathirika wa ajali ambaye amepoteza kiungo muhimu katika maisha yake, mguu. Hivyo maisha yake hayatakuwa kama ilivyokuwa mwanzoni kabla ya ajali.

Akieleza tukio la ajali hiyo, kijana anayeonekana pichani (jina limehifadhiwa)alisema kwamba ilikuwa majira ya saa moja usiku huko Mkuranga, akitoka matembezini, gari lililokuwa ikienda kwa kasi sana lilipasuka gurudumu la mbele na hivyo gari liliyumbayumba na kumfuata yeye akiwa pembeni mwa barabara, likamgonga na halikusimama tena likakimbia.Hakujua kilichotekea kwani alipoteza fahamu. Wasamaria wema walimbeba na kumpeleka hospitali ya Mkuranga na hatimaye akapewa rufaa hadi Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) ambapo wataalam waligundua kwamba mguu umeharibika kabisa na hivyo ikabidi ukatwe chini ya goti.

kutokana na uzembe wa dreva huyo, kijana anayeonekana pichani amepata ulemavu wa kudumu.

Mr Bobos Class tunampa pole kwa matatizo yaliyompata.ushauri tunaompa ni kwamba kupoteza kiungo sio mwisho wa maisha.

Thursday, February 19, 2009

EPUKA MATUMIZI YA SIMU ZA MKONONI UNAPOENDESHA


Ni kitu ambacho watu wengi wanakichukulia kuwa kidogo na wanakidharau lakini madhara yake ni makubwa sana! Kupokea simu ya mkononi au kutuma meseji unapoendesha!

Utafiti uliofanywa na Harvard University unaonyesha kwamba nchini Marekani, kila mwaka zaidi ya watu 200 hufariki dunia na wengine 500,000 hupata majeraha mbalimbali kutokana na ajali zinazosababishwa na matumizi ya simu za mkononi aidha wakiongea au kutuma meseji wakiwa wanaendesha.
Pichani kulia ni moja ya ajali ambazo zilitokea dreva alipokuwa anaendesha na kutuma meseji!
UNAPOENDESHA USIONGEE NA SIMU YA MKONONI AU KUTUMA MESEJI, UTAOKOA MAISHA!

Tuesday, February 17, 2009

AJALI ZINA KINGA!


Wengi hupendelea kusema kwamba "Ajali Haina Kinga", kwa aslimia fulani hii ina ukweli kwa sababu hakuna anayepanga kwamba sasa afanye ajali.
Ninachosema mimi ni kwamba,ajali zina kinga. Kama inavyoonekana pichani, je mtu kama huyu aliyekaa juu ya guta kwa staili hii akidondoka na kuumia atamlaumu nani? Au na yeye atasema ajali haina kinga? Na je, Askari wa usalama barabarani wanawaona watu kama hawa?
Wadau maoni yenu yanakaribishwa juu ya hili.

KWA TAKWIMU HIZI TUSIMAME KIDETE!

Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipokuwa akiahirisha Kikao Cha 14 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitoa takwimu kwamba mwaka jana kulikuwa na ajali za barabrani 20,148 ikiwa ni wastani wa ajali 55 kila siku au ajali 1,679 kwa mwezi na kusababisha jumla ya vifo vya watu 2,924 na kujeruhii wengine 17,825.
Tangu tuanze mwaka huu wa 2009, jumla ya ajali 252 zimeishatokea na kusababisha vifo 185 na majeruhi 387.
Hoja yangu: Takwimu hizi hakika zinaogofya na ni muhimu hatua madhubuti zichukuliwe ikiwa ni pamoja na adhabu kali dhidi ya wahusika ili iwe mfano kwa wengine.

JIRANI ZETU NAO WAMO!




Kwa majirani zetu inaonekana na wao hawapo nyuma, takwimu zilizotolewa nchini Zambia zinaonyesha kwamba kila mwaka kuna watu 13,000 hupoteza maisha kutokana na ajali za brabarani. Pichani ni ajali iliyotokea katika jimbo la Ndola,dreva wa gari dogo na abiria wake aliyekuwa amekaa kiti cha nyuma walipoteza maisha papo hapo, na dreva wa basi walilogongana nalo na abiria wake wote walikuwa salama.
Chanzo cha ajali, inasemeka kwamba baada ya kufika katika T-junction, gari dogo lilipata hitilafu ya breki hivyo kushindwa kusimama na kukutana uso kwa uso na basi hilo.
Hoja yangu: Ni vema kuhakikisha kwamba gari linafanyiwa matengenezo ya mara kwa mara ili kuepukana na ajali kama hizi.

Monday, February 16, 2009

WAATHIRIKA AJALI YA ARUSHA KUDAI FIDIA

Waathirika wa ajali iliyotokea hivi karibuni katika barabara kuu ya Arusha-Moshi, katika daraja la Mto Nduruma wilayani Arumeru, wameshauriwa kuandaa taratibu za kudai fidia kutoka katika bima ili waweze kulipwa haki zao.
Ushauri huo umetolewa mwishoni mwa wiki mjini Arusha, na Katibu wa Baraza la Huduma za Usafirishaji Nchi Kavu Bw. Oscar Kikoyo alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Usimamizi na Ushauri wa Huduma za Usafirishaji Mkoa wa Arusha, kuhusu utaratibu wa waathirika wa ajali hiyo kuwasilisha madai yao ili walipwe fidia.
Amesema kuwa kwa mujibu wa sheria mbalimbali zinazotawala sekta ya usafirishaji nchini, ikitokea ajali ni lazima wenye chombo cha usafiri, pamoja ba bima kumlipa mwathirika wa ajali ikiwa ni pamoja na waliopoteza maisha(Taarifa hii imeandikwa na Magesa Magesa wa gazeti la majira 16 Februari, 2009).
Hoja yangu: Ni jambo la kutia moyo kuona kwamba kuna vyombo ambavyo vipo tayari kutoa ushauri na kuwasaidia walioathirika katika ajali mbalimbali kudai haki kwanii wengi wa waathirika hupoteza haki zao kwa kutojua au wanapoona zoezi zima la kudai fidia linakuwa ni mlolongo mrefu.

TRAFIKI HAWAJAMUELEWA WAZIRI MKUU PINDA


Ifuatayo ni makala iliyoandikwa na Flora Wingia,mwandishi wa gazeti la Nipashe la Februari 15, 2009 katika safu ya maoni. kwa kuzingatia kwamba moja kwa moja inahausu suala kupunguza ajali nadhani ni ema tukaiweka hapa ili wadau wanaohusika na masuala ya ajali na jamii kwa ujumla wakapata ujumbe mzuri kutoka katika makala hii.

Flora ameanza kwa kuandika;

"Akiahirisha Mkutano wa 14 wa Bunge kule Dodoma wiki hii Waziri Mkuu Mizengo Pinda pamoja na mambo mengine amelishikilia bango suala la ajali za barabarani ambazo bado ni tishio kwa maisha ya watu na mali kupotea wkati zinaweza kuzuiwa kwa kiwango kikubwa.

hakuna mtu asiyetambua jinsi taarifa nyingi kuhusu ajali za barabarani zinavyoripotiwa karibu kila siku katika miji yetu mbalimbali. na katika ajali hizi, maisha ya watu wasiokuwa na hatia yamekuwa yakipotea huku wengine wakibakia na vilema ya kudumu, achilia mbali uharibifu wa vyombo vyenyewe vya usafiri.

miongoni mwa vyanzo vya ajali hizi ni pamoja na mwendo wa kasi, madereva wasio wazoefu katika uendeshaji wa magari, madereva walevi na pia vyombo vyenyewe kutofanyiwa matengenezo ya mara kwa mara na kadhalika.

kwa upande mwingine, ajali hizo pengine kwa kiasi kikubwa zingeweza kuepukwa ikiwa polisi wa usalama barabarani wangetimiza wajibu wao ipasavyo.
baadhi ya madereva wamekuwa wakijiona kuwa hakuna anayweza kuwagusa na zaidi pale wanapotoa rushwa kwa baadhi ya polisi wetu wa usalama barabarani baada ya kuvunja sheria.
Wakati akifunga kikao cha Bunge wiki hii, Waziri Mkuu Pinda alivilaumu vyombo vya dola kwa kutosimamia sheria zilizopo zifanye kazi kikamilifu na hivyo kuwapa mwanya madereva kufanya vile watakavyo.
kwa mfano, alisema alikataza matumizi ya majani, mawe na magogo, kama alama ya kuonyesha kuharibika kwa gari, na badala yake vitumike viakisi mwanga(triangle reflectors)pembetatu.
pamoja na agizo hilo, lakini hadi leo hii, bado vitu hivyo vinaonekana barabarani pale gari linapoharibika. Matokeo yake, ajali nyingi zimeonekana kutokea katika eneo lenye alama hizo badala ya reflectors.
wanaopaswa kuhakikisha alama sahihi za barabarani zinakuwepo na zinazingatiwa ni trafiki wetu. Hawa wamepewa uwezo wa kuchukulia hatua za kisheria watakaobainika kuweka majani kama ishara ya tahadhari.
lakini swali ni je, kwanini hili hawalisimamii ipasavyo? Wamemuelewa Waziri wetu Mkuu? Kwa tafakari yangu nadhani bado hawajamuelewa. Kama wangemuelewa, uchafu huo unaowekwa barabarani ambao umechangia kutokea ajali nyingi na kwa muda mrefu sasa ungekuwa umeshaondolewa kitambo.
Wakati nalazimika kuungana na waziri mkuu kuwalaumu trafiki wetu kwa uzembe huo, lakini pia niiulize serikali yetu, kwamba je, polisi wa usalama barabarani wanazo nyenzo za kutosa kuwawezesha kusambaa sehemu mbalimbali katika umbali fulani wa barabara zetu ili kufuatilia nyendo za madereva wawapo safarini?
Hawa wanahitaji maari ya doria ili kuweza kuwanasa madereva wanaovunja sheria na kanuni za barabarani. pia wanapaswa kulipwa mishahara toshelezi kuwafanya waepuke vishawishi vya kudai chochote(rushwa) toka kwa madereva ili kuficha wavunjifuwa sheria na kanuni za usalama barabrani. Pengine haya yanaweza kusaidia kuwapa motisha mapolisi wetu watekeleze wajibu wao kwa ari na uadilifu. Vinginevyo, ajali zitaendelea kutikisa nchi huku nguvu kazi muhimu ikiendelea kutoweka.
katika angalizo, Waziri Mkuu ametoa takwimu kwamba mwaka jana kulikuwa na ajali za barabrani 20,148 ikiwa ni wastani wa ajali 55 kila siku au ajali 1,679 kwa mwezi na kusababisha jumla ya vifo vya watu 2,924 na kujeruhii wengine 17,825.
kwa Januari mwaka huu, akaongeza kuwa kulitokea ajali 252 ambazo zilisababisha vifo 185 na majeruhi 387. Takwimu hizi hakika zinaogofya na ni muhimu hatua madhubuti zichukuliwe ikiwa ni pamoja na adhabu kali dhidi ya wahusika ili iwe mfano kwa wengine.
Hata hivyo, Waziri Mkuu amependekeza pamoja na matumizi yaa viakisi mwanga, pia madereva wanaobainika kusababisha ajali wafungiwe leseni kwa kipindi kirefu na kama ni mara nyingi, basi wanyang'anywe kabisa leseni. hili hata mimi naliafiki ".
Hoja yangu:Makala hii ni muhimu na inabeba yale yote ambayo Waziri Mkuu alipendekeza ili kuhakikisha kwamba maisha na mali haviteketei kwa sababu ya uzembe wa madereva ambao hawathamini maisha ya binadamu wenzao. nathubutu kusema kwamba wanapoona binadamu mwingine amekufa haimshtui na labda anajisikia furaha. Kwanini? kwa sababu wengekuwa hawapo hivyo basi wangezingatia sheria na maadili ya kazi yao na kuokoa maisha na mali za watu. Kwa matrafiki hatuna jipya la uongeza, karibu yote yameshaongelewa, tusubiri kuona utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu.

AJALI NA MOTO PAPO HAPO!


Katika ajali kama hii ni mara chache watu kutoka hai. ujumbe wetu, AJALI ZINA KINGA, ENDESHA KWA UANGALIFU

DAKTARI WA MIFUGO AFA AJALINI.

Habari iliyopatikana katika gazeti la Majira la leo inaripoti kwamba, gari lililokuwa likiendeshwa na mhandisi wa shirika la Ugavi wa Umeme nchini(TANESCO) tawi la Moshi, mkoani Kilimanjaro, limepata ajali na kumuua Daktari wa Mifugo, Bw. Amani Tete anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 40-45.
kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Lucas Ng'hoboko alisema marehemu marehemu ni daktari wa mifugo Machame, wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro na gari iliyopata ajali ni Toyota Chaser yenye namba za usajili T132 ATE. alisema ajali ilitokea eneo la mnadani Weruweru katika barabara kuu ya moshi Arusha.
Hoja yetu: Ajali za barabarani zina madhara makubwa kama inayoonekana katika ajali hii kwamba mtaalamu ambaye Taifa linamhitaji ameshapoteza maisha na kuacha pengo si kwa ndugu na jama, sehemu anayofanyia kazi bali ni kwa Taifa kwa ujumla. TUENDESHE KWA UANGALIFU KUZUIA AJALI.

Sunday, February 15, 2009

LORI LA TAKA LAUA.


Lori la la kubeba taka liliigonga Bajaj na kusababisha kifo cha mama na mtoto wake. Ajali hiyo ilitokea barabara ya Kawawa eneo la Magomeni ambapo lori hilo kabla ya kuanguka liligonga malori mengine. mashuhuda wanasema kwamba ajali hiyo ilisababishwa na kukatika breki kwa lori hilo. Dereva wa lori alitimua mbio baada ya ajali (Habari hii inapatikana pia katika gazeti la Majira la leo). Lori la kubeba takataka linaloonekana pichani kulia, lina mapungufu mengi lakini bado lipo barabarani na hakuna anayeonekana kushtuka hadi yatokee madhara kama yaliyotokea katika ajali ya leo.
Kwa muda mrefu kumekuwa na kilio cha wananchi kuhusu haya malori ya taka, kama sio yote ailimia kubwa ni mchakavu na mabovu ambapo kuyaona yakipita mbele ya askari wa usalama barabarani bila hata kuulizwa ni kitendawili kisichokuwa na jibu. Nafikiri ni lazima wito wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda uzingatiwe maana kumekuwa na ajali nyingi kutokana na uzembe, iwapo sheria zingezingatiwa maisha ya watu na mali vingeokolewa.

Saturday, February 14, 2009




Picha hapo juu zinaonyesha majeruhi wa ajali iliyotokea usiku wa kuamkia jana katika eneo la St. Peters Barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es salaam (Picha kwa hisani ya Nifahamishe.com)


AGONGWA NA KUFA PAPO HAPO!

Mwendesha pikipiki ,yenye namba za usajili T 831 AVN, Rajab Said (31) amefariki baada ya kugongwa na gari katika barabara ya Mbande jijini. Abiria aliyekuwa amebebwa katika pikipki hiyo aliyejulikana kwa jina la Mohamed Said alijeruhiwa vibaya sana. Gari lililosababisha nii aina ya Toyota Corolla yenye namba za usajili T956 ADQ lililokuwa likiendeshwa na Ramadhani Kapata(32) akitokea Chamazi kwenda Mbagala. Hiyo ni kwa mujibu wa Taarifa ya Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Emannuel Kandihabi.
katika tukio jingine, Kamanda wa Mkoa wa kipolisi Ilala,Faustine Shilagile, alitoa taarifa kwamba Kulwa Lucas au Lugame mkazi wa mtoni sabasaba alikufa papo hapo baada ya kugongwa na gari akijaribu kuvuka barabara. Ajali ilitokea jana majira ya saa 1.30 usiku katika barabara ya Nyerere katika njia panda ya Jet.

AJALI! AJALI! AJALI!

Hii ni wiki ambayo imepambwa na matukio ya ajali kama ilivyokuwa wiki iliyopita. Ndani ya wiki, kuanzia tarehe 7 Februari hadi kufikia leo ambapo watu wanaadhimisha siku ya wapendao ni mengi yametokea na si vibaya kama tukiyaangalia kwa makini na kutafakari kama ajali zinaashiria kupungua au kuongezeka hapa nchini.

Kama kawaida timu ya Mr. Bobos Class imekuwa ikipitia Taasisi ya Tiba ya Mfupa(MOI) ili kungalia majeruhi waliopokelewa katika Taasisi hiyo. kwa Mujibu wa Taarifa za Ofisa Mawasiliano wa MOI Bwana Jumaa Almasi, ndani ya wiki inayoishia leo, wamepokea majeruhi zaidi ya 50 na wengi wao wameruhusiwa baada ya kupata matibabu na baadhi waliokuwa na majeraha makubwa walilazwa. aliwataja baadhi ya majeruhi kuwa ni: Athumani Ramadhani(40) aliyevujika mguu, Mathias Juma(33) aliyepata ajali na kusagika mkono kutoka kimbiji, Castory Mussa(19) aliyevunjika mfupa wa paja na Eric Nyaonga kutoka Bagamoyo aliyevunjika mfupa wa paja na kupata maumivu ya kichwa.

Wengine ni:Michael Samwel Miyoyi(39), aliyepokelewa kutoka Hospitali ya Amana akiwa amepata majeraha mwilini na maumivu ya kichwa, Peter Sylvester(54) aliyepokelewa kutoka Hopsitali ya Tumbi, Kibaha akiwa amepata aliyeumia kichwa, Ahmed kandoro (23) aliyepata maumivuu ya kichwa, Joseph Mpanda aliyevunjika mguu chini ya goti na Joseph Robert (36) aliyepelekwa na polisi kutoka Temeke akiwa amevunjika mguu wa kushoto sehemu ya paja.

Kufuatana na Taarifa ya Bw. Almasi, wodi za MOI kwa sasa hivi zimejaza wagonjwa kuliko uwezo wake kutokana na kupokea majeruhi wengi sana.

Bwana Almasi alimaliza kwa kutoa ushauri kwamba, wakati huu ambao watu wengi wanasherehekea Siku ya Wapendanao "Valentine Day", ni vema watu wote wakazingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali zisizo za lazima, kwani kwa muda mrefu imeonekana Wakati wa sikukuu kama hizi ajali huongezeka sana.

Wakati huo huo, taarifa zilizotoka katika gazeti la majira zilieleza kwamba askari mmoja amekamatwa na vitu vinavyoaminika kuwa vya wizi vilivyopatikana kwa majeruhi wa ajali, jambo ambalo linasikitisha sana kwani kumekuwa na malalamiko sehemu mbalimbali za nchi kwamba kuna watu ambao baada ya tukio la ajali wao hufanya kazi ya kuwapora majeruhi na maiti. lakini la askari amabaye anatakiwa kulinda usalama, kukutwa na vitu kama hivyo inashtua sana.
Gazeti la Alasiri jana na leo limeripoti kuhusu ajali mbalimbali. ajali ya jana ni ile iliyopelekea watu 6 kufa papo hapo na leo Alasiri limeripoti kwamba lori aina ya scania lenye namba za usajili T110 AAG na tela lenye namba T 773AEA lilokuwa likitokea Rufiji kueleka Dar es salaam liliacha njia , kupinduka na kusababisha vifo vya watu watatu kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa polisi Mkoa wa Pwani Absalom Mwakyoma. Pia alieleza kwamba, katika ajali nyingine gari aina ya Toyota Landcruiser lenye namba T354 AEC lilimgonga mwendesha baiskeli mmoja ambaye alifariki baada ya kufikishwa Hospitali ya Tumbi. Aidha alieleza zaidi kwamba katika eneo la Ubena Zomozi gari lenye namba T 932 AGK lilimgonga kijana anayeitwa Simon Kaluna (22) na kufa papo hapo.

Saturday, February 7, 2009

SUMATRA YAANZA KUNG'ATA

Mamlaka ya Usafirishaji Majini na Nchi Kavu(SUMATRA) wameanza zoezi la operesheni ya kuondoa magari madogo ya abiria au "vipanya" katikati ya jiji la Dar es salaam ambayo leseni zake zimeisha muda.
Kwa mujibu wa Afisa mwandamishi wa Mamlaka hiyo Bwana Walukani Luhamba, wame amua kufanya zoezi hilo pamoja na kukamata magari mengine yenye makosa mbalimbali kama vile kukatisha ruti, kutoza nauli za juu, kunyanyasa wanafunzi, sare chafu na lugha chafu.
Katika kamata kamata hiyo magari 100 yameshakamatwa na wamiliki wake watatozwa faini kwa mujibu wa sheria. Mr. Bobos Class tunapongeza jitihada hizo kwani tuna imani kwamba itasaidia kupunguza ajali zisizo za lazima.(habari kwa hisani ya dullonet.com)

MTOTO AGONGWA NA KUFARIKI

Mtoto mwenye umri wa miaka 7, mwanafunzi wa darasa la kwanza Osama Hamidu amegongwa na gari na kufariki. Kamanda wa polisi Mkoa wa Temeke, Emmanuel Kandihabi alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 1.30 asubuhi katika barabara ya Kilwa eneo la Mbagala rangi tatu jijini Dar es salaam. Alisema maiti ya mtoto huyo imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Amana.
Dreva wa gari lililo mgonga mtoto huyo, Mustafa Saidi(52) anashikiliwa na polisi.

AJALI ZAIDI, VIFO ZAIDI!

Taarifa zilizopatikana jioni hii zinasema kwamba taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) impeokea waogonjwa wanne ambao wamelazwa kufuatia ajali zilizotokea jana na leo alfajiri. Waliopokelewa jana ni Mwema Nicolaus (27) ambaye amepata maumivu ya kichwa na Kajim Ally(22) ambaye alivunjika mkono wa kulia. Waliopokelewa alfajiri leo hii ni Abdulrahman Shiloo(34) aliyevunjika mguu na Mudhihir Ubagala(35) ambaye amevunjika mfupa wa paja. Afisa Uhusiano wa MOI, Bw. Jumaa Almasi amethibitisha kuwapokea wagonjwa hao.
Wakati huo huo, imeripotiwa kwamba ajali 384 zilua watu 58 na kujeruhi 487 mkoani Kigoma mwaka jana. Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana nifahamishe.com zikimnukuu Mkuu wa polisi Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kigoma SSP Said Mbaga. Hii ni kutokana na ajali 211 zilizosababisha majeruhi 487 na ajali za kawaida 121.
SSP SMbaga alisema kuanzia Januari 2009 mpaka mwezi huu wa February kumekuwa na jumla ya ajali 18 ambapo mtu 1 amepoteza maisha. mbali na hayo imefahamika kwamba kesi 68 za makosa mbalimbali ya usalama barabarani zilifikishwa mahakamani, kati ya hizo 33 wahusika walitiwa hatiani na nyingine 31 bado zinasikilizwa.
Hapo jana nifahamishe.com ilitoa habari ya ajali iliyohusisha magari yapatayo saba iliyotokea katika barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam imesababisha vifo na majeruhi kadhaa waliokimbizwa hospitali wengine wakiwa katika hali mbaya sana
Ajali hiyo imetokea leo asubuhi, maeneo ya Kimara Bucha katika barabara ya Morogoro ambayo inasemekana gari aina ya RAV 4 kupinduka, pia yakiwemo mabasi mawili ya daladala aina ya Isuzu Jorney na Toyota Hiace.Mengine yaliyohusika katika ajali hiyo ni Toyota LandCruiser, Toyota Hilux, Nissan Patrol na RAV 4 ambayo yote yalikuwa yakitokea Mbezi kuelekea Mjini.Inasemekana kuwa gari moja kati ya hayo lilileta hitilafu ya breki barabarani na kusababisha kutoweza kusogea pembeni ndilo lililosababisha mengine sita yaliyo nyuma yake kulivaa na kugongana kimpigo.
Katika Mtandao huo leo hii kuna taarifa kwamba mtu mmoja amefariki dunia baada ya kugongwa na kusagwasagwa na treni wakati alipopitiwa na usingizi katikati ya reli ya Tazara eneo la Ukonga jijini Dar es Salaam.
Mr. Bobos Class tunasikitika sana kufuatia ongezeko la ajali hapa nchi na kusababisha vifo kadhaa na uharibifu wa mali unaosababisha hasara kubwa.

Thursday, February 5, 2009

WANNE WALAZWA KWA AJALI MOI

Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) leo imepokea usiku wa kuamkia leo wamepokea wagonjwa wa ajali wanne kwa mujibu wa Afisa Uhusinao wa Taasisi hiyo. Waliopokelewa ni Sefu Lenjeka(42) ambaye alipokewa MOI kutoka Hopitali ya Mwananyamala ambaye aliumia kichwa (Mild Head Injury), mwingine ni Charles Lupande(19) aliyevunjika mfupa wa paja(femur), Juma Mwadia(29) ambaye alipokelewa kutoka Hopitali ya Amana na kuumia mguu wa kulia, na wa mwisho ni Michuzi Chande ambaye amefahamika kuwa ni mgonjwa wa akili ambaye aligongwa na gari na kuumia mguu wa kulia na kupata maumivu ya kichwa (head injury) hali iliyosababisha apokewe kama mgonjwa asiyetambulika (unknown male) lakini baadaye alitambuliwa na ndugu.

Sunday, February 1, 2009

MAISHA ZAIDI YATEKETEA!

Wiki inayoishia leo zimetokea ajali ambazo zimeteketeza maisha ya wananchi kadha na kuwaacha wengi wakiwa majeruhi.
kwa kujibu wa gazeti la "Habari Leo" la tarehe 31 Januari 2009, lilikuwa na kichwa kisemacho "Ajali zaua watu 15", watu 15 walikufa katika ajali zilizohusisha magari na treni katika mikoa ya Daresalaam na Morogoro huku zikiacha majeruhi zaidi ya 20.
Katika ajali hizo mbili iliyotokea Dar es salaam watu 9 walikufa papo hapo na wengine 10 kujeruhiwa na ajali ilitokea maeneo ya Jet Club, Kipawa barabara ya Nyerere, wakati Morogoro watu 6 walikufa papo hapo na wengine 10 kujeruhiwa katika ajali ya treni ya Kampuni ya Reli Tanzania(TRL).
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, inaonekana kwamba ajali zote zilisababishwa na uzembe wa madereva. Dreva wa dalala lenye namba za usajili T700 Toyota Hiace "kipanya" lililoua watu 9, aliligonga lori lenye namba za usajili T452 ACP ambalo lilikuwa limepinduka. Inasemekana "kipanya" kilikuwa kinafanya safari za usiku tu kutokana na leseni yake kumaliza muda wake.
Kwa kweli inasikitisha kuona kwamba, wakati jitihada za makusudi zinafanywa na wadau mbalimbali ili kuokoa maisha na mali za wanaopata ajali, bado kuna wachache ambao wanafanya uzembe wa makusudi na kurudisha nyuma jitihahada zote hizo.
Mr. Bobos Class tunaamini kwamba sheria itachukua mkondo wake na wale wote watakaobainika kuwa na makosa ya uzembe watachukuliwa hatua kali za kisheria.
blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker