Saturday, February 7, 2009

AJALI ZAIDI, VIFO ZAIDI!

Taarifa zilizopatikana jioni hii zinasema kwamba taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) impeokea waogonjwa wanne ambao wamelazwa kufuatia ajali zilizotokea jana na leo alfajiri. Waliopokelewa jana ni Mwema Nicolaus (27) ambaye amepata maumivu ya kichwa na Kajim Ally(22) ambaye alivunjika mkono wa kulia. Waliopokelewa alfajiri leo hii ni Abdulrahman Shiloo(34) aliyevunjika mguu na Mudhihir Ubagala(35) ambaye amevunjika mfupa wa paja. Afisa Uhusiano wa MOI, Bw. Jumaa Almasi amethibitisha kuwapokea wagonjwa hao.
Wakati huo huo, imeripotiwa kwamba ajali 384 zilua watu 58 na kujeruhi 487 mkoani Kigoma mwaka jana. Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana nifahamishe.com zikimnukuu Mkuu wa polisi Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kigoma SSP Said Mbaga. Hii ni kutokana na ajali 211 zilizosababisha majeruhi 487 na ajali za kawaida 121.
SSP SMbaga alisema kuanzia Januari 2009 mpaka mwezi huu wa February kumekuwa na jumla ya ajali 18 ambapo mtu 1 amepoteza maisha. mbali na hayo imefahamika kwamba kesi 68 za makosa mbalimbali ya usalama barabarani zilifikishwa mahakamani, kati ya hizo 33 wahusika walitiwa hatiani na nyingine 31 bado zinasikilizwa.
Hapo jana nifahamishe.com ilitoa habari ya ajali iliyohusisha magari yapatayo saba iliyotokea katika barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam imesababisha vifo na majeruhi kadhaa waliokimbizwa hospitali wengine wakiwa katika hali mbaya sana
Ajali hiyo imetokea leo asubuhi, maeneo ya Kimara Bucha katika barabara ya Morogoro ambayo inasemekana gari aina ya RAV 4 kupinduka, pia yakiwemo mabasi mawili ya daladala aina ya Isuzu Jorney na Toyota Hiace.Mengine yaliyohusika katika ajali hiyo ni Toyota LandCruiser, Toyota Hilux, Nissan Patrol na RAV 4 ambayo yote yalikuwa yakitokea Mbezi kuelekea Mjini.Inasemekana kuwa gari moja kati ya hayo lilileta hitilafu ya breki barabarani na kusababisha kutoweza kusogea pembeni ndilo lililosababisha mengine sita yaliyo nyuma yake kulivaa na kugongana kimpigo.
Katika Mtandao huo leo hii kuna taarifa kwamba mtu mmoja amefariki dunia baada ya kugongwa na kusagwasagwa na treni wakati alipopitiwa na usingizi katikati ya reli ya Tazara eneo la Ukonga jijini Dar es Salaam.
Mr. Bobos Class tunasikitika sana kufuatia ongezeko la ajali hapa nchi na kusababisha vifo kadhaa na uharibifu wa mali unaosababisha hasara kubwa.

No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker