Saturday, February 14, 2009

AJALI! AJALI! AJALI!

Hii ni wiki ambayo imepambwa na matukio ya ajali kama ilivyokuwa wiki iliyopita. Ndani ya wiki, kuanzia tarehe 7 Februari hadi kufikia leo ambapo watu wanaadhimisha siku ya wapendao ni mengi yametokea na si vibaya kama tukiyaangalia kwa makini na kutafakari kama ajali zinaashiria kupungua au kuongezeka hapa nchini.

Kama kawaida timu ya Mr. Bobos Class imekuwa ikipitia Taasisi ya Tiba ya Mfupa(MOI) ili kungalia majeruhi waliopokelewa katika Taasisi hiyo. kwa Mujibu wa Taarifa za Ofisa Mawasiliano wa MOI Bwana Jumaa Almasi, ndani ya wiki inayoishia leo, wamepokea majeruhi zaidi ya 50 na wengi wao wameruhusiwa baada ya kupata matibabu na baadhi waliokuwa na majeraha makubwa walilazwa. aliwataja baadhi ya majeruhi kuwa ni: Athumani Ramadhani(40) aliyevujika mguu, Mathias Juma(33) aliyepata ajali na kusagika mkono kutoka kimbiji, Castory Mussa(19) aliyevunjika mfupa wa paja na Eric Nyaonga kutoka Bagamoyo aliyevunjika mfupa wa paja na kupata maumivu ya kichwa.

Wengine ni:Michael Samwel Miyoyi(39), aliyepokelewa kutoka Hospitali ya Amana akiwa amepata majeraha mwilini na maumivu ya kichwa, Peter Sylvester(54) aliyepokelewa kutoka Hopsitali ya Tumbi, Kibaha akiwa amepata aliyeumia kichwa, Ahmed kandoro (23) aliyepata maumivuu ya kichwa, Joseph Mpanda aliyevunjika mguu chini ya goti na Joseph Robert (36) aliyepelekwa na polisi kutoka Temeke akiwa amevunjika mguu wa kushoto sehemu ya paja.

Kufuatana na Taarifa ya Bw. Almasi, wodi za MOI kwa sasa hivi zimejaza wagonjwa kuliko uwezo wake kutokana na kupokea majeruhi wengi sana.

Bwana Almasi alimaliza kwa kutoa ushauri kwamba, wakati huu ambao watu wengi wanasherehekea Siku ya Wapendanao "Valentine Day", ni vema watu wote wakazingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali zisizo za lazima, kwani kwa muda mrefu imeonekana Wakati wa sikukuu kama hizi ajali huongezeka sana.

Wakati huo huo, taarifa zilizotoka katika gazeti la majira zilieleza kwamba askari mmoja amekamatwa na vitu vinavyoaminika kuwa vya wizi vilivyopatikana kwa majeruhi wa ajali, jambo ambalo linasikitisha sana kwani kumekuwa na malalamiko sehemu mbalimbali za nchi kwamba kuna watu ambao baada ya tukio la ajali wao hufanya kazi ya kuwapora majeruhi na maiti. lakini la askari amabaye anatakiwa kulinda usalama, kukutwa na vitu kama hivyo inashtua sana.
Gazeti la Alasiri jana na leo limeripoti kuhusu ajali mbalimbali. ajali ya jana ni ile iliyopelekea watu 6 kufa papo hapo na leo Alasiri limeripoti kwamba lori aina ya scania lenye namba za usajili T110 AAG na tela lenye namba T 773AEA lilokuwa likitokea Rufiji kueleka Dar es salaam liliacha njia , kupinduka na kusababisha vifo vya watu watatu kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa polisi Mkoa wa Pwani Absalom Mwakyoma. Pia alieleza kwamba, katika ajali nyingine gari aina ya Toyota Landcruiser lenye namba T354 AEC lilimgonga mwendesha baiskeli mmoja ambaye alifariki baada ya kufikishwa Hospitali ya Tumbi. Aidha alieleza zaidi kwamba katika eneo la Ubena Zomozi gari lenye namba T 932 AGK lilimgonga kijana anayeitwa Simon Kaluna (22) na kufa papo hapo.

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker