Saturday, February 28, 2009

Mazingira Hatarishi kwa Watoto!Kwa kawaida maeneo ambayo yanatumiwa na watu wengi kama maeneo ya shule, misikiti na makanisa, ni vema yakiwa na "Alama za Kivuko cha Watembea kwa kwa Miguu" au "Zebra Crossing" ili kuepusha hatari ya wavukaji katika maeneo kama hayo kugongwa na magari yaendayo kasi. Pichani ni watoto wa shule waliokutwa Mkoani Morogoro wakivuka barabara bila mpangilio maalumu na hivyo kujiweka katika hatari ya kugongwa. Ni vema mamlaka husika zikazingatia hilo kwani watoto wengi wamepata athari, wamepoteza viungo au hata kupoteza maisha kutokana na kugongwa na magari yaendayo kasi. Watoto wanaoonekana pichani walipohojiwa, walisema kwamba wenzao wengi wameishagongwa na magari katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker