Sunday, March 1, 2009

Ajali Yaua Wawili na kujeruhi Kadhaa mjini Moshi!

Kwa mujibu wa habari iliyotolewa leo katika mtandao wa www.dullonet.com kama ilivyoandikwa na Hellen Mlacky kutoka Moshi inaeleza kwamba, wafungwa wawili wa gereza la Karanga mjini Moshi wamekufa papo hapo na wengine 15 kujeruhiwa vibaya wakiwamo askari magereza watatu, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka. Ajali hiyo ilitokea jana saa 8.45 mchana katika eneo la Kilimakyaro kata ya Mweka, wakati wafungwa hao wakitoka Uru Mweka, Moshi Mjini, kukata kuni kwa ajili ya kupikia chakula chao gerezani. Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Linus Sinzumwa, alisema ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Isuzu namba STG 1570 mali ya Magereza lililokuwa likiendeshwa na askari A7080 koplo Hamza(42). Kwa habari zaidi tembele www.dullonet.com/28.02.09_ajali_wafungwa.php


Wakati huo huo, Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imepokea majeruhi wa ajali mbalimbali wanne kutokea jana hadi leo saa 12 jioni. Waliopokelewa ni: Mwanaume mtu mzima ambaye hajatambulika alipokelewa majira ya saa 8 usiku kuamkia leo, akiwa ameumia kichwa kiasi cha kupoteza fahamu na kutojitambua. Pia amevunjika mguu wa kushoto. Mwingine ni Solomon Mduma(30) alipokelea saa 10 alfajiri akiwa ameumia kichwa baada ya ajali. Nyange kadefu(21) amepokelewa akiwa amevunjika mfupa wa paja. Alipokelewa MOI saa 7 mchana.wagonjwa wote hao wamelazwa katika wodi ya Sewa haji wodi Namba 17. Kwa upande wa wodi za kinamama,alipokelewa Suzanne Kipini kutoka kigamboni. Alipokelewa majira ya saa 11 jioni akiwa amevunjika mfupa wa paja. Na wa mwisho ni amina Saidi(28) ambaye alianguka na kuvunjika mguu akiwa anaendesha baiskeli huko chanika. Alipokelewa MOI jana saa 3.30 asubuhi. Afisa Uhusiano wa Taasisi hiyo alithibitisha kupokelewa kwa majeruhi hao na akaongeza kwamba, hali zao zinaendelea vizuri.


No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker