Sunday, March 1, 2009

Dereva Mwingine wa Pikipiki Auawa!

Habari iliandikwa na Chondoma Shabani katika mtandao wa www.nifahamishe.com jana tarehe inasema kwamba mwendesha pikipiki anayejishughulisha na kubeba abiria kupitia usafiri huo katika eneo la Kimara Suka ameuawa.
Kijana huyo anakadiriwa kuwa na miaka kati ya 14 hadi 16 ambaye anafahamika kwa jina moja la Solo aliuawa juzi majira ya usiku, wakati akiwa anampeleka mteja wake.Marehemu alikuwa ni dereva mwenye umri mdogo kabisa kuliko madereva wengine waliopo kituo hicho.Mmoja anayemfahamu marehemu wakati akizungumza na Nifahamishe alisema kuwa marehemu alikuwa ndio kwanza amemaliza darasa la saba mwaka jana na wazazi wake waliamua kumnunulia pikipiki hiyo ili aweze kujikomboa kimaisha.Inasemekana kuwa kama kawaida mteja alifika na kumtaka kijana huyo ampeleke sehemu husika na kijana huyo bila kujua kama ni mbaya wake alianza safari ya kumpeleka mteja wake huyo.Inasemekana kuwa mteja huyo alitaka ampeleke sehemu inayoitwa Golani nje kidogo ya Suka stendi.Ndipo mtu huyo ambaye hakuwa mwema kwake alipofika eneo ambalo aliona anaweza akafanya mauaji hayo alimtaka kijana huyo kusimamisha pikipiki.Inasemekana mtu huyo alitumia kisu kumuulia kijana huyo na kufanikiwa kuondoka na pikipiki hiyo.Baadhi ya mashuhuda walioenda eneo la tukio na kukuta maiti hiyo walisema kuwa marehemu alichomwa na kisu sehemu za kichwani na usoni,na kusababisha kifo chake.Pia walikuta kiatu kimoja ambacho inadaiwa kuwa mtuhumiwa alikiacha baada ya zoezi la mauaji kukamilika na kuondoka na pikipiki na kusahau kiatu hicho.Ndipo wasamaria wema walipokwenda kuripoti kituo cha polisi na maiti hiyo kwenda kuhifadhiwa hospitali ya Mwananyamala na kiatu kimechukuliwa ikiwa sehemu ya ushahidi wa mauaji hayo.Polisi wanaendelea na uchunguzi kuanzia leo kubaini nani amehusika na tukio hilo na kukifanyia kazi kiatu hicho kibainike ni cha nani.Katika hali isiyo ya kawaida kijana mwingine katika kipindi kisichopungua majuma manne ambaye pia alikuwa dereva wa pikipiki ameuawa na watu wasiofahamika kwa mtindo huohuo wa kukodishwa na hatimaye kuuawa.

No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker