Friday, March 20, 2009

SUMATRA Yazuia Vyombo Vidogo Vya Majini Kusafiri Usiku!




Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imepiga marufuku vyombo vidogo vya usafiri majini kusafiri usiku ili kupunguza ajali nchini.


sanjari na hilo, SUMATRA imepiga marufuku vyombo vidogo visivyo na mitambo (injini) kupakia abiria.


Mkurugenzi wa Usalama wa vyombo vya majini, King Chilagi aliyasema hayo juzi kwenye mkutano uliowakutanisha wamiliki, waendeshaji na wavuvi wa vyombo vidogovidogo uliofanyika katika bandari ya Bagamoyo Mkoani pwani.

Alisema SUMATRA imechukua hatua hiyo ili kukabiliana na wimbi la ajali za majini ambazo zinahusisha vyombo vidogo vidogo kutokana na vyombo hivyo kusafiri usiku vikiwa havina taa hali ambayo inasababisha kugongwa na vyombo vikubwa vya majini.

Alisema kuanzia sasa vyombo hivyo, licha ya kuzuiliwa kuanza safari zake usiku pia havitaruhusiwa kuondoka kabla ya kukaguliwa na kuruhusiwa na mkaguzi wa bandari husika baada ya kujiridhisha kuwa chombo kina vifaa vya kujiokolea pindi inapotokea ajali majini.

"Hivi sasa kila bandari ndogo atakuwepo mkaguzi atakayehakikisha chombo kinachoondoka bandarini kina vifaa vya kuokolea maisha ya watu (Life Jackets) pamoja na vyombo vya mawasiliano kama simu. Alisema chilagi(Mwananchi).

HOJA:Naamini hii ni hatua muhimu sana katika mapambano dhidi ya ajali ambazo zinachukua maisha ya watanzania kila kukicha. Ni vema kuzuia kuliko kusubiri mpaka yatokee maafa ya kutisha ndio hatua zichukuliwe. Lakini pia ni muhimu kuhakikisha kwamba, hili sio zoezi la siku mbili halafu watendaji wanalipuuzia, ni zoezi ambalo linalopaswa kufuatiliwa kila siku kama kweli tunathamini maisha ya watanzania. Kuna dhana iliyojengeka kwa watanzania wengi kwamba unapoanzisha udhibiti wa aina fulani, basi wale wanaohusika umewapa nafasi ya kujitajirisha.

No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker