Monday, March 23, 2009

GARI ZAWAFUATA PEMBENI NA KUWAGONGA!

Katika hali ya kusikitisha sana, Aisha Shabani mtoto wa miaka 12 leo amejikuta anafuatwa na gari pembezoni mwa barabara na kugongwa katika maeneo ya Tangi Bovu. Baba wa Aisha, Bwana Shabani Dadi, anasema kwamba akiwa na mwanae mara waliona gari linawafuata pembeni kwa kasi na mwanae alipokosa mwelekeo ndipo gari ikamgonga na kumvunja mguu. Amesema kwamba Aisha amelazwa wodi ya watoto ya Taasisi ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ajali Muhimbili (MOI).Aisha anasoma shule ya Msingi Kawe B. Gari iliyomgonga ina namba za usajili T 149 AQR saloon.
Mwingine ni Bwana Robert Masawe ambaye ameelezea tukio hilo kwamba, alikuwa anasubiri gari katika pembeni kabisa mwa barabara, daladala liliacha njia na kumfuata alipo na kumgonga. Robert aliteguka bega.
Mwisho ni Arumela Mwapalala(15) mkazi wa kimara alikuwa ana vuka barabara gari likamgonga ambapo alipata jeraha kubwa katika kidevu na kupoteza jino moja.alipata matibabu na kuruhusiwa kwenda nyumbani.
Afisa Uhusiano wa MOI Bwana Jumaa Almasi alisema kwamba, wagonjwa walifikishwa MOI na kupatiwa matibabu. Robert Masawe na Arumala waliruhusiwa , na Aisha alilazwa.

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker