Monday, March 9, 2009

13 wapoteza maisha,34 wajeruhiwa!

JINAMIZI la ajali limeendelea kuchukua roho za watu ambapo Mkoani Mbeya wilaya ya Tukuyu katika eneo la iduda, gari la abiria Toyota Hiace liligongwa kwa nyuma na lori na kwenda kujigonga katika lori jingine ambapo watu 4 walikufa papo hapo.Waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni watu 17.
Wakati huohuo, mkoa wa kusini Unguja watu 9 wamekufa katika ajali ambapo wanne walikufa papo hapo na wengine 17 kujeruhiwa.Ajali hiyo ilitokana na daladala mbili kukimbizana kwa mwendo wa kasi sana na hatimae zikakutana na gari aina ya Escudo, katika kukiwepa daladala moja iligonga mwembe.Dereva wa Escudo , Padre Anselmo Mwangamba ambye alinusurika japo gari lake liliharibiwa vibaya alisema,"ajali ilitokana na madereva wa magari mawili ya daladala kushindana kwa mwendo wa kasi, nilipotokeza na gari yangu walichanganyikiwa na katika jitihada za kunikwepa, daladala moja liligonga mti wa mwembe".
HOJA:Katika ajali zote mbili, imeonekana kwamba uzembe wa madereva umechangia kwa kiasi kikubwa. Je, tutakubali hadi lini maisha yetu kuchezewa na madereva wazembe?

No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker