Saturday, March 7, 2009

WAATHIRIKA WA AJALI WASIKATE TAMAA!




Waathirika wa ajali mbalimbali ambao wamepoteza viungo vyao, huhitaji vifaa kama hivi vya viungo bandia ili angalau kuwasaidia kufanya shughuli zao za kila siku kama walivyokuwa kabla ya kuathirika kwa ajali. Vifaa kama hivi hupatikana Taasisi ya Tiba ya Magonjwa ya Mifupa na Ajali(MOI) Mkoa wa Dar es salaam, hospitali ya KCMC Kilimanjaro na CCBRT mkoani Dar es salaam.
Viungo vya bandia huwasaidia waathirika wa ajali ambao wamepoteza viungo waweze kujisikia kama hawajapoteza kitu kwani huwasaidia kurudia maisha ya kawaida kwa kufanya shughuli zao mbalimbali. lakini wamekumbwa na matatizo kadhaa katika jitihada za kupata vifaa hivyo. Kwanza, waathirika wa ajali wapo nchi nzima, lakini Taasisi ambazo zinatengeneza vifaa hivyo kwa kiwango ni kama zilivyotajwa juu kwa hiyo mwathirika kutoka Lindi , Songea nk anahitajika kusafiri kutoka huko kwenda kuja Dar ili aweze kupata kifaa hicho ambapo wengi wao kupata nauli tu ni mtihani.Pili, gharama za vifaa ni kubwa kwa mwananchi wa kawaida. Kwa mfano, mguu uliokatwa chini ya goti ni shilingi 250,000 na juu ya goti si chini ya shilingi 500,000 za kitanzania.Kwa wananchi wengi hicho kiwango ni kikubwa sana. Kwa mfano nimeshuhudia msichana wa miaka 20 akitafuta mguu bandia kwa miaka2 bila mafanikio. Wengine hata magongo ya kutembelea(crutches) kabla ya kupata mguu bandia tayari ni tatizo na wameishia kutembea kwa kutumia vipande vya miti!
Idara ya ustawi wa jamii imeshindwa kuwasaidia kutokana na ukata, na mara nyingi wanapoenda huko huambiwa waache maelezo yao(particulars) halafu fedha ikipatikana watapewa taarifa! kwa hili hata mtoto mdogo atajua anadanganywa. Kwa maana nyingine ni kwamba kama anatoka Songea arudi huko halafu "Afisa" huyo atamtafuta!
KWA LEO NAOMBA WATANZANIA WENZANGU KAMA UNAJUA MAHALI AMBAPO TUNAWEZA KUWAELEKEZA HAWA WENZETU WAKAPATA MSAADA TAFADHALI WASILIANA NAMI, AU HATA KAMA WEWE UNAWEZA KUSAIDIA SI VIBAYA. CHONDE CHONDE TUWASAIDIE WATANZANIA WENZETU WANAOTAABIKA! NAWASILISHA!

No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker