Friday, March 27, 2009

ICCT WAGAWA VITABU VYA MILIONI 500!







Injury Control Center in Tanzania(ICCT) kwa kushirikiana na Canadian Network for International Surgery(CNIS) wametoa msaada wa vitabu 7719 vyenye thamani ya Dola za Kimarekani 420,480(zaidi Tsh Mil. 500). kulingana na maelezo ya Prof Lawrence Museru ambaye ni Mwenyekiti wa ICCT, vitabu hivyo vinagawiwa katika Taasisi mbalimbali hapa nchini zinazotoa elimu ya udaktari ambazo ni, Muhimbili University of Health and Allied Sciences(MUHAS), Herbert Kairuki University, Buhando University, Kilimanjaro Christian MEdical Center(KCMC) na Muhimbili Orthopeadic Institute(MOI). Mgao wa vitabu na thamani yake ni kama ifuatavyo; MUHAS USD 11,000, Bugando USD 73,500, Herbert Kairuki USD 68,532 na MOI USD 62,000.



Prof. Museru alisema kwamba vitabu hivyo vitasaidia sana kufundishia wanafunzi wanaosomea fani mbalimbali za udaktari kama tiba ya meno, mifupa, uuguzi,dawa ya usingizi n.k. ni vitabu vipya ambavyo si rahisi kuvipata hapa Tanzania na hata vikipatikana vitakuwa ni ghali sana.



Prof. Cassian Magori akitoa shukrani kwa niaba ya Taasisi zilizopata msaada huo, alisema kwamba wanashukuru kupata vitabu hivyo ambavyo vimeandika na mabingwa wa fani mbalimbali za tiba na ni vya miaka ya hivi karibuni. Aliongeza kwamba, watahakikisha kwamba vitabu vinatunzwa ili kuwasaidia wanafunzi katika vyuo vyao. Mwisho aliipongeza ICCT kwa kazi nzuri wanayofanya.



Mwenyekiti wa ICCT, prof. Museru alisema kwamba wao kama ICCT wanafanya jitihada kubwa kwa kutoa mafunzo kwa wanaotoa huduma kwa majeruhi mbalimbali na kwamba wamekuwa wakitoa mafunzo katika hospitali jinsi ya kuhudumia majeruhi wa ajali mbalimbali(madaktari na wauguzi), wahudumu wa vyumba vya dharura.Alisema mafunzo yameishafanywa katika hospitali za; Temeke, Mwananyamala,Tumbi-Kibaha, Mkuranga, Iringa, Morogoro na hivi karibuni yalifanyika Musoma. Pia alisema wameweza kutoa mafunzo ya jinsi ya kutoa huduma ya kwanza(First Aid) katika shule za msingi za Dar es salaam pamoja na madereva wa taxi, zimamoto na Polisi wa Usalama barabarani ili wajue nini cha kufanya kuokoa maisha ajali inapotokea.Pichani Prof. Museru akikabidhi vitabu na baadhi ya vitabu vikipakiwa katika gari.

PONGEZI: Mimi kama mdau wa kupambana na ajali zinazopoteza maisha ya watanzania kila kukicha, naipongeza ICCT kwanza kwa kutoa msaada huo na pili, kutoa mafunzo ya jinsi ya kuokoa maisha inapotokea jali kwa kutoa mafunzo ya utoaji wa hudma ya kwanza. ICCT Big up sana.

No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker