Monday, March 30, 2009

Waitaka Serikali Itumie Busara kukomesha Ajali!

Wamiliki wa mabsi ya abiria katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara wameijia juu serikali kwa kile wanachodai ni kucheza mchezo mchafu wa kuwafilisi kwa kuanzisha mipango ya kukurupuka ambayo haiwezi kudhibiti ajali nchini.

Wanachama wa chama cha wasafirishaji wa mikoa hiyo (AKIBOA) wamedai kuanzishwa kwa utaratibu wa mabasi yote kufunga kidhibiti mwendo ni mfano halisi wa maamuzi ya kukurupuka na sasa serikali imekuja na jambo jipya.

serikali kupitia Mamlaka ya udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imetoa muda wa miezi sita kufunga kifaa kingine mithili ya kile cha kudhibiti mwendo maarufu kama 'speed governor' lakini hiki kipya kinajulikana kama 'Tachograf' na kazi yake ni kutunza kumbukumbu za mwendo wa basi.

Kifaa hicho kinadaiwa kitagharimu sh. 1 milioni wakati kile cha Speed Governor ambacho kimeshindwa kudhibitia ajali kilifungwa kwa Sh. 600,000 kwa kila basi, uamuzi ambao unadaiwa ulikuwa mradi wa vigogo serikalini.

"Gavana tulifunga kwa Sh. 600,000 lakini ime-prove failure(imeshindwa) na roho za watanzania zimeendelea kuteketea na sasa wanakuja na kitu kingine mfano wa gavana" ,alilalamika Amoni Mlaki.

Mlaki aliipasha serikali kuwa dawa pekee ya kudhibiti ajali iliyokuwa na mafanikio tangu enzi za ukoloni za ukoloni ni kusimamiwa kikamilifu kwa vituo vya ukaguzi na kufuatwa kwa ratiba za mabasi(Mwananchi).

No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker