Sunday, March 8, 2009

Nauli Za Mabasi Zashushwa

Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Israel Sekirasa akiongea na vyombo vya habari amesema kwamba, nauli za mabasi yanayotoa huduma za usafiri mijini 'daladala' na yale yaendayo mikoani, zimeshushwa. Hii inafanya kilio cha wananchi kwa muda mrefu kuwa kimesikika.
Alisema daladala zitapunguza nauli kwa silimia 12 sawa na sh. 50 kwa Dar es salaam hivyo nauli itakuwa sh. 250 badala ya sh.300 wakati safari ndefu watalipa sh.550 badala ya 600.

Kwa nauli za mabasi yaendayo mikoani,nauli imepungua kwa asilimia 11 kwa mabasi ya kawaida yanayopita kwenye barabara za lami, hivyo kufanya nauli kuwa sh 26.60 kwa kilometa badala ya sh. 30. Barabara za zisizo za lami imeshuka kutoka sh. 37 kwa kilometa hadi sh. 32.70. Aliongeza kwamba, mabasi yenye hadhi ya juu nauli imeshushwa kwa asilimia 3 kutoka sh.42 kwa kilometa hadi sh. 40.70. Nauli za mabasi ya hadhi ya juu bei imeshushwa kwa asilimia 10 kutoka sh.52 kwa kilometa hadi sh. 46.40

Nauli mpya zitaanza kutumika Alhamisi ijayo.

No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker